Kuna mbwa mmoja anauza vipodozi kawe kuna siku mamilow kanituma nimfuatie. Yule mshenzi nimepanda gari hadi kawe kanisani. Ofisi yake iko karibu na lile eneo. Kunielekeza akawa anaona usumbufu akaanza ukali nikamchenjia maana alizidi.
Kuelekeza hajui halafu akawa analazimisha niingie nyumba ambayo sijui kama ndio yenyewe namwambia toka nje ya geti anakaza nikamwambia kama hilo hawezi mi niondoke zangu tusibishane sana. Akamtuma mtoto akasimama nje ya geti na kuniita.
Sikutaka hata kuonana nae wala kuingia ndani niliamuru nipewe bidhaa husika niondoke haraka iwezekanavyo. Basi mineno ikawa inamtoka huyo mama huko ndani, Oh hii ofisi yangu ina utaratibu sio mtu unakuja kunipangia, watu wote wanaingia ndani wanaelekezwa sijui blah blah. Nikamjibu wenye ofisi wako Bagamoyo Road sio uswahilini kawe tena kwenye makazi ya watu 😂😂😂 akasonya nikachukua zaga nikasepa.
Tangu siku hio nimemwambia bibie biashara ya kuniagiza nikuchukulie vitu vyako vya order kama hawakuletei sintofanya upuuzi huo.