Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Mkuu tafuta kitu kingine ufanye. Biashara huwezi. Preferably ingia jeshi au tafuta makampuni ya ulinzi uombe kazi

Unalalamika maswali ya wateja? We ulitakaje yaani, mtu anunue tu bila kujiridhisha?

Kila mtu Hela yake inamuuma aisee, hakuna Hela za kutoa toa tu. Hata mtu akikuuliza swali lile lile mara elfu we mjibu. Acha kujiona matawi wakati Hela ya mteja unaitaka
 
Ingawa niweke wazi kuna baadhi ya wauzaji hawana elimu ya vile vitu wanavyoviuza hii hata physically nimegundua. Unaiona bidhaa unamuuliza kuhusu baadhi ya sifa zake hata hajui hizo sifa ni kitu gani.

mfano mtu anauza computer anachojuanyy ni ram na hdd tu. unamuuliza hii processor ni i5 gen ya ngapi hajui.

mtu anauza simu anachojuayeye ni Ukubwa wa kamera ram na Storage tu.
Watu kukuhoji unaita ujinga? Punguza ujuaji mzee! Huko AliExpress kwenyewe pamoja na details zote za bidhaa kuwekwa bado seller anahojiwa na anatoa ushirikiano mujarabu. Wewe unadai eti ni ujinga jirekebishe mzee online business inataka uwe smart
 
Sijawahi kuona wafanyabiashara wapuuzi kama wa Online katika hii nchi! Anaweka product na kazi yake tu ila specifications hamna na bei haweki anataka umpigie simu au uende inbox. Sasa unauza kitu ambacho thamani yake huijui ama! Hii tabia inakera mno mbadilike.
Huwa inakera sana, biashara za online wafanyabiashara wa kibongo bado sana
 
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.
Acha hizo mkuu,hapo juu Achimwene wa Makete kaelezea vizuri,ni tabia ya wateja kujihakikishia anachohitaji kabla hajatoa pesa yake,inatokea hata kwenye maduka,unaingia dukani unamwambia muuzaji nipe simu ile unaiangalia,then unamwabia nipe na ile unaiangalia,then unaondoka kabisa bila hata ya kununua,sasa hapo ukinuna utawanunia wangapi,kifupi wengi wenu customer care hamuijui,mnakurupuka tu kufanya hizo biashara...
 
Watu kukuhoji unaita ujinga? Punguza ujuaji mzee! Huko AliExpress kwenyewe pamoja na details zote za bidhaa kuwekwa bado seller anahojiwa na anatoa ushirikiano mujarabu. Wewe unadai eti ni ujinga jirekebishe mzee online business inataka uwe smart
Daah sasa mkuu unahoji vipi mambo ambayo kwenye maelezo ya bidhaa yapo mkuu.
AliExpress, Kikuu hadi now nanunua bidhaa. kwa asilimia zote me huwa natafuta description tu na kwa kiasi kikubwa inakuwa imejitosheleza.

Si kwa ubaya ila huwa inaboa imagine mtu anakuja inbox anakuomba no ya simu wakati ulishaiweka kwenye tangazo. tena kwa maandishi makubwa na yamekolezwa rangi.
 
Wateja watalaumiwa bure,
Ila Tatizo linaanzia kwa wauzaji wenyewe,

Wengi wao Hawana elimu ya marketing, maswali kdg mteja anakudadisi, tayar muuzaji ushapanic.

-Sasa asipokuuliza maswali wewe,unadhani atamuuliza Nani?

- Unadhani Kuna mjinga atatoa pesa mfukoni kirahisi kulipia bidhaa ambayo hajajiridhisha uhalali,ubora na uaminifu nayo?
 
Mwingine anaweka tangazo, Bei haweki.
Anaaandika TU "serious buyer, check my pm"

Unabaki kujiuliza,
huyu mtu anaakili kweli?

Hivi Ni wangapi wataingia pm kwake?
Hajui kua wengine hushawishika kununua Kwasababu Bei iko chini?
 
Biashara ya nguo naona itanipasua kichwa aisee. Ukiweka za aina hii watu wazima wanasema hizo ni za vijana. Ukileta za vijana watu wazima wanakuambia sivai Modo😅
Ngoja nihamie kwenye simu tu au niuze vyote kwa pamoja. Advice??

Diversification kwenye biashara muhimu sana usitegemee biashara moja mauzo yanaweza kushuka au wateja wakapungua kwa sababu ya competition ile nyingine ikakubeba.

Ndio maana unaona watu kama akinaa Mo na Bakhresa hawaridhiki tu na biashara moja

Ushauri wangu kama mtaji unaruhusu uza vyote kwa pamoja
 
Una tatizo la anger management. Hufai kuwa kitengo cha Customer Service utakuwa unaharibu sana. Kwa msaada zaidi soma types of Customers. Mi ukinilitea mawenge nakupa spana live bila chenga na biashara inakufa.

Jenga mentality mteja ni kama mtoto tu, kuna wanaoelewa fasta na kuna wanaochelewa kuelewa.
Sahii kabisa,
Unapodeal na wateja unadeal na Aina za watu tofauti, Kama Huwezi kunyumbulika kuendana nao wote lazima biashara uione ngumu[emoji4]
 
Ingawa niweke wazi kuna baadhi ya wauzaji hawana elimu ya vile vitu wanavyoviuza hii hata physically nimegundua. Unaiona bidhaa unamuuliza kuhusu baadhi ya sifa zake hata hajui hizo sifa ni kitu gani.

mfano mtu anauza computer anachojuanyy ni ram na hdd tu. unamuuliza hii processor ni i5 gen ya ngapi hajui.

mtu anauza simu anachojuayeye ni Ukubwa wa kamera ram na Storage tu.
[emoji4][emoji106]
 
Biashara ya nguo naona itanipasua kichwa aisee. Ukiweka za aina hii watu wazima wanasema hizo ni za vijana. Ukileta za vijana watu wazima wanakuambia sivai Modo😅
Ngoja nihamie kwenye simu tu au niuze vyote kwa pamoja. Advice??
Tena kama vitu vya electronics ni muhimu unaweka tu model.
me vitu vya electronics ninachokifanya huwa naomba tu model naingia mtandaoni naangalia zaidi sifa zake, hii ni kwa wale wanauza kitu kipya.
then nakuwa nimejirudhisha bila kuwa na maswali mengi kwa muuzaji nikirudi kwake ni kujadili bei na jinsi ya kuipata basi.
 
Back
Top Bottom