Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Zakumi,
Mkuu sio kweli, miji mingi Ulkaya ipo kando ya mito au bahari tena basi ukitaka kupata uhakika zaidi tazama old city zote za miji yao utaona ipo karibu zaidi na bahari kwa sababu wao wanatazama urahisi wa kusafirisha mali zao.. sasa ukienda mashambani ndiko unakuta miji ipo juu ma mashamba yako chini kwa sababu ya upatikanaji wa maji vile vile.. Hii yote inatuonyesha kwamba biashara na uzalishaji unatangulia sehemu za makazi yao..
Sisi tunajenga miji yetu bila malengo, Dodoma ile pale hadi leo tumeshindwa kuhamia.. Hatuna sababu ya kuhamia wala sababu ya kutohamia..

Nakubaliana na wewe lakini nilikuwa nanukuu ujenzi wa karne ya 13 na kurudi nyuma.

Walivyoweza kushinda mazingira waliendelea sehemu nyingine. Na vilevile nilikuwa nasisitizia kuhusu ugonjwa wa Malaria.

Kushindwa kupambana na magonjwa mengi kwa Tanzania kuna sababishwa na watu kutochagua maeneo mazuri ya kujenga makazi yao.

Malaria na kipindupindu ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa good planning kwa upande wa Goverment na individuals. Watu wanaoishi kwenye maeneo mazuri kiafya wataamka asubuhi na kufikiri wabuni nini kuhusu maisha yao. Na wale wanaoishi kwenye maisha duni, wataamka kufikiri ni jinsi gani wa-survive kabla jua kuzama.

Hivyo kwa kulinganisha, katika karne ya 13 wazungu walikuwa wanafanya juhudi za kuchagua sehemu gani wajenge. Wakati huku kwetu watu wanajenga hili wapate sehemu za kuishi tu na baadaye watafute tiba.
 
Zakumi,
Duh basi nchi kama Canada kila sehemu ni maji mkuu wangu miji yote iko kando ya ziwa, mito au bahari na huko kusikokuwa na maji ni mbuga tupu kuliko ile ya Dodoma Singida..Pamoja na yote haya malaria inaweza kabisa kuzuiwa hata Kipindupindu yote haya ni maradhi yanayotokana na uchafu.. ndio yale alosema Nyani Ngabu na uchafu unaolundikwa kila kona ya mji tukauza vyakula vyetu sehemu karibu na dampo hizo..
Kisha tunadai kuwa chakula cha pale kitamu kuliko mahotel makubwa mjini..
 
Naam ndivyo tulivyo - Wajamaa hata katika uvumbuzi. Jamii zetu zinavumbua na kutumia uvumbuzi wao kwa Mjamaa. Ndio maana mwarobaini, dawa ya malaria, haukuwa unahodhiwa. Hebu cheki nukuu hii:

"Throughout Africa, people have also developed knowledge around ... bio-resources. The knowledge has been widely shared within communities and freely transferred from one generation to the other. In this way innovation and what was produced was never meant to benefit individuals and were not claimed to be individual properties of the innovators. For example, communities of hunters and gatherers used and continue to use, in some ways, thousands of plants and animals for food, medicine, and shelter...These resources and knowledge have remained, over the years, community property. They were and are produced, owned and controlled by communities themselves. These resources and the knowledge that people have been able to develop and accumulate over time, and passed through one generation to the other, are at the verge of being dispossed of the rightful owners...mainly through commoditization and privatization...through patenting (the modern form of enclosure) ...this takes the form of intellectual property rights..." - The Mute Plunder: Bio-resources and Dispossession in Tanzania, pp. 1-4

Ndio maana Ngabu anashinda kwenye mjadala huu bila kuponyeza keyboard yake.

Uvumbuzi wa Mwarobaini ulikuwa hauna reasoning yoyote. Inawezekana watu walitafuna majani ya miti mbalimbali kabla ya kupata nafuu kwa kutumia mwarobani. Hii ni trial and error method na haionyeshi ubunifu wowote hule.

Ubunifu unakuja pale mtu anapofanya kazi zake methodically na sio kucheza bahati nasibu.
 
