Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Sijui hata nani kawaloga. Unaweka maelezo yote kamili bei na njia ya mawasiliano etc.

Anakuja mtu anakuuliza maswali ambayo majibu yake kwenye maelezo ulishaweka. Yaani mwisho wa siku ni usumbufu tu. Anakwambia naomba picha zaidi wakati picha za kutosha umeshaweka kwenye tangazo. Mwingine anauliza bei tena wakati bei umeshaweka.

Anakuja anakusumbua maswali kibao mwisho wa siku anakwambia eti niidhani hivi na vile. Una muuliza ina maana maelezo ya bidhaa hukusoma kwenye Tangazo?

Ingawa wateja serious wachache sana pia huwa wapo tena hawanaga mambo mengi ni anakuja tu moja kwa moja anauliza discount na njia ya kuipata.

KUTOKA KWA WADAU;

Kwa uzoefu wao pia mara nyingi wateja serious husoma maelezo ya bidhaa husika na mara nyingi hupiga simu moja kwa moja. Ila wale wateja wasio serious me nawaita wazururaji wa mitandaoni. wao kila sehemu wanataka kufanya kijiwe muanze kupiga story ndio huja na maswali ambayo majibu tayari yapo kwenye maelezo ya bidhaa husika.

KUHUSU UTAPELI;

Ni kweli kuwa upo kwa baadhi ya wauzaji. Jambo la msingi mara nyingi matapeli upendelea kuweka location kuwa wanapatikana Zanzibar. Hapo kuwa makini, wengine hawasemi kuwa wanapatikana wapi ukimfata inbox au ukimtext kuwa unahitaji bidhaa ataanza yeye kukuuliza kuwa unapatikana wapi ili ataje eneo tofauti na ww ulilopo ili mwisho wa siku utakiwe kutuma pesa atume mzigo.

Ukichumguza kwa makini utagundua picha za bidhaa ni za kudownload. Ila muhimu ni vyema kwa mara ya kwanza pendelea kama unajamaa yako mkoa husika ampelekee bidhaa yeye then jamaa yako akutumie.

Pendelea kujua bei halisi ya bidhaa. Mfano bidhaa fulani inauzwaga laki moja unakuta mtu ameweka bei nusu yake. Embu shtuka hata ww mwenyewe hujiulizi.(hapa nazungumzia kwa bidhaa mpya)
Siku hizi comment huwa wanafunga kwanini ufunge comment?? Hapo pia pita mbali.
 
Wauzaji pia sio waaminifu.. ndo maana wateja tunakua na maswali mengi ili kujiridhisha na huduma mkuu..
Imagine kuna mzgo nmeagiza kutoka dar tangu J3 ya wiki iliyopita, ila cha ajabu mpaka leo muuzaji hajautuma.

Uaminifu wenu ni ZERO
 
Sijui hata nani kawaloga. Unaweka maelezo yote kamili bei na njia ya mawasiliano etc.

Anakuja mtu anakuuliza maswali ambayo majibu yake kwenye maelezo ulishaweka. Yaani mwisho wa siku ni usumbufu tu.
Boss kabla ya kufanya business online unatakiw uwe na elimu ya customer care... je hy elimu unayo maan hii nchi haina watu wanaofanan akil kila mmoja na akil zake
 
Boss kabla ya kufanya business online unatakiw uwe na elimu ya customer care... je hy elimu unayo maan hii nchi haina watu wanaofanan akil kila mmoja na akil zake
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.
 
Sijawahi kuona wafanyabiashara wapuuzi kama wa Online katika hii nchi! Anaweka product na kazi yake tu ila specifications hamna na bei haweki anataka umpigie simu au uende inbox. Sasa unauza kitu ambacho thamani yake huijui ama! Hii tabia inakera mno mbadilike.
 
Biashara online hata Sellers wenyewe wana mbambamba na ugaigai ,ukijichanganya tu wanasepa na mshiko ,kwahiyo lazima uhoji sana ili kujua kama ni muuzaji kweli au tapeli ,na mara nyingi matapeli hawataki kuhojiwa sana ukimdadisi sana tu lazima apanic.
 
Una tatizo la anger management. Hufai kuwa kitengo cha Customer Service utakuwa unaharibu sana. Kwa msaada zaidi soma types of Customers. Mi ukinilitea mawenge nakupa spana live bila chenga na biashara inakufa.

Jenga mentality mteja ni kama mtoto tu, kuna wanaoelewa fasta na kuna wanaochelewa kuelewa.
 
Ingawa niweke wazi kuna baadhi ya wauzaji hawana elimu ya vile vitu wanavyoviuza hii hata physically nimegundua. Unaiona bidhaa unamuuliza kuhusu baadhi ya sifa zake hata hajui hizo sifa ni kitu gani.

mfano mtu anauza computer anachojuanyy ni ram na hdd tu. unamuuliza hii processor ni i5 gen ya ngapi hajui.

mtu anauza simu anachojuayeye ni Ukubwa wa kamera ram na Storage tu.
 
Hili nalo ni tatizo, deep knowledge ya product na benefits inahitajika kabla hujaanza kumshawishi mtu ainunue.
 
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.
boss kuna kitu umekikosa kwny elimu ya biashar ila inaonesha unahic unacho iko kitu..

kazi njema mkuu
 
Jiwe gizani

Wasumbufu wameguswa hapo juu

Ukiona blue ticks kwenye whatsap yangu unaweza ukaacha kabisa online business

Mtu anakuja na screenshot yenye bei Halafu anakuuliza bei gani?

Umeandika location anauliza unapatikana wapi

Picha umeweka anaomba picha zaidi

Wengine wanaomba mpaka feedback kutoka Kwa wateja wengine [emoji119]
 
Hahahaha lazma awe mkali ili upunguze maswali utume hela. Ogopa sana wale wanaojifanya duka liko Zanzibar utalia kilio cha samaki
Biashara online hata Sellers wenyewe wana mbambamba na ugaigai ,ukijichanganya tu wanasepa na mshiko ,kwahiyo lazima uhoji sana ili kujua kama ni muuzaji kweli au tapeli ,na mara nyingi matapeli hawataki kuhojiwa sana ukimdadisi sana tu lazima apanic.
M
 
Sijawahi kuona wafanyabiashara wapuuzi kama wa Online katika hii nchi! Anaweka product na kazi yake tu ila specifications hamna na bei haweki anataka umpigie simu au uende inbox. Sasa unauza kitu ambacho thamani yake huijui ama! Hii tabia inakera mno mbadilike.
Nakiri hili wengi wa wauzaji wana hii shida.
Kingine hawazijui vyema bidhaa wanazo ziuza, hili bila shaka hata upande wa physically umeligundua.

Ila hili nimelizungumzia kwa upande wangu. Unakuta nimeweka kila kitu bayana. lakn kinachonishangaza mtu anakuja kukuuliza maswali ambayo kwenye description nilishaweka.

Kuokoa muda nishanunua vitu vingi online kama maelezo yameshiba basi sinaga mambo mengi ni simu tunajadili bei then mzigo unaletwa.
 
Ila mkuu, sometimes mtu anakua anataka maelezo ZAIDI kuhusu ulichokitangaza, so wavumilie tu mzee
 
Back
Top Bottom