Tanzania imeonyesha ukomavu katika kupambana na janga la Corona, big up kwa Mhe. Rais Magufuli.
Kwa hali ilivyo, imethibitika hata WHO wanakiri uwezekano wa kuishi na corona kwa muda mrefu.
Kama ni hivyo kuna haja ya kuendelea na shughuli zetu huku tukiishi na huyo corona katikati yetu.
Shule hasa kwa madarasa ya mitihani (STD VII, FORM IV, FORM VI, VYUO) yanaweza kuendelea ingawa umakini ndio wapaswa kuongezwa.
Serikali inaweza kuita madarasa hayo na Walimu wao wakiwa na Sanitizer, barakoa kila mtu kama tunavyofanya tukiwa sokoni, benki n.k na kwa vile shuleni idadi itakuwa ndogo ni rahisi kutumia madarasa mengine km sehemu ya kupunguza wingi na ku keep distance.
Maisha lazima yasonge kuna mambo mengi nje ya pazia la corona.
Hatuna budi kuendelea na shughuli zetu japo kwa umakini zaidi kama kifo kimewekwa mbele yetu kipo tu na katika imani tunasmini Mungu ndiye anachagua wa kuchukua roho.
"Maisha na Corona katikati yetu yanawezekana"