Yaani mimi kwa kweli kuna vitu vinanishangaza sana awamu hii sijawahi kuona awamu yenye uoga na isiyojiamini kama hii, miaka yote iliyopita uoga kama huu haukuwepo, upinzani uliachwa ufanye siasa na mikutano vyombo vya habari vilipewa nafasi kufanya kazi yake.
Lakini kipindi hichi pamoja na awamu hii kutuletea maendeleo Watanzania na watanzania kuonekana kumpenda jpm kupitiliza, ila jamaa ni muoga kupitiliza.
Sasa kama unaamini unapendwa unaanzaje kuwa muoga namna hii, mitandao tokea jana haieleweki, wewe unasema unapendwa basi usiwe muoga, ukiwa muoga inamaana watu hawana imani na wewe na unaujua ukweli.