Usinichekeshe miye weee!..
Unajua kahawa ilivumbuliwa vipi..
based on True story - Mtu mmoja (Ethiopia) alikuwa akichunga mbuzi wake wamechokaaa......sasa ikatokea wakala mbegu za mibuni muda mfupi wakaanza kuchangamka.. basi ikiwa kila siku lazima kuwalisha hizo mbegu hadi siku mzungu alipokuja na kuambiwa habari ile... mzungu katika kutafiti akaona kweli akaifanyia kazi..
Hivyo mbunifu hapa ni mbuzi, mwafrika alitazama na kufurahia kuwa mbuzi wake wanachangamka.. mzungu akaona biashara!
Sisi Miafrika jamani!
 
Zakumi,
Duh basi nchi kama Canada kila sehemu ni maji mkuu wangu miji yote iko kando ya ziwa, mito au bahari na huko kusikokuwa na maji ni mbuga tupu kuliko ile ya Dodoma Singida..Pamoja na yote haya malaria inaweza kabisa kuzuiwa hata Kipindupindu yote haya ni maradhi yanayotokana na uchafu.. ndio yale alosema Nyani Ngabu na uchafu unaolundikwa kila kona ya mji tukauza vyakula vyetu sehemu karibu na dampo hizo..
Kisha tunadai kuwa chakula cha pale kitamu kuliko mahotel makubwa mjini..

Nakubaliana na wewe. Nimeandika kwenye posti moja kuwa mabonde ya maji yasiotiririka ni sehemu kubwa ya chanzo cha magonjwa.

Ukizungumza mito unazungumza maji yanayotiririka na ukizungumza sehemu hizo na sehemu zenye maji ya kutuama ni vitu viwil tofauti. Vilevile Canada ina winter. Baridi ya winter inapunguza ongezeko la bakteria ambao ni chanzo cha magonjwa mengi.
 
Usinichekeshe miye weee!..
Unajua kahawa ilivumbuliwa vipi..
based on True story - Mtu mmoja (Ethiopia) alikuwa akichunga mbuzi wake wamechokaaa......sasa ikatokea wakala mbegu za mibuni muda mfupi wakaanza kuchangamka.. basi ikiwa kila siku lazima kuwalisha hizo mbegu hadi siku mzungu alipokuja na kuambiwa habari ile... mzungu katika kutafiti akaona kweli akaifanyia kazi..
Hivyo mbunifu hapa ni mbuzi, mwafrika alitazama na kufurahia kuwa mbuzi wake wanachangamka.. mzungu akaona biashara!
Sisi Miafrika jamani!

Hii kali sana mzee kwikwikwi. Itabidi niikopi kwa ajiri ya future generation.

Hivi watanzania wangapi wamepanda mlima Kilimanjaro humu ndani? Yaani inabidi tuwekee thread?

Naangalia Animal planet na wanaonyesha Tanzania.
 
Ndio maana Ngabu anashinda kwenye mjadala huu bila kuponyeza keyboard yake.

Uvumbuzi wa Mwarobaini ulikuwa hauna reasoning yoyote. Inawezekana watu walitafuna majani ya miti mbalimbali kabla ya kupata nafuu kwa kutumia mwarobani. Hii ni trial and error method na haionyeshi ubunifu wowote hule.

Ubunifu unakuja pale mtu anapofanya kazi zake methodically na sio kucheza bahati nasibu.

Hehehehehe...Companero ni Utopian huyo....
 
Unasema ukitaka kuwaficha waAfrika andika maarifa vitabu. Nimetumia vitabu kuonyesha unasema nafunga kamba.

Ulinzi ulikuwa ni sababu moja na sababu nyingine ni magonjwa. Sehemu yoyote yenye maji yasiotiririka na yanayotoa harufu ni hatari kwa magonjwa.

Wapare ni kabila moja kati makabila 121 ya Tanzania. Hivyo wao kuishi milimani ni coincident na sio design. Na ndio maana wanyakyusa kwao Mbeya wanaishi kwenye mazingira mazuri ya milimani yasio na magonjwa, lakini wakifika DSM wanasahau na kujazana Keko Mwanga.

