blogger
JF-Expert Member
- Mar 13, 2012
- 12,112
- 15,060
Kwanza kabisa naanza kwa kumsalimia Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan kwa heshima zote kabisa maana najua atasoma uzi huu kwani anapita humu na tupo naye.
Ni swali la moja kwa moja tu, kama ni kweli yule DC wa Sumbawanga katolewa kwa igizo lile basi hatuna budi kujitafakari upya lakini pia kuwa watu wa kuhimili mihemko yetu.
Shida ilikuwa ni nini? Kuuvaa uhusika wa kimamlaka kuu au kuleta taharuki? Je, taharuki ilitokea? Kama ishu ilikuwa ni kuuvaa uhusika wa Mamlaka Kuu ya Nchi kwa kuigiza kama Mama (kwa kile kilemba alichovaa) mbona Marais wote nchini huchezwa kimaigizo na wengine huchorwa na sauti zao zinaigwa?
Mbona hii video hapa ilisherekewa.
Kwanini hapo ilikuwa ni sawa na ionekane DC huyu wa Sumbawanga kakosea wakati alikuwa akionesha ukakamavu na utayari wa jeshi la kina mama panapotokea shida.
Sasa maswali mengi tunajiuliza, je, ni watu tu wamejipendekeza ili waonekane au ni fitna tu na husda kwa aliyetumbuliwa?
Bado nachelea kuamini Rais ndio kamtengua huyu DC au la kashauriwa vibaya.