CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA.
Demokrasia haijengwi kwa kuogopa mageuzi, wala haijengwi kwa fikra za kidumu au adumu. hatuwezi kujenga chama kwa kuabudu mtu au kijikundi ka watu, Hatuwezi kujenga chama kwa umaarufu au fedha za mtu. Chama kitajengwa kwa kufuata katiba na taratibu zilizowekwa. Na kamwe hakuna mwenye hati miliki ya chama hata waanzilishi, kwani chama ni watu na si jina la chama.
Wacheni uchaguzi ufanyike, hakuna sababu ya kuogopa ni nani anapeleka jina lake ilimradi hajavunja katiba na sheria za chama.Tuache wapiga kura waamue ni nani anayefaa.
Na kama chama kinataka kufyeka jina la mtu na kuwe na sababu ya msingi si ya kumlinda mgombea mmojawapo. Kufanya vizuri si kigezo cha kutopata upinzani, uwoga wa kupingwa na mabadiliko ndio yanayoifanya CCM kuendelea kuiba kura, kuwanunua wajumbe ya Tume ya Uchaguzi, na kutumia Polisi na usalama wa Taifa kudhibiti mageuzi. sasa mbona Chadema tunataka nasi kwenda huko huko?
Zitto ana sifa za kugombea uenyekiti kwa mujibu wa katiba, na Mbowe anasifa kugombea uenyekiti vilevile, basi tuachieni wapiga kura tuamue ni nani anatufaa zaidi kwani wote tunawahitaji. Waacheni waje watueleze wana nini cha kukifanyia Chama, tusiogope challenge.
Demokrasia ina gharama kubwa sana, na hii ni moja wapo, Tuache uchaguzi huu uende ili kujenga chama na si jina mtu, Chama hakitajengwa kwa umaarufu wa mtu mmoja mmoja bali kwa mikakati ya kisera na katiba, pale haya yanapoachwa na kufuta mtu mmoja mmoja mnaua chama.
Pendekezo, Zitto abakize jina lake pamoja na mbowe. Na mtu yeyote mwenye sifa achukue form demokrasia ifanye kazi, ni heri kuyazoe haya sasa kuliko kusubiri kwenye ulafi na umimi , ni heri kuyazoea sasa kuliko kujenga ukiritimba.
Chadema kumbukeni vijana wengi wasomi wapo nyuma ya chama kwa sababu wanaamini mabadiliko na utawala wa sheria na katiba, utawala usio waabudu watu wala kuwalinda, utawala unaoenzi demokrasia na usawa kwa wote, utawala ulio tayari kwa mabadiliko yenye manufaa kwa wengi na ujenzi wataifa.
Hekima haina shule, wala busara haina mwalimu, huzaliwa navyo.