Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Angetajwa kwa mema usingesema kuwa acheni kumtaja mfu ila kwa kuwa anatajwa kwa maouvu yake ndio unakereka kwa sababu hatujui huenda ulikuwa mnufaika wa hayo.
Biblia inasema usimwache mwovu ashuke kaburini kwa amani.
Nahisi ndicho kinachowndelea kwa yule mtu kwa sasa kama ilivyo kwaFarao, Hitler, Musolin, Beneto, Bokasa nk.
 
Kama hujui unakotoka hutaweza kujua unakokwenda. Adolf Hitler anatajwa na ataendelea kutajwa kila siku. Wanaomtaja ni wapuuzi? Hakika wewe ni mpuuzi wa kiwango cha juu.
 
Hakuan kupanic mtu hapa. Muuaji atabaki kuwa muuaji na ni lazima akumbukwe kwa mauaji aliyofanya pamoja na ujinga mwingine mwingi, mpaka wa kukataa uwepo wa korona na hiyo hiyo korona ikaja kumuondoa.
 
Well, huwezi kumpangia mwenye maumivu namna ya kulalamika. Kama inakukera, then fuatilia yanayokuhusu.
Hata haya yananihusu pia kama yasingenihusu basi hayo malalamiko wangekuwa wanalalamika majumbani kwao kwa wake na waume zao na mue nisingeyasikia. Lakini anayezungumziwa hapa alikuwa kiongozi wa nchi ya Tanzania na mie ni mtanzania.

Mie nina rafiki yangu nae anakiri kuguswa na uongozi wa Magufuli ila hakutaka kuniambia aliguswa vp ila watu kama hawa ndio kutwa kumnanga Magufuli kumbe ni hasira zake binafsi na si kwamba anachukia maovu.
 
Kama hujui unakotoka hutaweza kujua unakokwenda. Adolf Hitler anatajwa na ataendelea kutajwa kila siku. Wanaomtaja ni wapuuzi? Hakika wewe ni mpuuzi wa kiwango cha juu.
Hata Nyerere anatajwa ila mbona hatajwi kwa mabaya kama alivyomchambua Lissu bungeni? Mwisho wa siku Lissu akaonekana anamkosea heshima baba wa taifa.
 
Kikubwa mwanadamu yoyote hupaswi kuwa mwovu na usijiinue sana hadi kujifananisha na malaika na kujiuona hukosei, Magufuli alipitiliza kujiona yeye ni yeye na hakuna kama yeye.
Kipi hicho cha ajabu sana alichofanya hadi useme alijiona yeye ndio yeye na hakosei? Kwamba alipitiliza.
 
Hakuan kupanic mtu hapa. Muuaji atabaki kuwa muuaji na ni lazima akumbukwe kwa mauaji aliyofanya pamoja na ujinga mwingine mwingi, mpaka wa kukataa uwepo wa korona na hiyo hiyo korona ikaja kumuondoa.
Ndio msipanic hapa ni hoja tu, kuendelea kutumia muda mwingi kujadili maovu ya Magufuli kuliko kujadili maovu yanayoendelea kutendwa na waliyo hai hilo ndio jambo ambalo mleta mada anaona halina faida kwa taifa ni suala la kihisia watu kupunguza tu hasira zao. Tungekuwa tunajadili makosa na maovu ya Nyerere hadi sasa sidhani kama tungesonga mbele.
 
Wanaomsema magufuli, na Kwa usahihi zaidi sio kumsema bali kuonyesha 'sura' yake halisi, sio upinzani. Ni watu wote ambao sio wanafiki, wanaopenda ukweli.

Sura yake halisi Watu wengi wanajua,
Nafikiri tungejikita kwenye ishu za msingi kama Katiba Mpya,
 
Kwa Nyerere, mazuri yake ni mengi kuliko mabaya..
Kwa jiwe ni kinyume chake!
Kwahiyo hapa mnaangalia idadi ya maovu au athari zake hata kama hayo maovu yalikuwa machache? Na kama wewe ndio una mtazamo huo kwa Nyerere basi pia wengine wana mtazamo tofauti na wewe kwa Magufuli na hata Nyerere.
 

Na hili ndio tatizo la wengi wetu.
Kulaumu mambo yaliyopita ilhali yaliyopo tukiyafumbia macho
 
Kama hatakuelewa basi
 
Mwalimu Nyerere alisema TUJISAHIHISHE yamkini hayo mabaya ya sasa Yana msinginwake kwa yaliyopita sio we have to identify the mistakes before we correct them.
 
Mungu ndiye anayejua Zaidi.
Kila Jambo limekadiriwa,
Samehe nawe usamehewe.
Kama unataka kuwa bingwa wa kusamehe, msamehe na Shetani! Matendo ya Jiwe yalikuwa ya Kishetani kwa Watanzania, tutaendelea kumkemea kama tunavyomkemea Shetani kila siku.
 
Kama unataka kuwa bingwa wa kusamehe, msamehe na Shetani! Matendo ya Jiwe yalikuwa ya Kishetani kwa Watanzania, tutaendelea kumkemea kama tunavyomkemea Shetani kila siku.
Duhh, lakini tuliopo ndio turekeshe tunavyoishi na tuangalie matendo yetu pia badala ya kuishia kulalamikia matendo ya Mtu mwingine huku bila ya kujifunza kupitia yeye na kuishi na kutenda vyema vile tupasavy
 
Sisi Tunachojua, kuna siku Magufulification itaingizwa kwenye Mtaala wa Elimu yetu, na hayo ndio Mafanikio na mwanzo wa Utambuzi wa Kweli kwa vitukuu vyetu kesho.
True Legend.
 
Reactions: nao
Hujazuiawa kuyataja mabaya yake kama unaona yaliwaumiza watanzania au wewe binafsi
 
Mwenye kuelewa na aelewe ufafanuzi huu mujarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…