Kufanya kazi vijijini nilikuwa nasikiaga tu kwa jirani


Dah Laki mbili tu nikiangalia mimi nimeingiza hio pesa kwa siku na bado natamani ingezidi zaidi ya hivyo
Mungu akufanyie wepesi,usichoke kumuomba
 
Mkuu,vumilia.Ajira zenyewe ni ngumu mnoo.Wakati naajiriwa mara ya kwanza nilipangwa kikazi wilaya fulani vijijini.Kwa ujana,sijui ni utoto,niliondoka na kuacha kazi kwa urahisi/ujinga tu.Kilichofuata baada ya mwaka mmoja tu,nilijuta.Usifanye kosa nililolifanya miaka zaidi ya 22 iliyopita.Vumilia na utafunguliwa njia yenye neema tu.
 
Kuna fursa ya hela mfano mazao au hakuna?

Kama kuna fursa ya kilimo na mazao, hayo mengine ni ya kawaida tu wewe ndio unatakiwa uyabadilishe hayo mazingira.

Chumba ulipe elfu tano halafu ushindwe kukarabati na kupulizia dawa, huku ukijipanga kujenga yako huko huko?

Mshahara unalipwa halafu ushindwe kufungua saluni ya kisasa?

Usikubali mazingira yakutawale, bali yatawale mazingira.
 
Hao manesi kama ni ke na dk ni me panakalika vizuri sana.
 
Pole sana mkuu kikubwa pambana usikate tamaa
 
Hivi na Nyie mnaamuamini huyu?
Kuna Ajira gani Ya 200k? Hata Mwl wa Cheti sidhani kama anapata chini ya 400k.
 
OK acha kazi urudi nyumbani kuna umeme.
 
Nimependa saana ushauri wako. Kuna watu wanbwabwaja tu humu hata hawana la maana kumshauri jamaa..

Kuna jamaa alifika kijijini kuripoti, ndo kijijini kwangu na mimi nikiwa huko.

Aliponiona akaona nafanana kuongea naye. Akaniulizia shule ya sekondari ilipo. Sikuwa na noma, nikaazima boda ya mshikaji. Nikamkimbiza hadi shuleni bure.

Kwa siku chache nikiwa kijijini alikuwa karibu nami akilalamikia mazingira. Nilimshauri anunue lau eka moja apande miti, itamsaidia.

Kweli, jamaa alifanya hivyo. Siku hizi ukimwambia ahamie mjini kawa mkali kama mbogo. Ana ekari za miti kama 100 hivi na ameshaamua kustaafia huko. Kanunua kiwanja, kajenga na ana biashara yake inayolinda mshahara wake. Kifupi kaniacha kimaisha.

Siku zote ukifika mahali usianzie kugundua udhaifu wa mazingira. Anza kugundua nguvu au uwezo wake (fursa). Anza kupambana. Mengine yakukute ukiwa vitani.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kwanini usisakafie vema, piga dari safi, dawa za mchwa zipo. Panda maua na mboga nje hadi wenyeji wakuone kweli wewe mwalimu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
nyie si ndo mnaimba Tz ya samia inawaka waka ....kula chuma hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…