Kufanya ngono kabla ya ndoa ni dhambi au sio dhambi?

Kufanya ngono kabla ya ndoa ni dhambi au sio dhambi?

kwani amri za Mungu moja wapo si inasema usizini? na wimbo uliobora pia unasema usiyachochee mapenzi mpaka yatakapo ona vyema yenyewe



ila hata mimi siwezi olewa na mtu sijajua kama yaliyomo yamo au hayamo
si ndo hapo sasa. Mara nikakute bwawa tuanze kuachana
 
Pale mlimani walisemwa wazinzi tu, waasherati hawahusiki 😂

Au labda inaingia kwenye “usitamani vitu vya jirani yako”?
😂😂 unataka kusemaje kwa wavunja amri ya 6? Sio waasherati?

Cha jirani umetamani kikojoleo chake au😆
 
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala ...
waasherati ni wale waliokwisha ingia kwenye ndoa alafu wakachepuka
 
waasherati ni wale waliokwisha ingia kwenye ndoa alafu wakachepuka
Hawa mi nafahamu ni wazinzi, kuna comment ya member huko juu amesema waasherati ni neno jumuishi, ngoja waje Bakita……
 
Wagalatia 5:19-21

19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu.


Ukisoma hapo utakutana na neno UASHERATI, hivyo kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa ni dhambi.
Kwahiyo maana ya Uasherati ni kufanya mapenzi kabla ya Ndoa ?? 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom