Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

mwingine alikuja inbox maswali mengi nikawa namjibu kama ilivyopaswa.
kaomba na picha za kutosha nikamtumia ile bidhaa ilikuwa juu ya meza. mwisho wa siku ananiuliza "hiyo meza vipi huuzi?"🙌🙌😂

Yaani tutoke kwenye kujadili bidhaa husika tuanze kujadili meza tena.
 
Biashara ya nguo naona itanipasua kichwa aisee. Ukiweka za aina hii watu wazima wanasema hizo ni za vijana. Ukileta za vijana watu wazima wanakuambia sivai Modo[emoji28]
Ngoja nihamie kwenye simu tu au niuze vyote kwa pamoja. Advice??

Biashara ya nguo ni ngumuu hata physically

Yaani watu wana machaguo unaweza ukachanganyikiwa atleast wanaume kidogo

Ila za kike[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Sijawahi kuona wafanyabiashara wapuuzi kama wa Online katika hii nchi! Anaweka product na kazi yake tu ila specifications hamna na bei haweki anataka umpigie simu au uende inbox. Sasa unauza kitu ambacho thamani yake huijui ama! Hii tabia inakera mno mbadilike.
Mkuu wanafikiri sisi wanunuzi hatujielewi.
Ukiuliza ugomvi unakuja ,japo sio wote kuna watu wako vyema sana kwa taarifa.
 
Mbona hata physical ni hivyo hivyo tu, siye wauza genge anakuja bidada anaminyaminya nyanya halafu ananunua biringanya.
Sisi wauza urembo unakuta mdada anataka wanja anachagua mmoja anautest halafu anarudisha anachukua mpya ambao haujaguswa ndio ananunua ule aliotest anakuachia .Hii tabia wanafanya hata kwa bidhaa nyingine pia .
 
Sijawahi kuona wafanyabiashara wapuuzi kama wa Online katika hii nchi! Anaweka product na kazi yake tu ila specifications hamna na bei haweki anataka umpigie simu au uende inbox. Sasa unauza kitu ambacho thamani yake huijui ama! Hii tabia inakera mno mbadilike.
Nje ya mada mkuu. Scenario ya mtoa inahusu kuweka maelezo kamili.
 
Mkuu tafuta kitu kingine ufanye. Biashara huwezi.

Unalalamika maswali ya wateja? We ulitakaje yaani, mtu anunue tu bila kujiridhisha?

Kila mtu Hela yake inamuuma aisee, hakuna Hela za kutoa toa tu. Hata mtu akikuuliza swali lile lile mara elfu we mjibu. Acha kujiona matawi wakati Hela ya mteja unaitaka
Kuna mbwa mmoja anauza vipodozi kawe kuna siku mamilow kanituma nimfuatie. Yule mshenzi nimepanda gari hadi kawe kanisani. Ofisi yake iko karibu na lile eneo. Kunielekeza akawa anaona usumbufu akaanza ukali nikamchenjia maana alizidi.

Kuelekeza hajui halafu akawa analazimisha niingie nyumba ambayo sijui kama ndio yenyewe namwambia toka nje ya geti anakaza nikamwambia kama hilo hawezi mi niondoke zangu tusibishane sana. Akamtuma mtoto akasimama nje ya geti na kuniita.

Sikutaka hata kuonana nae wala kuingia ndani niliamuru nipewe bidhaa husika niondoke haraka iwezekanavyo. Basi mineno ikawa inamtoka huyo mama huko ndani, Oh hii ofisi yangu ina utaratibu sio mtu unakuja kunipangia, watu wote wanaingia ndani wanaelekezwa sijui blah blah. Nikamjibu wenye ofisi wako Bagamoyo Road sio uswahilini kawe tena kwenye makazi ya watu 😂😂😂 akasonya nikachukua zaga nikasepa.

Tangu siku hio nimemwambia bibie biashara ya kuniagiza nikuchukulie vitu vyako vya order kama hawakuletei sintofanya upuuzi huo.
 
Nilichogundua biashara ya online. Watu hawasomi yale maelezo unayoandika. Kama umeweka link ya whatsaapp ye anaingia tu na kuanza kukuuliza habari ambazo uliandika kwenye tangazo. Unatakiwa kulijua hilo japo linakera. Unaweza kuweka Lists yote ya bidhaa ulizonazo lakini mtu akauliza kingine kabisa, pengine amekitafuta sana hivyo anajaribu tu kwa matumaini. Hilo nalo ulijue na usamehe.

Pia tambua kuweka maelezo mengi siyo kwamba ndiyo utaepuka wingi wa maswali. Ni bora ukaweka machache yanayoenda kwenye points, ambayo mtu hataona uvivu kusoma.

mwisho, hiyo ni biashara, haulose kitu ukimhudumia bila makasiriko. Zaidi zaidi anaweza kukuletea wateja zaidi
 
Hahahaha lazma awe mkali ili upunguze maswali utume hela. Ogopa sana wale wanaojifanya duka liko Zanzibar utalia kilio cha samaki

😁😁 Umenikumbusha mwana wa hapo zenji anayeuza Ducati 900 SS kwa $2000 afu hatukaki maswali na location anasema tu zenji hamna maelezo zaidi.Nikamcheki tu nikasema hiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Nilichogundua biashara ya online. Watu hawasomi yale maelezo unayondika. kama umeweka link ya whatsaapp ye anaingia tu na kuanza kukuuliza habari amabazo uliandika kwenye tangazo. Unatakiwa kulijua hilo japo linakera. Unaweza kuweka Lists yote ya bidhaa u;lizonazo lakini mtu akauliza kingine kabisa, pengine amekitafuta sana hivyo anajaribu tu kwa matumaini. Hilo nalo ulijue na usamehe.

Pia tambua kuweka maelezo mengi siyo kwamba ndiyo utaepuka wingi wa maswali. Ni bora ukaweka machache kwenye point ambayo mtu hataona uvivu kusoma.

mwisho, hiyo ni biashara, haulose kitu ukimhudumia bila makasiriko. Zaidi zaidi anaweza kukuletea wateja zaidi
itakuwa kweli hawasomi ni mtu anatazama tu picha then huyo direct anakuja inbox
 
Hawa wauzaji wa viatu na saa classic Instagram na WhatsApp sitaki hata wasikia...WENGI WANAUZA FAKE VITU. Bongo wakweli wachache Sana..saa ya sh 170,000 imevaliwa Mara 3 kwa special occasion imekufa na rangi imeanza kuchubuka...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sasa unanunua Rolex kwa tsh. 170,000 unategemea Nini mkuu?
 
Biashara online hata Sellers wenyewe wana mbambamba na ugaigai ,ukijichanganya tu wanasepa na mshiko ,kwahiyo lazima uhoji sana ili kujua kama ni muuzaji kweli au tapeli ,na mara nyingi matapeli hawataki kuhojiwa sana ukimdadisi sana tu lazima apanic.
Kwa hiyo mkuu tuhitimishe kwamba hata mleta mada ni mgaigai na kirusi hamuachi mtu salama?
 
Tena kama vitu vya electronics ni muhimu unaweka tu model.
me vitu vya electronics ninachokifanya huwa naomba tu model naingia mtandaoni naangalia zaidi sifa zake, hii ni kwa wale wanauza kitu kipya.
then nakuwa nimejirudhisha bila kuwa na maswali mengi kwa muuzaji nikirudi kwake ni kujadili bei na jinsi ya kuipata basi.
Customer reviews hua hauangalii?
 
Back
Top Bottom