Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Invisible,

Mwambie mzee Mtei wanachemsha BIG time. Hata sisi tunaotaka mabadiliko ndani ya CCM tunaona kama Chadema ni alternative sasa kama wanachemsha namna hii ni hatari!!!

Acheni u MKWE upinzani uimarike!!
 
Inaonekana Zitto akuwasiliana na Freeman kabla ya kuchukua form, mawasiliano kama haya hayaitajiki CCM kutokana na ukubwa wake, lakini kwa chama kama CHADEMA ambacho mihimili yake ni Freeman, Slaa na Zitto ni lazima wawasiliane kabla ya hayo maamuzi. Ndiyo ni demokrasia lakini inaonekana kuna vita ya chini chini kati ya Freeman na Zitto..

Usemi wa Zitto kwamba Freeman arudishe form ili kukinusuru chama ni dhairi kwamba hakubaliani na mwenyekiti wake na kunakurukupushani kati ya hao wawili.

Sidhani kama Kibanda angeweza kumshambulia Zitto bila kujua kuwa kuna mvutano kati ya Zitto na Freeman.....
 
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.

Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.

Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...

Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.

Katika hili, mmechemsha!

Huo ubinafsi wa kutaka kukaa kwenye uongozi miaka nenda miaka rudi ndiyo sababu kubwa ya hivi vyama vya upinzani kutokuwa na mikakati yoyote ya kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kuiondoa CCM madarakani. Kwa kuogopa kupoza nafasi za uongozi walizokuwa nazo, wako radhi wabaki kwenye uongozi wa vyama vyao dhaifu badala ya kuwa mstari wa mbele kuunda chama kimoja chenye nguvu.
 
Huu ni mtihani mkubwa sana kwa CHADEMA, itajitenga ama kujibomoa kwa kutofuata misingi midogo ya demokrasia, uhuru wa kumua na uhuru wa kujieleza, kugombea na kuchaguliwa. Hazina kubwa ya CHADEMA ni vijana wasomi wenye nia ya kuleta mabadiliko, sasa hili la kung'ang'ania Mbowe awe mwenyekiti milele linanipa shida. Wazee wa CHADEMA ushauri wenu umesikika wacheni Zitto agombee silazima ashinde ...sasa manapohisi anatumika kwa kunufaisha CCM...hili halina maana ...mbona Mbowe naye anahusishwa na ufisadi?

Nafikiri mara mbili uanachama wangu CHADEMA!


sasa wewe ndugu yangu Masa. Unaipenda Chadema huku haumsapoti mgombea wake Kyela?!!! unamsapoti Mwakyembe ambaye ni CCM!

Mzee kuwa na MSIMAMO
 
sasa wewe ndugu yangu Masa. Unaipenda Chadema huku haumsapoti mgombea wake Kyela?!!! unamsapoti Mwakyembe ambaye ni CCM!

Mzee kuwa na MSIMAMO

Philosophy yangu mzee huwezi ijua ndugu yangu! Ni mwanachama wa CHADEMA lakini huwa nasupport zaidi mgombeaji yeyote ambaye analeta mabadiliko ya kweli.....Acha Mwakyembe wapo wengi wa CCM ninao wakubali....Kilango, Seleli, Kimaro etc...siko rigid na chama hata kama mgombea ni boomu! Mwakalinga hafai
 
Hicho chama cha Wachaga na wakwe zao. Zitto mtu wa bara huko hawawezi kumruhusu aongoze hicho chama.

Wangwe alijitahidi lakini akaishia kufa.

Pole sana Zitto; ndio siasa za TZ hizo.
 
..Chadema wafanye kila linalowezekana kuondoa dhana kwamba Wachaga na Wakristo ndiyo wenye sauti ndani ya chama hicho.

..sasa kama wamemzuia Zitto asigombee nadhani watakuwa wanatoa nafasi ya mashambulizi makubwa zaidi.

..kama ni kweli Zitto ameamua kuondoa jina lake bila shinikizo lolote, halafu anataka Mbowe naye aondoe jina lake, kwa kweli tutakuwa na haki ya kuutilia mashaka uwezo wake[zitto] wa kufikiri.
 
Hicho chama cha Wachaga na wakwe zao. Zitto mtu wa bara huko hawawezi kumruhusu aongoze hicho chama.

Wangwe alijitahidi lakini akaishia kufa.

Pole sana Zitto; ndio siasa za TZ hizo.


