Kufuatia kauli ya WHO na maono ya Rais Magufuli kuhusu kuizoea Corona naomba shule na vyuo vifunguliwe

Kufuatia kauli ya WHO na maono ya Rais Magufuli kuhusu kuizoea Corona naomba shule na vyuo vifunguliwe

Na isije ikatokea leo mkatangaza sik 3 mbele shule zimefunguliwa,,watoe mda wa kutosha pia,na wawapishanishe yaani waanze watoto wa primary na seckndary baada ya wiki ndio wafungue vyuo,au kinyume chake
Nashukuru kwa kuona jinsi Hali ya corona nchini ilvyozibitiwa. WATANZANIA msikimbilie kumla huyu mbuzi bado tunammalizia kumbanika vizuri. hii aonyesha wazi TANZANIA tunaendelea vizuri hadi watu mtani wakuona na kuamini corona Tanzania Sasa basi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado Corona ipo na inaua sana japo haiwekwi wazi, huku mtaani hali ni mbaya

Labda zifunguliwe July mwanzoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ugonjwa upo na hali ni mbaya kama unavyosema Je unadhani hatua zinazochukuliwa na serikal katika kuukabili huu ugonjwa unadhan mpaka July utakuwa umekwisha na Shule kufunguliwa? Ndio kwanza tunaambiwa tujifunze kuishi nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo.” Kwa tafsiri rahisi ni kwamba lazima tuambizane ukweli -----Nyerere
Kwa huo mtazamo wako ninaouona, manake shule haziwezi kufunguliwa kamwe kutokana na nature au uchumi wa nchi yetu. Umeshaambiwa huenda lisiishe na tukaishi nao Kama magonjwa mengine kikubwa tahadhari. Wenzio tumeshaanza kuishi nao Kama kifaduro. Tunaomba Mungu tu shule zifungue vijana wetu waendelee na masomo huko.

Umezungumzi kusoma kwa njia ya TV halafu hujagusia changamoto zake. Wadogo zangu mpaka leo hawajawahi kushuhudia hicho kipindi huko kijijin waliko. TV yenyewe shida, umeme wenyewe ndo usiseme. Usifananishe unafuu wako kwa mwenzio.

Shule zikifungua wanao ubaki nao kwanza maana watapata Corona[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa huo mtazamo wako ninaouona, manake shule haziwezi kufunguliwa kamwe kutokana na nature au uchumi wa nchi yetu. Umeshaambiwa huenda lisiishe na tukaishi nao Kama magonjwa mengine kikubwa tahadhari. Wenzio tumeshaanza kuishi nao Kama kifaduro. Tunaomba Mungu tu shule zifungue vijana wetu waendelee na masomo huko...

Great, jamii forum ina watu wengi wenye mawazo chanya. Inawezekana hata wanaotoa maoni ya kwamba watoto watakufa huenda hawana hata watoto.

Binafsi nina watoto na wanasoma ngazi zote nawaona jinsi wanavyopata tabu kwenda na kasi ya vipindi ktk TV. Nawaza je wale walioko vijijini hali ikoje? Natambua "practice makes perfect"

Narudia tena lete hoja ni kwa vipi serikali ikiruhusu baadhi ya madarasa yarudi (sio shule mzim) italeta nafuu au italeta athari?
 
Na isije ikatokea leo mkatangaza sik 3 mbele shule zimefunguliwa,,watoe mda wa kutosha pia,na wawapishanishe yaani waanze watoto wa primary na seckndary baada ya wiki ndio wafungue vyuo,au kinyume chake

Sent using Jamii Forums mobile app

Iwe hivyo kabla ya kufungua shule watoe taarifa ya kufungua wiki 2 au 3 kabla wazaz watafute ada, nauli na pesa za kujikimu...

Ikiwezekana wafungue michezo yote, matamasha na shughuri za mikusanyiko ili iwe kipimo Cha kutathimini ueneaji wa huu ugonjwa... Sio kuwafanya watoto majaribio.
 
Ni jambo jema sana kusikia maambukizi yamepungua nchini hasa ukizingatia sisi ni nchi ambayo tuliuchukulia poa sana hu ugonjwa

Kama hizi takiwimu ni za kweli kwa Dar na Pwani kuwa na wagonjwa idadi yao hata hawazidi 50 ni jambo la kushukuru sana

Hakuna tena sababu ya kupoteza muda ni bora shule zifunguliwe maisha yaendelee kama kawaida

Au kama hamziamini takiwimu zenu mnaweza kuanza kufungua madarasa ya mitihani yani darasa la 4 , kidato cha 4 na 6

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachangamke na ligi kuu ya mpira irudi, tunataka tuone vurugu za Haji Manara Simba akipewa kombe lake na taifa pakiwa pamefurika
 
Back
Top Bottom