Kufuata Bidhaa hapo China kusikufanye ukajiona umeyapatia maisha ukadharau watu!

Una bahati kweli kweli,
 
Bahati nzuri sifanyi biashara direct ila nafanya kwenye kampuni ya mtu naona vingi
 
Madam mambo mazuri! Kuna mda unafeel we ni last born wa Mungu
 
Acha wivu mkuu!
 
Tupe code tuwauzie wanaijeria kesi mkuu...wamfundishe adabu kidogo..
POLE SANA ILA USIKATE TAMAA BRO
 
Naogopa sana fitna kwenye biashara.huwa nawaza sijui itakuaje?
Mkuu fitna zipo mno ni kukabiliana nazo tu, kwenye hizi biashara umakini unahitajika sana hasa hizi za masokoni maana kufilisika na kuanguka kibiashara ni kugusa tu.

Mfano, mchina anazalisha bidhaa leo kwa tsh 2,000, wewe kama supplier/wholesaler unaichukua na kuiuza kwa tsh 2,200. Faida 200.

Kesho unaamka yule yule mchina baada ya kumaliza mzigo wake, anaingiza sokoni bidhaa ile ile kwa tsh 1,700 kwa kumtumia supplier/wholesaler mwingine. Yeye atauza tsh 1,900. Hapo unadhani wauzaji wa mwsho watakimbilia kwa nani kufuata bidhaa?
 
Ni nomaaa mkuu!. Ndio maana wanasema biashara ni vitaa
 
Bahati nzuri sifanyi biashara direct ila nafanya kwenye kampuni ya mtu naona vingi
Mambo ni mengi nimeshafanya ya watu nimeona fitna nyingi, nimefanya yangu nimeona pia mengi. Biashara ni kukomaa haswa vinginevyo utajifia na mapresha au kujikatia tamaa.
 
Biashara risk sana
 
Biashara risk sana
Sana mkuu ukiona mtu kaanzia chini na hana msaada anapambana mwenyewe na kasimama kibiashara ujue kapitia mengi mno. Nna jamaa yangu amepitia mengi mno kwenye biashara ila namuona mbali sana, nlichojifunza kwake ni nidham ya fedha na kutokukata tamaa.
 
Kwahyo umeamua kuloga na wewe...
Hapana mimi sio mlozi ila inapokuja ishu ya kwanini uchukue bidhaa yangu na uache yao kuipamba bidhaa yangu na uongo na kukandia za wengine ni muhimu.

Kwenye zone yenu huko kuna mtu alinifanyia fitna sana nikapoteza uaminifu kwa wateja wangu wakubwa watatu, siku hiyo nilijiskia vibaya mno ila nikakubali uhalisia wa biashara. Kuna muda ni lazima umchafue mwenzio ili uteke soko/uuze vinginevyo utajiuzia mwenyewe au bidhaa zikuharibikie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…