Uchaguzi 2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

Uchaguzi 2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

Rafiki yangu Ally Maswanya alipo gomea uteuzi wa Rais Magufuli kuwa DC Mbozi kulifanya mheshimiwa achukie sana.
Hata akishinda kura za maoni Urambo hawezi pitishwa na Magufuli kwa kisingizo cha kakosa maadili
 
Mbona mnataka kuwaharibia watu mapema hivi? Hizi tetesi zinaweza kufanyiwa kazi na watu wakaanza kupigana vikumbo kwa nia ovu. MSIWATIE WATU GUNDU
 
Amani iwe kwenu!!

Huyu dada mhe! Amekuwa msaada kwetu na jamii ya Wana Mbeya kwa ujumla kwani kawasaidia wakina Mama wengi kupata mikopo yenye riba nafuu na vijana wengi kwenda Shule Mimi na awa wenzangu tumeapa kumpigia kampeni bure kabisa Dr Tulia Ackson Mwansansu kuwa Mbunge wa Mbeya 2020.
tafuta kazi ya kufanya mkuu. huu ukibaraka siyo mzuri
 
Moshi mjini na vijijini naona wote chadema na ccm hawana watu wa maana kwani wanaotaka hawafai na wanaofaa hawataki.
Vyama visisubiri watu waje, watafute watu wanaokubalika wawashawishi wagombee.
Hawa waroho wanaojikomba na hawa waluoshindwa kutekeleza majukumu kwa miaka 5 sasa tupa kule?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki yangu Ally Maswanya alipo gomea uteuzi wa Rais Magufuli kuwa DC Mbozi kulifanya mheshimiwa achukie sana.
Hata akishinda kura za maoni Urambo hawezi pitishwa na Magufuli kwa kisingizo cha kakosa maadili
hivi kwani bado anania hiyo..? si bora abaki kwenye Ajira yake huko huko au akapige magoti kwa Mzee
 
Ameanza kampeni mapema mpeni kura muone km mtamuona, ila watu wa Mbeya jinsi walivyo na msimamo sidhani km atachukua Ubunge.
Namshauri Magufuli afute uchaguzi pesa za uchaguzi zikawajengee barabara nchi jirani ya Kigoma angalau nao waunganishwe na Tanzania
 
hivi kwani bado anania hiyo..? si bora abaki kwenye Ajira yake huko huko au akapige magoti kwa Mzee
Ally kazi yake kwa sasa ni NONO sana hawezi wania Ubunge ambao sasa hauna deal kwa sababu Rais wa TZ ndiye pia muamuzi wa mwisho kuhusu posho za wabunge na akaamua kakata posho kibao za kusafiri.za wabunge.
Wabunge wana tengeneza pesa kwa safari lkn sasa hazipo!!
 
Bila shaka tunamkumbuka Mh. Lowasa wakati akiwa Waziri Mkuu kazi alizofanya.

Ndani ya mwaka mmoja tuu, 2006-2007 alijenga vyumba vya kutosha vya madarasa shule zote za kata nchi nzima. Ikumbukwe ndiye aliyeasisi wazo la kila kata nchini iwe na Sekondari.

Utafiti mdogo nilioufanya,umeonyesha baadhi ya hizi shule hazijaongeza hata jengo moja la darasa. Yapo yaleyale yaliyojengwa ns Mh. Lowasa.

Nimejaribu kufuatilia taarifa za vyombo vingi vya habari. Mwaka huu 2020, baadho ya wanafunzi hawatapata nafasi za shule ( form one) kwa vile hakuna vyumba. Maeneo mengi ya nchi yana tatizo hilo.
Baadhi ya viongozi wanatoa kauli kinzani kuhusu nini kifanyike,madarasa yajengwe,watoto wapate nafasi wasome. Ikumbukwe:

1. Ilishatolewa kauli kuwa Elimu ni bure,Serikali itagharamia.
2. Mwananchi asisumbuliwe kutoa michango ya shule, Mwl Mkuu au kiongozi atakayechangisha atachukuliwa hatua.
3. Wananchi wapo katika mtanziko kuwa kama kauli za awali za Serikali zimebadilika kuhusu elimu bure kwa vile hakuna tamko rasmi kuwa " ni kuchangia elimu"

Niombe rai kwa viongozi waliopo watumie hazina za viongozi wastaafu kupata ushauri. Mh, Lowasa ni moja ya viongozi waliofanikisha mambo haya kwa muda mfupi na yupo.

Serikali ina nia njema japo changamoto kama hizi zinaweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa viongozi wao.
 
Usichokumbuka ni kuwa katika ule ujenzi kulikuwepo NGUVU ZA WANANCHI KWANZA halafu SERIKALI inaweka mchango wake. Wewe hukuchangia? Sehemu nyingine nguvu kazi ilitumika kujenga wakati serikali ikitowa vifaa
 
We ulishaenda jimbon kwake Monduli ukaona hali ya maendeleo ya jimbo lake? Nenda kaone ili uweze kujua kuwa yule jamaa hovyo kabisa yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Kiongozi wa Kitaifa hapimwi kwa maendeleo ya jimboni kwake tuu bali ni ya Kitaifa kwa Ujumla wake!!!! Hii dhana unayoongea labda iwe imejitokeza zaidi awamu hii, enzi za Mwl, Nyerere, Mwinyi Mkapa na Kikwete halikuwepo. Fanya utafiti,nenda majimboni mwao!
 
Back
Top Bottom