Nimekubaliana na wewe ila sio kwa Mwakalinga!! alikuchukulia DEMU wako nini mlipo kuwa High school???? unamuota kila mara!!!
 
I am completely perplexed and annoyed by this move.

Who ever is behind this move, we probably had underestimated his/her strength in dismantling the costly molded 'alternative' to the ruling elite.

This will bring shame not only to the opposition, but to the country as a whole and thus casting serious doubts to our readiness to practice the so called multi-party system.
 
CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA.
Demokrasia haijengwi kwa kuogopa mageuzi, wala haijengwi kwa fikra za kidumu au adumu. hatuwezi kujenga chama kwa kuabudu mtu au kijikundi ka watu, Hatuwezi kujenga chama kwa umaarufu au fedha za mtu. Chama kitajengwa kwa kufuata katiba na taratibu zilizowekwa. Na kamwe hakuna mwenye hati miliki ya chama hata waanzilishi, kwani chama ni watu na si jina la chama.

Wacheni uchaguzi ufanyike, hakuna sababu ya kuogopa ni nani anapeleka jina lake ilimradi hajavunja katiba na sheria za chama.Tuache wapiga kura waamue ni nani anayefaa.

Na kama chama kinataka kufyeka jina la mtu na kuwe na sababu ya msingi si ya kumlinda mgombea mmojawapo. Kufanya vizuri si kigezo cha kutopata upinzani, uwoga wa kupingwa na mabadiliko ndio yanayoifanya CCM kuendelea kuiba kura, kuwanunua wajumbe ya Tume ya Uchaguzi, na kutumia Polisi na usalama wa Taifa kudhibiti mageuzi. sasa mbona Chadema tunataka nasi kwenda huko huko?

Zitto ana sifa za kugombea uenyekiti kwa mujibu wa katiba, na Mbowe anasifa kugombea uenyekiti vilevile, basi tuachieni wapiga kura tuamue ni nani anatufaa zaidi kwani wote tunawahitaji. Waacheni waje watueleze wana nini cha kukifanyia Chama, tusiogope challenge.

Demokrasia ina gharama kubwa sana, na hii ni moja wapo, Tuache uchaguzi huu uende ili kujenga chama na si jina mtu, Chama hakitajengwa kwa umaarufu wa mtu mmoja mmoja bali kwa mikakati ya kisera na katiba, pale haya yanapoachwa na kufuta mtu mmoja mmoja mnaua chama.

Pendekezo, Zitto abakize jina lake pamoja na mbowe. Na mtu yeyote mwenye sifa achukue form demokrasia ifanye kazi, ni heri kuyazoe haya sasa kuliko kusubiri kwenye ulafi na umimi , ni heri kuyazoea sasa kuliko kujenga ukiritimba.

Chadema kumbukeni vijana wengi wasomi wapo nyuma ya chama kwa sababu wanaamini mabadiliko na utawala wa sheria na katiba, utawala usio waabudu watu wala kuwalinda, utawala unaoenzi demokrasia na usawa kwa wote, utawala ulio tayari kwa mabadiliko yenye manufaa kwa wengi na ujenzi wataifa.

Hekima haina shule, wala busara haina mwalimu, huzaliwa navyo.
 
mie si chadema,lakini huu utamaduni umeanza lini ? watu wachache kuamua kupindisha misingi ya demokrasia ..We are tired of waiting for freedom, we want freedom now, tomorrow it will be so far,we will meet Mbowe at cross road and will tell him what we want....
 
..
..kama ni kweli Zitto ameamua kuondoa jina lake bila shinikizo lolote, halafu anataka Mbowe naye aondoe jina lake, kwa kweli tutakuwa na haki ya kuutilia mashaka uwezo wake[zitto] wa kufikiri.

Article ya Kibanda ilitosha kuwa shinikizo kwa Zitto...Kibanda si Mtu mdogo...kama alivyosema kuwa yeye yu karibu na wote watatu...!!!

Wazee wanajua ukiruhusu Mbowe kuwa na Mpinzani...unaleta uncertainity ambayo kwa sasa hawajajiandaa kuipokea...anything can happen!!!

Zitto anafahamika kwa ushawishi....UDSM alikuwa kila ukitokea Mgomo yeye lazima asimamishwe chuo hata kama hayumo ktk Uongozi...!!!
 
