Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism


Nakubaliana na wewe lakini nilikuwa nanukuu ujenzi wa karne ya 13 na kurudi nyuma.

Walivyoweza kushinda mazingira waliendelea sehemu nyingine. Na vilevile nilikuwa nasisitizia kuhusu ugonjwa wa Malaria.

Kushindwa kupambana na magonjwa mengi kwa Tanzania kuna sababishwa na watu kutochagua maeneo mazuri ya kujenga makazi yao.

Malaria na kipindupindu ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa good planning kwa upande wa Goverment na individuals. Watu wanaoishi kwenye maeneo mazuri kiafya wataamka asubuhi na kufikiri wabuni nini kuhusu maisha yao. Na wale wanaoishi kwenye maisha duni, wataamka kufikiri ni jinsi gani wa-survive kabla jua kuzama.

Hivyo kwa kulinganisha, katika karne ya 13 wazungu walikuwa wanafanya juhudi za kuchagua sehemu gani wajenge. Wakati huku kwetu watu wanajenga hili wapate sehemu za kuishi tu na baadaye watafute tiba.
 
Zakumi,
Duh basi nchi kama Canada kila sehemu ni maji mkuu wangu miji yote iko kando ya ziwa, mito au bahari na huko kusikokuwa na maji ni mbuga tupu kuliko ile ya Dodoma Singida..Pamoja na yote haya malaria inaweza kabisa kuzuiwa hata Kipindupindu yote haya ni maradhi yanayotokana na uchafu.. ndio yale alosema Nyani Ngabu na uchafu unaolundikwa kila kona ya mji tukauza vyakula vyetu sehemu karibu na dampo hizo..
Kisha tunadai kuwa chakula cha pale kitamu kuliko mahotel makubwa mjini..
 


Ndio maana Ngabu anashinda kwenye mjadala huu bila kuponyeza keyboard yake.

Uvumbuzi wa Mwarobaini ulikuwa hauna reasoning yoyote. Inawezekana watu walitafuna majani ya miti mbalimbali kabla ya kupata nafuu kwa kutumia mwarobani. Hii ni trial and error method na haionyeshi ubunifu wowote hule.

Ubunifu unakuja pale mtu anapofanya kazi zake methodically na sio kucheza bahati nasibu.
 
Usinichekeshe miye weee!..
Unajua kahawa ilivumbuliwa vipi..
based on True story - Mtu mmoja (Ethiopia) alikuwa akichunga mbuzi wake wamechokaaa......sasa ikatokea wakala mbegu za mibuni muda mfupi wakaanza kuchangamka.. basi ikiwa kila siku lazima kuwalisha hizo mbegu hadi siku mzungu alipokuja na kuambiwa habari ile... mzungu katika kutafiti akaona kweli akaifanyia kazi..
Hivyo mbunifu hapa ni mbuzi, mwafrika alitazama na kufurahia kuwa mbuzi wake wanachangamka.. mzungu akaona biashara!
Sisi Miafrika jamani!
 

Nakubaliana na wewe. Nimeandika kwenye posti moja kuwa mabonde ya maji yasiotiririka ni sehemu kubwa ya chanzo cha magonjwa.

Ukizungumza mito unazungumza maji yanayotiririka na ukizungumza sehemu hizo na sehemu zenye maji ya kutuama ni vitu viwil tofauti. Vilevile Canada ina winter. Baridi ya winter inapunguza ongezeko la bakteria ambao ni chanzo cha magonjwa mengi.
 

Hii kali sana mzee kwikwikwi. Itabidi niikopi kwa ajiri ya future generation.

Hivi watanzania wangapi wamepanda mlima Kilimanjaro humu ndani? Yaani inabidi tuwekee thread?

Naangalia Animal planet na wanaonyesha Tanzania.
 

Hehehehehe...Companero ni Utopian huyo....
 

Mkuu unajua mimi nakerwa sana na fabrications. Soma historia ya Wapare - Professor Emeritus Isaria Kimambo kaiandika sana na Watafiti wa Kijerumani wameiandika pia mf. 'Kilimanjaro - A Regional History Volume 1: Production and Living Conditions c. 1800-1920' cha Ludger Wimmelbucker - uone kuwa ilikuwa design kukaa huko hasa enzi za vita na Wamasai!

P.S. Alafu kasome PhD ya Rogate Mshana ya 'Insisting Upon People's Knowledge to Resist Developmentalism: Peasant Communities as Producers of Knowledge for Social Transformation in Tanzania' uone jinsi Wapare/Waasu walivyokuwa wanadhibiti magonjwa kwenye mifereji yao huko Vuasu/Milimani. Ndio maana nauliza ni lini tulianza kuwa 'ndivyo tulivyo' ilhali zamani - enzi za Ujamaa wa Mwafrika - hatukuwa hivi tulivyo?
 