Mkuu unajua mimi nakerwa sana na fabrications. Soma historia ya Wapare - Professor Emeritus Isaria Kimambo kaiandika sana na Watafiti wa Kijerumani wameiandika pia mf. 'Kilimanjaro - A Regional History Volume 1: Production and Living Conditions c. 1800-1920' cha Ludger Wimmelbucker - uone kuwa ilikuwa design kukaa huko hasa enzi za vita na Wamasai!

P.S. Alafu kasome PhD ya Rogate Mshana ya 'Insisting Upon People's Knowledge to Resist Developmentalism: Peasant Communities as Producers of Knowledge for Social Transformation in Tanzania' uone jinsi Wapare/Waasu walivyokuwa wanadhibiti magonjwa kwenye mifereji yao huko Vuasu/Milimani. Ndio maana nauliza ni lini tulianza kuwa 'ndivyo tulivyo' ilhali zamani - enzi za Ujamaa wa Mwafrika - hatukuwa hivi tulivyo?
 
Nyani, Zakumi na Mkandara inabidi mumhoji Bongo Mzizi, mganga maarufu awape shule ya mantiki za utafiti wao wa asili wa dawa za mitishamba - muona jinsi wanavyotumia Fizikia, Jiografia na Biokemia kuvumbua na kutengeneza dawa! Hivi mmewahi kujiuliza kwa nini dawa zilikuwa zinachimbwa uchi au mlidhani ni uchawi? Au kwa nini watu walikuwa wanachukua magome ya upande fulani tu wakati wa kutengeneza dawa au mlidhani ni wanga? Kwa nini tunakuwa na kasumba kiasi hiki badala ya kujaribu kuelewa jinsi jamii zetu za Kijamaa zilivyo bila kutumia hizi lensi za mawazo mgando ya Kimagharibi?
 
Ana maabara huyo mganga wa kienyeji?
 
Nadhani wewe ndio unaofanya fabrication. Ukichukua kabila moja that stands out among 121 tribes, hiyo ni coincedency na sio design.

Unarudia kuhusu wapare, wakati kuna makabila 121 nchi Tanzania. Na kwa taarifa yako, kuna makabila Tanzania yana mchanganyiko watu kutoka Middle East.

Hata ule ukuta wa Zimbabwe inasemekana ni moja ya kabila la wana wa Israel waliopotea.

Na Nyerere anasemekana ni mtutsi au Mwarabu wa Sudan.
 
Companero:

Bongo Mzizi kama angekuwa anafanya analysis angeweza kujisaidia mwenyewe au taifa. We subiri tu, mzungu au mchina atakuja na kufanya chemical analysis ya mizizi na kujipatia u-star.

Je unajua alchemy ni nani? Hayo mambo ya bongo mizizi, alchemy walipitia miaka mingi sana. Lakini baadaye waliweza kufanya formalization ya shughuli zao.
 
Companero: Bongo Mzizi kama angekuwa anafanya analysis angeweza kujisaidia mwenyewe au taifa. We subiri tu, mzungu au mchina atakuja na kufanya chemical analysis ya mizizi na kujipatia u-star.

Halafu mzungu ata diagram process nzima kwa faida ya humanity. Sasa huyo mganga wa kienyeji ataficha hata huo mchakato aliotumia kupata hiyo dawa yake.
 
Companero,
Mkuu mimi niondoe katika fungu la kufikiria kwamba hatuna uwezo huo. Naamini uwezo tunao na sababu tunazo isipokuwa NIA hatuna na ndicho kinachotufanya NDIVYO TULIVYO...Nadhani umeona somo kubwa la mafanikio nchi za ulaya wakisema don't let anyone discourage U on success..U can, anyone can just believe in urself that U can..

