GE2025 Kufarijiana kunaendelea kule Bumbuli karma ipo kazini siku zote

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
9,414
Reaction score
6,029
Nakumbuka namna Mzee Makamba alivyokuwa akitokwa na maneno mazito kiasi cha meza kuu yote kuinama chini kwa kujawa na aibu, waliingiwa na tahayari (uncomfortable) ya wazi usoni mwao.

Mzee Makamba akasema wema huwa hawafi huku akichombezwa na vicheko vilivyokuwemo mle ukumbini. Lakini miongoni mwa waliomsikiliza alikuwepo mjane wa hayati John Pombe Magufuli ambaye naamini hakuamini kile alichokuwa akikisikia kikisemwa katika mtindo wa maneno ya mipasho.

Muda umepita na kile kiburi cha Mstaafu Makamba kimemrudia ndani ya Familia yake baada ya kijana wake mara mbili kupigwa chini na CCM. Naamini Rais Samia alitumia busara ya kupitisha kifungu katika mkutano maalum wa mtandaoni ili kujipunguzia maadui kwa kuyarudisha majina ambayo yalishakatwa hapo awali. Likiwepo jina la mtoto wa mkongwe Makamba.

Majina mapya ya wagombea wamesomwa jana na kwa mara nyingine halipo jina hilo la Mheshimiwa aliyepigwa chini kwenye uwaziri. Malipo yanakuwa hapa hapa juu ya uso wa dunia. Hausubiriwi ukakata roho ndio ukutane na moto wa milele unaanza kuuhisi mvuke mkali wa moto ukiwa bado unapumua.

Inawezekana muda huu ndani ya nyumba ya Mzee Makamba huko Bumbuli vichwa vimeinamishwa chini na chakula kinaliwa kwa huzuni na maswali mengi yasiyojibika yanaulizwa bila ya kuwepo kwa majibu. Tulikosea wapi?, mchawi wetu ni nani?, hata JK kashindwa kweli kumshawishi Samia mpaka jina limekatwa?.

Mzee Makamba katika uzoefu na hazina ya uzee wake alishindwa kabisa kuufahamu udhaifu wa mwanae kiutendaji. Habari za nyuma ya kapeti zinadai Samia alikerwa na namna Makamba alivyoamua kuingilia masuala ya utendaji wa Mamlaka ya Anga TCAA kwa kuamua kumpigia simu Waziri wa mambo ya nje wa Kenya ili watatue tatizo wakati mamlaka zipo na siku zote zinatatua zenyewe bila ya kuingiliwa!.

Baada ya Samia kukerwa ilikuwa ni suala la muda tu Makamba apigwe chini. Zile tambo za Baba yake mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu zisingeweza kumsaidia chochote, maji yalishamwagika.

Karma ipo kazini na Mungu ndiye anayeijua adhabu ambayo binadamu anaistahili na muda upi akutane nayo. Fitina za kupenda kuzungukana zina mwisho wake.

Mheshimiwa alikuwa na ndoto za kugombea urais wa JMT siku moja akiwa hai lakini ubunge wa jimbo lake umekuwa mtihani mkubwa.
 
Huyu mzee ni mshenzi na shetani mkubwa, mwasisi wa huu mfumo mbovu wa laana wa kuumiza watu akijua atakuwa salama yeye na familia yake kwenye mfumo maisha yao yote, pumbavu sn sijui anasubiri ni nini kufa?
Alimkejeli marehemu JPM akitaka kumfurahisha Kikwete aliyekuwemo mle ukumbini, kumbe kijana wake hana uwezo wa utendaji amejaa kujikweza na tabia za ujana za kuwasagia washindani wake.
 
Nakumbuka namna Mzee Makamba alivyokuwa akitokwa na maneno mazito kiasi cha meza kuu yote kuinama chini kwa kujawa na aibu, waliingiwa na tahayari (uncomfortable) ya wazi usoni mwao.

Mzee Makamba akasema wema huwa hawafi huku akichombezwa na vicheko vilivyokuwemo mle ukumbini. Lakini miongoni mwa waliomsikiliza alikuwepo mjane wa hayati John Pombe Magufuli ambaye naamini hakuamini kile alichokuwa akikisikia kikisemwa katika mtindo wa maneno ya mipasho.