Nyani, Zakumi na Mkandara inabidi mumhoji Bongo Mzizi, mganga maarufu awape shule ya mantiki za utafiti wao wa asili wa dawa za mitishamba - muona jinsi wanavyotumia Fizikia, Jiografia na Biokemia kuvumbua na kutengeneza dawa! Hivi mmewahi kujiuliza kwa nini dawa zilikuwa zinachimbwa uchi au mlidhani ni uchawi? Au kwa nini watu walikuwa wanachukua magome ya upande fulani tu wakati wa kutengeneza dawa au mlidhani ni wanga? Kwa nini tunakuwa na kasumba kiasi hiki badala ya kujaribu kuelewa jinsi jamii zetu za Kijamaa zilivyo bila kutumia hizi lensi za mawazo mgando ya Kimagharibi?
 

Ana maabara huyo mganga wa kienyeji?
 

Nadhani wewe ndio unaofanya fabrication. Ukichukua kabila moja that stands out among 121 tribes, hiyo ni coincedency na sio design.

Unarudia kuhusu wapare, wakati kuna makabila 121 nchi Tanzania. Na kwa taarifa yako, kuna makabila Tanzania yana mchanganyiko watu kutoka Middle East.

Hata ule ukuta wa Zimbabwe inasemekana ni moja ya kabila la wana wa Israel waliopotea.

Na Nyerere anasemekana ni mtutsi au Mwarabu wa Sudan.
 

Companero:

Bongo Mzizi kama angekuwa anafanya analysis angeweza kujisaidia mwenyewe au taifa. We subiri tu, mzungu au mchina atakuja na kufanya chemical analysis ya mizizi na kujipatia u-star.

Je unajua alchemy ni nani? Hayo mambo ya bongo mizizi, alchemy walipitia miaka mingi sana. Lakini baadaye waliweza kufanya formalization ya shughuli zao.
 
Companero: Bongo Mzizi kama angekuwa anafanya analysis angeweza kujisaidia mwenyewe au taifa. We subiri tu, mzungu au mchina atakuja na kufanya chemical analysis ya mizizi na kujipatia u-star.

Halafu mzungu ata diagram process nzima kwa faida ya humanity. Sasa huyo mganga wa kienyeji ataficha hata huo mchakato aliotumia kupata hiyo dawa yake.
 
Companero,
Mkuu mimi niondoe katika fungu la kufikiria kwamba hatuna uwezo huo. Naamini uwezo tunao na sababu tunazo isipokuwa NIA hatuna na ndicho kinachotufanya NDIVYO TULIVYO...Nadhani umeona somo kubwa la mafanikio nchi za ulaya wakisema don't let anyone discourage U on success..U can, anyone can just believe in urself that U can..

Sasa hapa kwa MASKINI wa hali na mali (Fukara na Mjinga) fikra hizii hazipo akilini wala hawezi kuona uwezekano (tumesha kata tamaaa) ndipo tuliposimama sisi..
Mtoto wa Sultan wa Saudia alikuja ambiwa kwamba Tanzania kuna watu hufuga majini (Gene) akaja nchini na kutoa Offer ya millioni moja akipewa jini moja tu.. Mkuu wangu jamaa alipelekwa bagamoyo, Sumbawanga, Msasani, Songea U name it sehemu zote hizi alikutana na waganga wa kila aina lakini hakuna hata mmoja aliweza kumpa hilo Jini...This is a true story mkuu wangu... Jamaa akarudi kwao mikono mitupu..
My point is hata kama tuna uwezo wa kufanya Ubunifu au wowote ule kama kufuga majini au kuruka na Ungo hatuwezi kutumia Ubunifu huo kwa maendeleo yetu isipokuwa ktk Uhasidi..Kuua watu wengine, kutupa uganga bungeni, kuwaondoa kina Kolimba na kadhalika....
Hivyo, NDIVYO TULIVYO!
 

There you go again with your fabrication. What follows after 'inasemekana' is not necessarily factual. Watu ambao genes zao zimeonekana kuwa ni zi Waisrael ni Wa-Venda wa South Africa. Na hao sio waliojenga Great Zimbabwe. Hizo dhana kuwa The Great Walls of Zimbabwe zilijengwa na watu kutoka nje ya bara la Afrika kama vile yule mzungu wa kufikirika ni sehemu ya mkakati mahususi wa kujaribu kuonesha kuwa Waafrika hawajawahi kufanya mambo makubwa duniani - ndio huo mkakati unaojaribu kusema si Waafrika waliojenga mapiramidi ya Misri. Cheick Anta Diop alipofanya utafiti wa kina kuthibitisha kuwa ni Waafrika, Chuo Kikuu cha Kifaransa kilimmaindi mpaka kikataka kumnyima Degree yake. Martin Bernal akawachanganya zaidi wenzie kwa kuthibitisha kuwa ni ustaarabu wa Waafrika uliojenga Misri katika utafiti wake wa The Black Athena.