Sasa hapa kwa MASKINI wa hali na mali (Fukara na Mjinga) fikra hizii hazipo akilini wala hawezi kuona uwezekano (tumesha kata tamaaa) ndipo tuliposimama sisi..
Mtoto wa Sultan wa Saudia alikuja ambiwa kwamba Tanzania kuna watu hufuga majini (Gene) akaja nchini na kutoa Offer ya millioni moja akipewa jini moja tu.. Mkuu wangu jamaa alipelekwa bagamoyo, Sumbawanga, Msasani, Songea U name it sehemu zote hizi alikutana na waganga wa kila aina lakini hakuna hata mmoja aliweza kumpa hilo Jini...This is a true story mkuu wangu... Jamaa akarudi kwao mikono mitupu..
My point is hata kama tuna uwezo wa kufanya Ubunifu au wowote ule kama kufuga majini au kuruka na Ungo hatuwezi kutumia Ubunifu huo kwa maendeleo yetu isipokuwa ktk Uhasidi..Kuua watu wengine, kutupa uganga bungeni, kuwaondoa kina Kolimba na kadhalika....
Hivyo, NDIVYO TULIVYO!
 
Nadhani wewe ndio unaofanya fabrication. Ukichukua kabila moja that stands out among 121 tribes, hiyo ni coincedency na sio design.

Unarudia kuhusu wapare, wakati kuna makabila 121 nchi Tanzania. Na kwa taarifa yako, kuna makabila Tanzania yana mchanganyiko watu kutoka Middle East.

Hata ule ukuta wa Zimbabwe inasemekana ni moja ya kabila la wana wa Israel waliopotea.

Na Nyerere anasemekana ni mtutsi au Mwarabu wa Sudan.

There you go again with your fabrication. What follows after 'inasemekana' is not necessarily factual. Watu ambao genes zao zimeonekana kuwa ni zi Waisrael ni Wa-Venda wa South Africa. Na hao sio waliojenga Great Zimbabwe. Hizo dhana kuwa The Great Walls of Zimbabwe zilijengwa na watu kutoka nje ya bara la Afrika kama vile yule mzungu wa kufikirika ni sehemu ya mkakati mahususi wa kujaribu kuonesha kuwa Waafrika hawajawahi kufanya mambo makubwa duniani - ndio huo mkakati unaojaribu kusema si Waafrika waliojenga mapiramidi ya Misri. Cheick Anta Diop alipofanya utafiti wa kina kuthibitisha kuwa ni Waafrika, Chuo Kikuu cha Kifaransa kilimmaindi mpaka kikataka kumnyima Degree yake. Martin Bernal akawachanganya zaidi wenzie kwa kuthibitisha kuwa ni ustaarabu wa Waafrika uliojenga Misri katika utafiti wake wa The Black Athena.

Hilo la makabila ndio eneo langu la utafiti - kuna makabila mengi tu yanakaa milimani hivyo hao Waasu sio exceptional. Na kuna makabila mengi tu hayakai milimani wala mabondeni. Talk of the so-called Highland Nilotesvis-a-vis Plane Nilotes among others. Wewe Zakumi wewe acha ku-fabricate historia na jiografia yetu kama umeshindwa kujenga hoja yako. Nasema turudi kwenye jamii zetu tuzitafiti in their own rights na sio kutegemewa mawazo mgando ya tafiti za kianthropolojia ya kikoloni!
 
Companero:

Bongo Mzizi kama angekuwa anafanya analysis angeweza kujisaidia mwenyewe au taifa. We subiri tu, mzungu au mchina atakuja na kufanya chemical analysis ya mizizi na kujipatia u-star.

Je unajua alchemy ni nani? Hayo mambo ya bongo mizizi, alchemy walipitia miaka mingi sana. Lakini baadaye waliweza kufanya formalization ya shughuli zao.

Hilo neno 'formalization' ndio kiini cha mgongano wa mawazo hapa. Kwetu sisi Wajamaa ubunifu na uvumbuzi ni kwa ajili ya jamii nzima. Ndio maana mwarobaini, mwache, muodo n.k. ni mali ya umma/jamii sasa ninyi mnataka ku-formalize/patent ili iwe mali binafsi ya Big Pharma kwenye mfumo wenu hasidi wa Kibepari/Kibeberu. Mtaitaje Intellectual Property Right ya mtu private wakati ni collective property right?

