Kufanya kazi vijijini nilikuwa nasikiaga tu kwa jirani

Kufanya kazi vijijini nilikuwa nasikiaga tu kwa jirani

Pole sana. But shukuru kwamba angalau una sehemu ya kupatia maokoto. Ever heard about Acres of Diamond?

Kuna wengine wengi tu wanatamani japo robo ya kile ulicho nacho wewe, na hawajahi kukipata -- mchana kutwa, usiku kucha wanahangaika miaka nenda rudi.

NB: Jaribu wewe mwenyewe kuwa badiliko unalotamani kuliona ulimwenguni.

Again, pole sana. It's never a laughing matter.
 
Yamenikuta natamani kulia, nimepata ajira somewhere jamani chumba ni wadudu tu mda wote hata raha hamna masisimizi kibao hadi kitandani, kipindi cha mvua kinaanza chumba kinavuja, majongoo yanaingiaga ndani unaweza sema Niko nje.

Ajira ajira za vijijini ni mateso hapa ninavyoongea umeme hamna nimebakiwa na asilimia 5% umeme umekata tangu SAA 5 Asubuhi.

Nilikuwa nasikia tu ajira za vijijini sasa najionea kwa macho huduma za kijamii chache mateso!!! mateso!!! Saluni zao za kunyoa sasa ha ha ha jamani jamani mchwa wametawala chumba cha kinyozi hakuna capeti ni vumbi mlangoni limewekwa pazia tu unaweza sema uko mgahawani.
Tafuta dawa ya wadudu kuna ile ya unga inasaidia sana kukimbiza wadudu, pia tafuta solar ndogo kwa ajili ya taa na back up umeme ukikatika

Mwisho wa siku pambana tu, bora wewe upo leo 2023 sisi wazee wetu walisomeshwa miaka hiyo ya 60's baada tu ya uhuru

Sasa pata picha ya vijiji vya enzi hizo, mbona sasa hivi kuna afadhali kubwa sana hivyo komaa tu
 
Acha Uchafu kwa kigezo Cha kusingizia kijijini.

Mbona vijijin tunaishi kwa Amani kabisa
Hapana mi ni msafi sana mazingira tu sio mazuri chumba ni gofu tu ukideki Asubuhi ukirudi job SAA Tisa chini mchwa washajenga,sema nyumba zao ni za zamani sana,chumba ninacholala kina ufa juu mpaka chini nakiogopa sijui kama hakitanidondokea na mvua zinazoanza na upepo mkali acha tu rafiki angu usicoment ivi mimi naishi mazingira magumu sana mshahara laki mbili tu.
 
Kuna zahanati ipo simiyu..ina manesi wawili tu...kila daktari akipangiwa kule anakimbia....
Umeme upo
Network hakuna yakutafta tafta
Wananchi wanaanzia kwa waganga kwanza alafu zahanati
Maji ya bwawani
Kijijini pasikie tu kwa mwenzio..kijana ukienda uko hutoboi
Ileje pasikie tu.....pazuri sana. Sema watumishi hujitenga Sana na wenyeji wakihofia kurogwa na wandali. But pako poa
 
Fanya kazi ukibadilishe hicho kijiji.Hili lote la kulalamika linachangiwa na malezi.Hapo ulipo ukiamua unaweza kuwa tajiri kutokana na hayo mazingira.Mbona mchaga akipangiwa kazi kijijini hata kama ni pagumu anaenda na anatoboa.
 
Kama ana uwezo wa kununua hiyp TVS basi atakuwa na uwezo wa kupata nyumba ya afadhali kidogo. Labda kama hicho kijiji nyumba zote zipo hivyo..

Malazi bora ni muhimu kwanza.
Hakika, Kama amefanikiwa kuwa mtumishi maana yake ni atakua na kipato fulani kinachokidhi mahitaji na ataweza kununua pikipiki.
Akitokea eneo tofauti na hapo mahala pa kazi ni muhimu zaidi na kunapunguza mengi.
 
Yamenikuta natamani kulia, nimepata ajira somewhere jamani chumba ni wadudu tu mda wote hata raha hamna masisimizi kibao hadi kitandani, kipindi cha mvua kinaanza chumba kinavuja, majongoo yanaingiaga ndani unaweza sema Niko nje network hakuna ni baadhi tu ya maeneo network inakamata.

Ajira ajira za vijijini ni mateso hapa ninavyoongea umeme hamna nimebakiwa na asilimia 5% umeme umekata tangu SAA 5 Asubuhi.

Nilikuwa nasikia tu ajira za vijijini sasa najionea kwa macho huduma za kijamii chache mateso!!! mateso!!! Saluni zao za kunyoa sasa ha ha ha jamani jamani mchwa wametawala chumba cha kinyozi hakuna capeti ni vumbi mlangoni limewekwa pazia tu unaweza sema uko mgahawani.
Shikamoo Mwalimu wa zamu, vumilia utazoea, huko ni pazuri kwa kubana mshahara, tena hata hautakuja kutamani kuondoka huko
 
Back
Top Bottom