Hilo la makabila ndio eneo langu la utafiti - kuna makabila mengi tu yanakaa milimani hivyo hao Waasu sio exceptional. Na kuna makabila mengi tu hayakai milimani wala mabondeni. Talk of the so-called Highland Nilotesvis-a-vis Plane Nilotes among others. Wewe Zakumi wewe acha ku-fabricate historia na jiografia yetu kama umeshindwa kujenga hoja yako. Nasema turudi kwenye jamii zetu tuzitafiti in their own rights na sio kutegemewa mawazo mgando ya tafiti za kianthropolojia ya kikoloni!
 

Hilo neno 'formalization' ndio kiini cha mgongano wa mawazo hapa. Kwetu sisi Wajamaa ubunifu na uvumbuzi ni kwa ajili ya jamii nzima. Ndio maana mwarobaini, mwache, muodo n.k. ni mali ya umma/jamii sasa ninyi mnataka ku-formalize/patent ili iwe mali binafsi ya Big Pharma kwenye mfumo wenu hasidi wa Kibepari/Kibeberu. Mtaitaje Intellectual Property Right ya mtu private wakati ni collective property right?

Hao kina Bongo Mzizi wanafanya tafiti zao na wanajitahidi kulisaidia taifa kama jamii/jumuiya ila wasomi wetu wenye mawazo mgando ya kimagharibi kama ninyi wanawapiga vita. Haya tu-formalize kila kitu chetu tukiweke kwenye makasha ya plastiki tuone kama tutafanikiwa - hata Wachina hawafanyi hivyo aisee na hizo dawa zao za asili!

P.S. Bongo Mzizi Sio Alchemy - Naona unafanya 'History by Analogy' as if we are evolving toward the West hence where they were long time ago is where we are now ! Sio hivyo, hivi ndivyo tulivyo na tutakavyokuwa - Wajamaa katika ubunifu, uvumbuzi na ulinzi wa ufahamu wetu!
 

Mkuu Mkandara hizi lugha za watu labda ni mimi,ila tueleweshane tu na nikielewa nitaweza kushukuru. So hapo chini mkuu unaweza kuona namba kama ulitaka waseme "Wangapi" Pia angalia chati niliyioposti na links fuatilia,tofauti yetu ilipo ni kwamba nakubaliana kabisa na stori yako kuwa madakatari hao walishindwa kutambua kwamna jamaa alikuwa na malaria,ila sik kwasababu walikuwa hawana uwezo ama kwasababu labda hawana utaalam huo,no ni kwamba vyanzo vyote vyenye kuweza ku contribute ama ku facilitate mazingira ya malaria vilikuwa effectively controlled,means it has been eradicated,na kwahiyo hawana expectations zozote zile za kukutana na wagonjwa wa malaria na ndio maana huwa wanashauriwa kupata baaadhi ya chanjo pale wanaposafiri kwenda kwenye nchi zenye magonjwa ambayo hawana haja tena ya kujisumbua nayo. Na hao wanajeshi waliotoka Iraqi FYI mostly common ndo hiyo PTDS ambayo ni Post Traumatic Disorder ambayo mara nyingi inawasababisha wanajeshi hao ku commmit suided.Ndo ukweli wengine wanarudi na magonjwa mengi tu ya kisaikolojia nk.
Kama umesoma habai hiyo hapo juu pia sikatia uliyosema kwani hukusoma info nilizokuwekea hapo juu mkuu kuhusu wnanajeshi waliotoka kwene vita enzi hizo ya Korea nk na walirudi na magonjwa hata malaria?
Ukwlei ni kwamba malaria inaweza kuwa effectively controlled si kubaki kubugia miklorokwin kwasababu ru bepari anataka auze dawa na kudai pia kuwa anawapa watu ajira


 

Na wewe na wenzako kukataa kwenu ni moja ya jitihada zenu za kujikakamua ili ionekane yanayosemwa kuhusu Miafrika kutochangia chochote ktk civilisation siyo ya kweli.

Cheick Anta Diop alipofanya utafiti wa kina kuthibitisha kuwa ni Waafrika, Chuo Kikuu cha Kifaransa kilimmaindi mpaka kikataka kumnyima Degree yake.

Well, kama walimstukia anatunga ulitaka wampe tu hiyo shahada? Halafu yeye alithibitisha vipi? Kwani alikuwepo kubeba zege? Hivi mtu unathibishaje mambo ambayo hata hujui kwa uhakika yalitokea lini? Au alitumia carbon-14 dating?

Martin Bernal akawachanganya zaidi wenzie kwa kuthibitisha kuwa ni ustaarabu wa Waafrika uliojenga Misri katika utafiti wake wa The Black Athena.

Alithibitishaje? alikuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…