Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mitandao ya Twitter, WhatsApp, YouTube na Telegram haipatikani kupitia baadhi ya mitandao ya simu

Sitaki hata kuwachosha maana muda nao ni mali, kila nikipita twitter naona haifunguki na sio kawaida kila browser nayotumia wapi, huko kwako unaonaje? ama kuna mambo nyuma ya dunia yanaendelea?

Tumia vpn
 
Watumiaji wa mtandao wa twitter wanashindwa kupata huduma hiyo kupitia kampuni ya simu ya Vodacom. Tatizo hilo limeanza siku ya leo.
Haya ni mambo ya kihanithi kabisa. Lakini hakuna kurudi nyuma! πŸ’ͺ🏽πŸ’ͺ🏽πŸ’ͺ🏽
 
Tutaelewana tu ngoja kwanza tuonyeshane makali, CCM watachia tu watu washachoka kama mbwae mbwae tu mwaka huu
 
Mkuu elekezeni wadau hatua kwa hatua jinsi zinavyofanya kazi..
Nenda playstore pakua proton VPN, kisha fanya registration kwa kujaza emails na password, kumbuka kubonyeza kitufe cha free,ili utumie bure kwa muda fulani. Kisha utatumiwa ujumbe kupitia email yako utaverify, ndio utaanza kutumia

Utaletewa unataka uaccess internet kutoka nchi gani ziko nyingi mm natumia ya Netherland, ukitaka ata USA ni wewe

Hapo utaweza ku bypass huu utopolo wa internet ya kupangiwa na vodacom. Sio tu Twitter, kesho internet inazimwa nchi nzima. Maana hata sasa haifanyi kazi vizuri
 
Mtandao wa twitter..kwa hapa Nchini umekuwa upo slow na asubuhi hii umegoma kabisa kufanya kazi.. what's happening!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…