Last edited:
Binafsi sikupenda Jazba za Kibanda za kuwaita Vijana "Wajinga" Hasa wale wanaonekana ni "Wasomi"...kama Mbowe ameipitia hio article alitakiwa amsimamishe "kazi" km hakuomba radhi ndani ya 24hrs...!!

Hii vita ni baina ya wale "Waliokikuza na Kukilea Chama"...na wale wanaokuja kuja kula "Matunda ya Chama
 
Zitto mwisho atakwenda ccm,chadema wanampa more than one reason ya kwenda ccm,immature politics za tanzania bwana as if ni maigizo.......
 
Zitto mwisho atakwenda ccm,chadema wanampa more than one reason ya kwenda ccm,immature politics za tanzania bwana as if ni maigizo.......

Zitto hawezi kwenda CCM....kama ikitokea kutoka Chadema basi ataachana na Siasa kwa wakati huu....hadi hapo Hali ya Mageuzi ya Kweli yatakapotokea...!!!
 
Binafsi sikupenda Jazba za Kibanda za kuwaita Vijana "Wajinga" Hasa wale wanaonekana ni "Wasomi"...kama Mbowe ameipitia hio article alitakiwa amsimamishe "kazi" km hakuomba radhi ndani ya 24hrs...!!

Hii vita ni baina ya wale "Waliokikuza na Kukilea Chama"...na wale wanaokuja kuja kula "Matunda ya Chama
Kuna mdau mmoja alisema Kibanda aliomba radhi kwakuwa aliandika akiwa katika mood mbaya, very sorry sijasoma ni wapi kaandika hivyo lakini kama ni kweli basi ni uungwana, maanake haya maandishi yanadumu ati.
 
Kuna mdau mmoja alisema Kibanda aliomba radhi kwakuwa aliandika akiwa katika mood mbaya, very sorry sijasoma ni wapi kaandika hivyo lakini kama ni kweli basi ni uungwana, maanake haya maandishi yanadumu ati.

Wengi tuwagumu kuombana radhi...
 
Binafsi sikupenda Jazba za Kibanda za kuwaita Vijana "Wajinga" Hasa wale wanaonekana ni "Wasomi"...kama Mbowe ameipitia hio article alitakiwa amsimamishe "kazi" km hakuomba radhi ndani ya 24hrs...!!

Hii vita ni baina ya wale "Waliokikuza na Kukilea Chama"...na wale wanaokuja kuja kula "Matunda ya Chama

Chuma hakuna anayekuja kula matunda.Zitto yuko Chadema muda wote toka akiwa 16 years old.

alichokifanya Kibanda ni kummaliza Zitto kwa makala ile. hii gea ya kudai kuwa kaomba radhi ni ujanja baada ya kuona Mbowe watu wanamueleza kuwa Kibanda anafanya kazi ya kukigawa chama kwa kampeni chafu.lazima Kitila na kundi lao wamekosa na watakosa amani daima kwa maneno ya KIBANDA.

MAANDISHI YA KIBANDA LEO AMEJIFANYA YUKO PAMOJA NA ZITTO BAADA YA KUONA KUNA PLAN B YA KUMZUIA ZITTO.

KUMZUIA ZITTO NDIO WAMECHOCHEA MGOGORO KWANINI WAZEE WANNE WAWANYIME HAKI WAJUMBE NA WANACHAMA WOTE?

MBOWE ALISEMA HATAKI KUGOMBEA KALAZIMISHWA NA WAZEE,KWANINI WASIMKATE HUYU ASIYE NA NIA YAKUGOMBEA NA KUMUACHA ZITTO MWENYE NIA NA DHAMIRA YA KUWA CHAIRMAN?

KIBANDA HAWEZI KUSIMAMISHWA KAZI NA MBOWE ANAMUINGIZIA ZAIDI YA MILIONI MIA MBILI KWA MWEZI KWENYE GAZETI HILI. HUKU AKITUMIA WAANDISHI VIBARUA WASIOLIPWA VIZURI NA KUCHANGIA NSSF.

GAZETI HILI LINA CHART KUBWA KWA MICHANGO YA MAKALA ZA WATU MBALI MBALI KAMA KARUGENDO N.K, NA PIA KIBANDA ANATOA NAFASI KWA VYAMA VYA UPINZANI KAMA CUF KUWEKA HABARI ZAO HIVYO ANA KULA SOKA LA WANA CUF ZNZ NA BARA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom