Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mitandao ya Twitter, WhatsApp, YouTube na Telegram haipatikani kupitia baadhi ya mitandao ya simu

Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mitandao ya Twitter, WhatsApp, YouTube na Telegram haipatikani kupitia baadhi ya mitandao ya simu

Watumiaji wa mtandao wa twitter wanashindwa kupata huduma hiyo kupitia kampuni ya simu ya Vodacom. Tatizo hilo limeanza siku ya leo.
Mimi natumia eatel pia ni takribani saa 9 zimepita toka niweze kupata taarifa mpya baada ya hapo hakuna kitu
 
Sababu huko ndio kuna targeted accounts za activist na ndio mtandao unaotegemewa kwa taarifa nyingi kwa sasa mingine imebaki soga tu na umbea..
 
Read between the lines. Si kila kitu kinaanikwa hadharani ili kuficha lengo lao kuu.
Bulk massaging and bulk voice calling, nikajua ni zile jumbe tunazotumiwa kutoka taasisi, mashirika, mbali mbali, mf: TAMISEMI, TAKUKURU, POLISI, TMA lengo kufikisha ujumbe au taarifa flani.

au simu inaweza ikaita ukapokea ukakuta nitangazo,taarifa au ujumbe flani.
 
Now naona telegram inasumbua pia...! Vp whatsapp iko sawa wenye mnaitumia..? Make Twitter mpaka utumie vpns, Na kuna baadhi ya vpn server zake ziko blocked...
 
Sitaki hata kuwachosha maana muda nao ni mali, kila nikipita twitter naona haifunguki na sio kawaida kila browser nayotumia wapi, huko kwako unaonaje? ama kuna mambo nyuma ya dunia yanaendelea?
Hii ni kweli..kwa watumiaji wa Vodacom Tanzania, Twitter haifunguki kabisa.

CCM na Magufuli ni coward sana.
Yapaswa wang'olewe madarakani kwa gharama yoyote ile.
 
Nenda playstore pakua proton VPN, kisha fanya registration kwa kujaza emails na password, kumbuka kubonyeza kitufe cha free,ili utumie bure kwa muda fulani. Kisha utatumiwa ujumbe kupitia email yako utaverify, ndio utaanza kutumia

Utaletewa unataka uaccess internet kutoka nchi gani ziko nyingi mm natumia ya Netherland, ukitaka ata USA ni wewe

Hapo utaweza ku bypass huu utopolo wa internet ya kupangiwa na vodacom. Sio tu Twitter, kesho internet inazimwa nchi nzima. Maana hata sasa haifanyi kazi vizuri
Wakizima kabisa hii VPN itasaidia au ndo habari yetu itakua imeishia hapo
 
Dahh Vpn inaraha mkuu.. Yaan nakata mbuga kwa ulaini kabisa tena iko fasta..

Vitu kuhusu ulaji wa mb (zinakwenda sana ukitafautisha na kawaida au vipi) ?
Sijachunguza kuhusu hilo
 
Back
Top Bottom