Mkuu fitna zipo mno ni kukabiliana nazo tu, kwenye hizi biashara umakini unahitajika sana hasa hizi za masokoni maana kufilisika na kuanguka kibiashara ni kugusa tu.
Mfano, mchina anazalisha bidhaa leo kwa tsh 2,000, wewe kama supplier/wholesaler unaichukua na kuiuza kwa tsh 2,200. Faida 200.
Kesho unaamka yule yule mchina baada ya kumaliza mzigo wake, anaingiza sokoni bidhaa ile ile kwa tsh 1,700 kwa kumtumia supplier/wholesaler mwingine. Yeye atauza tsh 1,900. Hapo unadhani wauzaji wa mwsho watakimbilia kwa nani kufuata bidhaa?