Uhuru wa kisanaa kwa nchi ya marekani ni mpana sana kiasi ambacho hata kucheza filamu za porn kunaruhusiwa, hivyo hata filamu za kiusalama zinatengenezwa sana.
Lakini movie zote za kimarekani huwa zinaigizwa na wasanii (sio maafisa usalama ndani ya serikali yao), hawaruhusu kabisa afisa usalama aende akaigize movie yenye kubeba uhalisia wa uafisa usalama wake. Hiyo kitaalamu inaitwa conflict of interest, ni kinyume cha sheria za uajiri na copyright kwao. Mtu akifanya hivyo tu, mara moja anapoteza kazi na kushtakiwa kulipa fidia kubwa.