Hao kina Bongo Mzizi wanafanya tafiti zao na wanajitahidi kulisaidia taifa kama jamii/jumuiya ila wasomi wetu wenye mawazo mgando ya kimagharibi kama ninyi wanawapiga vita. Haya tu-formalize kila kitu chetu tukiweke kwenye makasha ya plastiki tuone kama tutafanikiwa - hata Wachina hawafanyi hivyo aisee na hizo dawa zao za asili!

P.S. Bongo Mzizi Sio Alchemy - Naona unafanya 'History by Analogy' as if we are evolving toward the West hence where they were long time ago is where we are now ! Sio hivyo, hivi ndivyo tulivyo na tutakavyokuwa - Wajamaa katika ubunifu, uvumbuzi na ulinzi wa ufahamu wetu!
 
JmUshi!,
Mkuu hiyo graph inaonyesha wagonjwa wa maradhi hayo kati ya miaka hiyo na sii tiba zilizokuwepo ktk hospital zao. Hawakusema ni watu wangapi walikufa na maradhi hayo au ni wakati gani waliweza ku control kabisa....
Nimesema hapo juu kwamba mshikaji wangu hakupewa dawa hadi mtaalam wa magonjwa ya tropic lakini madaktari wengine walishindwa kuelewa anaumwa maradhi gani.. hiyo Marekani unayozungumza na wala sii case moja tu nazifahamu nyingine ambazo zilitokea pia...kwa hiyo unaposoma maandishi kisha unataka tubishane wakati mimi nimeona hali halisi tutakesha!.

Mkuu kuna vitengo kibao vya maradhi ya tropical lakini hadi leo hii tunavyozungumza kuna maradhi wanajeshi waliokwenda Iraq bado hayajapatiwa tiba kwa sababu ni mageni kwao, Vitengo vipo na wanajaribu kwa kila hali kuponya wagonjwa hao lakini huwezi ku walk in ktk hospital yoyote ukatibiwa wapo specialist wa maradhi hayo..Swine Flue pekee imeshaua watu kibao na haikuwa kila hospital au daktari anajua tiba yake...

Zakumi,
Mkuu nimekuelewa unaposema wazungu walijenga nyumba zao milimani hapa Afrika na kusema kweli sababu yako inaleta maana kwani ndicho nilichokuwa nazungumzia tofauti baina yetu na mazungu..
wao ktk mazingira yetu walifanya kile kinachotakiwa pamoja na kwamba kwao wanaweza kujenga karibu na maziwa, mito au bahari kutokana na infrastucture iliyokwisha jengwa kulingana na mazingira yao. Kama alivyosema Companero ujenzi kwao huko milimani ulihusiana zaidi na ulinzi, uwezo wa kumwona adui toka mbali kabla hajakaribia mji hivyo wawe wepesi kutuma majeshi yao chini ambako wananchi wanaishi..lakini huko chini infrastructure ilikuwawepo kuweza ku deal na magonjwa yao labda itokee maradhi ya kigeni kama ilivyoingia ugonjwa wa Panya (rabies)..

Hapa Afrika walijua sii kwao hawawezi kujenga infrastructure ya kudumu isipokuwa ile yenye manufaa kwao kibiashara... lakini sisi wenyeji kujenga mlimani ni adha kubwa kwaza tunafikiria ule mwendo wa kupanda mlima... Kisha basi hata kama tunajenga karibu na mito, maziwa na bahari tunashindwa kutanguliza kujenga infrastructure inayokabiliana na matatizo yatokanayo..

Companero,

Mkuu maneno yako hapo juu ni tafsiri safi ya NDIVYO TULIVYO pamoja na kwamba unajaribu kuibadilisha.. kwani ni kina nani waliokubali Lake Nyaza iitwe Victoria!..na kama hatukubali tunashindwa kipi kubadilisha jina leo hii miaka 48 ndani ya Uhuru..
Tukubali tusikubali sisi tuna matatizo, ikiwa kweli mwarabu mmoja na gobole la kushindilia risasi mbili anaweza kukusanya watumwa elfu akawatembeza kwa miguu toka Kongo hadi Bagamoyo
na kuwaingiza utumwani akiwatumia house nigger kina Tippu Tippu (wanyapala) kuna tofauti gani na mfumo huu wa leo..Tumebadilika kitu gani zaidi ya rangi ya watawala!
Tena bila aibu hao walikwenda Utumwani huko Marekani na visiwa vya carribean wanakataa kabisa asili yao, hakuna mzungu wala mtu yeyote anayefumba midomo yao kui recognise Afrika, kisha basi hata sisi Waafrika hatuwataki warudi hata kwa mbinde watakuja chukua ardhi zetu!..Israel na udogo wake kila siku wanalilia watu wake warudi..Kongo, Rwanda, Burundi na nchi kibao kila siku vita ya makabila kugombania ardhi ambayo urithi wake ni wazi kabisa...