Muda umepita na kile kiburi cha Mstaafu Makamba kimemrudia ndani ya Familia yake baada ya kijana wake mara mbili kupigwa chini na CCM. Naamini Rais Samia alitumia busara ya kupitisha kifungu katika mkutano maalum wa mtandaoni ili kujipunguzia maadui kwa kuyarudisha majina ambayo yalishakatwa hapo awali. Likiwepo jina la mtoto wa mkongwe Makamba.

Majina mapya ya wagombea wamesomwa jana na kwa mara nyingine halipo jina hilo la Mheshimiwa aliyepigwa chini kwenye uwaziri. Malipo yanakuwa hapa hapa juu ya uso wa dunia. Hausubiriwi ukakata roho ndio ukutane na moto wa milele unaanza kuuhisi mvuke mkali wa moto ukiwa bado unapumua.

Inawezekana muda huu ndani ya nyumba ya Mzee Makamba huko Bumbuli vichwa vimeinamishwa chini na chakula kinaliwa kwa huzuni na maswali mengi yasiyojibika yanaulizwa bila ya kuwepo kwa majibu. Tulikosea wapi?, mchawi wetu ni nani?, hata JK kashindwa kweli kumshawishi Samia mpaka jina limekatwa?.

Mzee Makamba katika uzoefu na hazina ya uzee wake alishindwa kabisa kuufahamu udhaifu wa mwanae kiutendaji. Habari za nyuma ya kapeti zinadai Samia alikerwa na namna Makamba alivyoamua kuingilia masuala ya utendaji wa Mamlaka ya Anga TCAA kwa kuamua kumpigia simu Waziri wa mambo ya nje wa Kenya ili watatue tatizo wakati mamlaka zipo na siku zote zinatatua zenyewe bila ya kuingiliwa!.

Baada ya Samia kukerwa ilikuwa ni suala la muda tu Makamba apigwe chini. Zile tambo za Baba yake mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu zisingeweza kumsaidia chochote, maji yalishamwagika.

Karma ipo kazini na Mungu ndiye anayeijua adhabu ambayo binadamu anaistahili na muda upi akutane nayo. Fitina za kupenda kuzungukana zina mwisho wake.

Mheshimiwa alikuwa na ndoto za kugombea urais wa JMT siku moja akiwa hai lakini ubunge wa jimbo lake umekuwa mtihani mkubwa.
Hivi makamba ni mwenyeji wa mkoa gani
 
Inawezekana muda huu ndani ya nyumba ya Mzee Makamba huko Bumbuli vichwa vimeinamishwa chini na chakula kinaliwa kwa huzuni na maswali mengi yasiyojibika yanaulizwa bila ya kuwepo kwa majibu. Tulikosea wapi?, mchawi wetu ni nani?, hata JK kashindwa kweli kumshawishi Samia mpaka jina limekatwa?.
Mkuu Steven Joel Ntamusano ukweli ni kuwa sasa hivi familia mbili hizi za wastaafu Yusufu Makamba na Jakaya Kikwete haziivi tena kama zamani na hata January kupigwa chini kwenye uwaziri ilikuwa handwork ya JK ili kumsafishia njia mwanawe Ridhwani ya Urais wa JMT siku za usoni na January ndiye alionekana kikwazo. Na hata anguko la pili la January kufyekwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge jimboni kwake Bumbuli JK katia mkono pia, licha ya ukweli kuwa wapiga kura wa Bumbuli wamemchoka January lakini kwa kawaida ya CCM kama mtu ana mkubwa wa kumshika mkono kama ilivyokuwa awali kwa January hata kama wananchi wakimkataa angepitishwa tu na mamlaka za juu.JK ni mzee wa fitna sana na hana rafiki wa kudumu linapokuja maslahi ya familia yake mfano halisi ni alivyomchijia baharini swahiba wake Lowassa ili kumsafishia njia nduguye Bernard Membe.
 
JK anatimiza miaka 75 October mwaka huu, kiakili na kimwili keshaanza kuchoka simuoni akiwa na nguvu sana za kujiingiza kwenye fitina ingawa anayo tabia hiyo ya ujuaji ambayo amezaliwa nayo.

Makamba alimzingua Samia mwenyewe katika masuala ya utendaji huko serikalini, aliingilia mamlaka ya mtu ambaye kwa sasa ni mwanasheria mkuu wa JMT Hamza Johari wakati ule akiwa mkurugenzi wa mamlaka ya anga TCAA. Samia hakupendezwa na ujuaji ule.
 
Back
Top Bottom