Kufuatia kauli ya WHO na maono ya Rais Magufuli kuhusu kuizoea Corona naomba shule na vyuo vifunguliwe

Kufuatia kauli ya WHO na maono ya Rais Magufuli kuhusu kuizoea Corona naomba shule na vyuo vifunguliwe

Nashukuru kwa kuona jinsi Hali ya corona nchini ilvyozibitiwa. WATANZANIA msikimbilie kumla huyu mbuzi bado tunammalizia kumbanika vizuri. hii aonyesha wazi TANZANIA tunaendelea vizuri hadi watu mtani wakuona na kuamini corona Tanzania Sasa basi.

Hili linajihirisha kwani hawajazika usiku wala kupotelewa na wapendwa wao wagonjwa bila kuambiwa Ni nini kumewauwa na kuzuiwa kuzika ,serikali sikivu bado inaendelea kujiridhisha mwenendo wa ugonjwa na kuumaliza katika jamii yetu ,Ni swala la muda tuuh na likiwa tayari tutawachia waendele na masomo pamoja na michezo kuendelea huku kampeni zikianza rasmi (wapinzani wasilie ooh atukupewa muda wa kutosha kwani ndiyo ajenda yao kuu hii nimeipata chinichini).

tuchukue tahadhari na kujikinga ili kumaliza kabisaa ugonjwa pia mzidi kupuza habari za UZUSHI wenye nia ya chuki na kuparaganisha jamii yetu ,tule vizuri na mazoezi yakutosha kwani Hali ya hewa Ni safi kwa kukimbia jioni au asubuhi.

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Shughuli ziendelee kama kawa, adui hakimbiwi kwa kujificha ndani
 
Kwani kuna shughuli zilifungwa?


Michezo, ligi kuu irudi bila mashabiki


Wanafunzi waende shule bila walimu
 
Ugonjwa usipoisha elimu ndo basi? Maana nionavyo mimi bora wangemaliza hawa wa darasa la saba, kidato cha sita na kidato cha nne wengine kurudia si mbaya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kuishi pasipo kuwa na elimu,maisha ni bora kuliko elimu,subiri kwanza hali itengemea(herd immunity ifanye kazi kwanza) kisha ndio shule zifunguliwe ,MOH inatoa miongozo ya kuzika watu wenye corona wewe unawaza shule zifunguliwe!!!

Umeshaona graph yetu ya cases na vifo? Vipi inapungua? Elimu bado haijaeleweka kisha unataka vyuo vifunguliwe? Subiri kwanza kama wewe ni teacher mshahara umepigwa pini ni bora ungeshauri serikali itoe stimulus packages kwa shule binafsi ili waweze kulipa mishahara wafanyakazi hata hili mimi naomba serikali iwaangalie walimu wa shule binafsi kwa kweli ikiwezekana hata wapewe NSSF zao katika kipindi hiki waweze kujikimu.
 
Eti shule zifunguliwe hivi inamaana tumewachoka watoto wetu na wadogo zetu kiasi hicho hebu tuache utani kwenye uhai lazima serikali iangalie mwenendo wa huu ugonjwa na ijiridhishe kwamba mazingira ni salama

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina uhakika kama mtoa mada mwenyewe ana mtoto hata wa kusingiziwa...!
 
Unaweza kuishi pasipo kuwa na elimu,maisha ni bora kuliko elimu,subiri kwanza hali itengemea(herd immunity ifanye kazi kwanza) kisha ndio shule zifunguliwe ,MOH inatoa miongozo ya kuzika watu wenye corona wewe unawaza shule zifunguliwe!

Nadhani umesahau kuna shughuli nyingine zenye mikusanyiko zinaendelea kuna masoko, kuna baa, bunge linaendelea, benk zipo wazi hizo ni baadhi ya sehemu ambazo zina mikusanyiko. Kuhusu shule na vyuo ndio masna nikatoa wazo kwa madarasa ya mitihani, labda km huna uelewa wa kutosha kuhusu athari za elimu kwa uchumi.
Msisubiri Wazungu waje wawatolee idea ndio mkubali.
 
Inawezekana kabisa, serikali ijipange kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kufungua shule na vyuo, sina shaka kwa shule ZA boarding tatizo lipo Kwa day schoolers na haswa shule za kata hapo ndipo utaratibu maalum ufanyik
 
Inawezekana kabisa, serikali ijipange kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kufungua shule na vyuo, sina shaka kwa shule ZA boarding tatizo lipo Kwa day schoolers na haswa shule za kata hapo ndipo utaratibu maalum ufanyik

Yes mawazo chanya ya kujenga, tusonge mbele na Mkuu wetu wa nchi
 
Back
Top Bottom