Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Zakumi,
Mkuu sio kweli, miji mingi Ulkaya ipo kando ya mito au bahari tena basi ukitaka kupata uhakika zaidi tazama old city zote za miji yao utaona ipo karibu zaidi na bahari kwa sababu wao wanatazama urahisi wa kusafirisha mali zao.. sasa ukienda mashambani ndiko unakuta miji ipo juu ma mashamba yako chini kwa sababu ya upatikanaji wa maji vile vile.. Hii yote inatuonyesha kwamba biashara na uzalishaji unatangulia sehemu za makazi yao..
Sisi tunajenga miji yetu bila malengo, Dodoma ile pale hadi leo tumeshindwa kuhamia.. Hatuna sababu ya kuhamia wala sababu ya kutohamia..
Nakubaliana na wewe lakini nilikuwa nanukuu ujenzi wa karne ya 13 na kurudi nyuma.
Walivyoweza kushinda mazingira waliendelea sehemu nyingine. Na vilevile nilikuwa nasisitizia kuhusu ugonjwa wa Malaria.
Kushindwa kupambana na magonjwa mengi kwa Tanzania kuna sababishwa na watu kutochagua maeneo mazuri ya kujenga makazi yao.
Malaria na kipindupindu ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa good planning kwa upande wa Goverment na individuals. Watu wanaoishi kwenye maeneo mazuri kiafya wataamka asubuhi na kufikiri wabuni nini kuhusu maisha yao. Na wale wanaoishi kwenye maisha duni, wataamka kufikiri ni jinsi gani wa-survive kabla jua kuzama.
Hivyo kwa kulinganisha, katika karne ya 13 wazungu walikuwa wanafanya juhudi za kuchagua sehemu gani wajenge. Wakati huku kwetu watu wanajenga hili wapate sehemu za kuishi tu na baadaye watafute tiba.