Kufariki kwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne Thaqaafa Sec Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 20/03/2022, uzembe wa shule hii umulikwe

Kufariki kwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne Thaqaafa Sec Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 20/03/2022, uzembe wa shule hii umulikwe

Shule nyingi za kiisilamu haziko kwenye viwango vya uendeshaji, unajua Morogoro kuna chuo kikuu kinachomilikiwa na BAKWATA! Wengi hawajui.
Ile shule sio ya kiislamu inapokea madhehebu yote bila ubaguzi japo mkrugezi wao ni muislamu.
 
Wabongo msiwe na haraka ya kusikiliza upande mmoja na kuchukua maamuzi, huyu ni member tu, hatuna uhakika akisemacho.

Mwenye watoto pale au anaetaka kupeleka watoto wake kusoma ni heri awaone thaqafa wenyewe.

Ni maoni yangu.
 
Kapicha hamna tuione hiyo shule..
.
810241594.jpg
393881010.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
iyo ni shule ni kongwe sijui wanakwama wapi,ilipo shule na hospitali ya mkoa Sekou toure ni pua na mdomo.
 
Halafu siku hizi wameshuka sana hata kwenye matokeo dawa ni kutopoleka watoto tu, halafu hii shule iko mjini kabisa kutoka thaqafa hadi seketure ni dk 10 tu, kwenda Mwanza hospital dk 5, Uhuru hospital dk 10, mtoto anakufaje bwenini?
Sijui Imepatwa na nini siki hizi...

Zamani walikuwa wanashindana na Taqwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu sasa ni upuuzi, kama mtu anasema anaumwa, si umpeleke kwenye hospitali hiyo iliyokaribu ili apimwe, kama haumwi anasingizia si itaonekana tu? Sasa hiyo kuzurura inatoka wapi? Wawajibishwe haraka sana! Halafu angalieni na majina ya shule , ‘Thaqaafa’ , just imagine..
Mmh ohooooo

Ova
 
Shida inaletwa na madam Opiyo kwanini anafanya maisha kuwa magumu kwa wanafunzi/ wanetu?

Hii haipo sawa inaleta shida na mvunjiko wa Mila shule ni mult religious why christians have no place for religious while Islamic have?

This isn't fair wewe unadhani watoto hawana dini?

Tuwe fair
 
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Mimi ni mzazi ambaye watoto wangu kadhaa wanasoma shule tajwa iliyopo jijini Mwanza.

Kwa huzuni kubwa naandika ujumbe huu kulaumu uongozi wa ThaqaafseSec kwa uzembe ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara watoto wakiumwa nyakati za usiku kwa wale wa bweni huwa hawapewi ruhusa kwa kudhaniwa kuwa wanakwenda zurura.

Hii hata mimi ilinitokea kwa mwanangu last year; alipozidiwa ndipo wakampeleka Hosp yao ya Al ijumaa, tena jirani kabisa na shule nami nikapigiwa simu mida mibovu ilinibidi kufika hosp na kulala na tiba hakupata kwa wakati, wanadai bima nikawaambia anayo hawakunielewa nikahamisha mtt kwenda hospitali nyingine asubuhi yake.

Juzi mtoto wa F4 kafariki kizembe kwa kunyimwa ruhusa na mkuu wa shule Madam Opiyo mpaka kijana akazidiwa kumpeleka hosp ikawa too late leo amezikwa kwao Jijini Mwanza.

Nitoe rai kwa Mzee Magongo, kamati ya shule, bodi ya shule kufanya tathmini mapema Sana Opiyo & others watatuulia wanetu shule siyo jela na kutupandishia ada bila taarifa mkome mnaanza utapeli, walimu kila leo wanaacha kazi kwa kutolipwa mishahara Ada zetu mnapeleka wapi? Opiyo kazi yake uchawi na wanga tu kwa watoto wetu na kuoga mlangoni mwa ofisi ya meneja Mzee Magongo wakati kitaaluma shule inashuka Bora angebaki Sekitya Yule mganda shule ilikuwa Bomba kitaaluma hili mzee Magongo aliangalie Ila mwakani nahamisha wanangu full stop.
Nina hasira zangu na msiba wa mwanafunzi mniache.

CC Mkuu wa Wilaya Nyamagana
DSEO Nyamagana
KUU Nyamagana
RC Mwanza aione kwa jalada
Angalieni shule za kupeleka watoto wenu, kuna baadhi ya shule watoto wanaenda kuongeza ujinga
 
Back
Top Bottom