Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Waandishi wa habari wekeni pembeni mapenzi yenu kwa vyama vya siasa

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Waandishi wa habari wekeni pembeni mapenzi yenu kwa vyama vya siasa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, waandishi wa habari nchini wametakiwa kujiweka mbali na mapenzi ya chama chochote cha siasa ili waweze kufanya kazi bila kukutana na changamoto.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile, wakati anaongea na wanahabari kuelekea mkutano mkuu wa jukwaa hilo utakaokutanisha wahariri zaidi ya 100 kutoka kila kona ya nchi yetu.

Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kuingiza wanachama wapya 24, utendaji wa vyombo vya habari, uchumi wa vyombo vya habari, mabadiliko ya Teknolojia na ufatiliaji wa maadili, sheria na miiko ya uandishi wa habari

Chanzo: EATV

GbsPgBMaMAAmd3c.jpg
 
Back
Top Bottom