Mkuu Mkandara hizi lugha za watu labda ni mimi,ila tueleweshane tu na nikielewa nitaweza kushukuru. So hapo chini mkuu unaweza kuona namba kama ulitaka waseme "Wangapi" Pia angalia chati niliyioposti na links fuatilia,tofauti yetu ilipo ni kwamba nakubaliana kabisa na stori yako kuwa madakatari hao walishindwa kutambua kwamna jamaa alikuwa na malaria,ila sik kwasababu walikuwa hawana uwezo ama kwasababu labda hawana utaalam huo,no ni kwamba vyanzo vyote vyenye kuweza ku contribute ama ku facilitate mazingira ya malaria vilikuwa effectively controlled,means it has been eradicated,na kwahiyo hawana expectations zozote zile za kukutana na wagonjwa wa malaria na ndio maana huwa wanashauriwa kupata baaadhi ya chanjo pale wanaposafiri kwenda kwenye nchi zenye magonjwa ambayo hawana haja tena ya kujisumbua nayo. Na hao wanajeshi waliotoka Iraqi FYI mostly common ndo hiyo PTDS ambayo ni Post Traumatic Disorder ambayo mara nyingi inawasababisha wanajeshi hao ku commmit suided.Ndo ukweli wengine wanarudi na magonjwa mengi tu ya kisaikolojia nk.
Kama umesoma habai hiyo hapo juu pia sikatia uliyosema kwani hukusoma info nilizokuwekea hapo juu mkuu kuhusu wnanajeshi waliotoka kwene vita enzi hizo ya Korea nk na walirudi na magonjwa hata malaria?
Ukwlei ni kwamba malaria inaweza kuwa effectively controlled si kubaki kubugia miklorokwin kwasababu ru bepari anataka auze dawa na kudai pia kuwa anawapa watu ajira

Malaria in the USA:
In the first quarter of this century, malaria was rampant in U.S.A. with nearly 6 million cases annually. Due to determined antimalaria measures and permanent vector control measures like screening of all constructions, malaria has been controlled effectively.
 
Hizo dhana kuwa The Great Walls of Zimbabwe zilijengwa na watu kutoka nje ya bara la Afrika kama vile yule mzungu wa kufikirika ni sehemu ya mkakati mahususi wa kujaribu kuonesha kuwa Waafrika hawajawahi kufanya mambo makubwa duniani - ndio huo mkakati unaojaribu kusema si Waafrika waliojenga mapiramidi ya Misri.

Na wewe na wenzako kukataa kwenu ni moja ya jitihada zenu za kujikakamua ili ionekane yanayosemwa kuhusu Miafrika kutochangia chochote ktk civilisation siyo ya kweli.

Cheick Anta Diop alipofanya utafiti wa kina kuthibitisha kuwa ni Waafrika, Chuo Kikuu cha Kifaransa kilimmaindi mpaka kikataka kumnyima Degree yake.

Well, kama walimstukia anatunga ulitaka wampe tu hiyo shahada? Halafu yeye alithibitisha vipi? Kwani alikuwepo kubeba zege? Hivi mtu unathibishaje mambo ambayo hata hujui kwa uhakika yalitokea lini? Au alitumia carbon-14 dating?

Martin Bernal akawachanganya zaidi wenzie kwa kuthibitisha kuwa ni ustaarabu wa Waafrika uliojenga Misri katika utafiti wake wa The Black Athena.

Alithibitishaje? alikuwepo?
 
Back
Top Bottom