Kufuatia kutumbuliwa kwa DC wa Sumbawanga, kuna vitu havipo sawa nchini na ni lazima visemwe

Wewe upo kwenye System unamuelekeza Dunga embee ambae lengo lake ni kubishaa tuu... Achana naee.. Ila kama zilitumika Risasi za moto kabisaa yule DC alipaswa afukuzwee usiku ule uleee yani mapema tu.
Punguza mihemko . Kijana mdogo ww. Utazeeka mapema.

Igizo lile lilikuwa well displayed.. perferctly role played..
 
Atakujibu kwamba hizo ni muvi zinachezwa na Hollywood actors na yule pale alikuwa ni DC wa Sumbawanga .

Hakuna jibu jingine mtu wa CCM anaweza kukupa..
 
Wale ni waigizaji jo. Huyu ni mtumishi wa umma.
 
Uhuru wa kisanaa kwa nchi ya marekani ni mpana sana kiasi ambacho hata kucheza filamu za porn kunaruhusiwa, hivyo hata filamu za kiusalama zinatengenezwa sana.

Lakini movie zote za kimarekani huwa zinaigizwa na wasanii (sio maafisa usalama ndani ya serikali yao), hawaruhusu kabisa afisa usalama aende akaigize movie yenye kubeba uhalisia wa uafisa usalama wake. Hiyo kitaalamu inaitwa conflict of interest, ni kinyume cha sheria za uajiri na copyright kwao. Mtu akifanya hivyo tu, mara moja anapoteza kazi na kushtakiwa kulipa fidia kubwa.
 
Ukiwa kazini au umestaafu, hatatoa siri za jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kuongea, kuandika, kuigiza, kuimba, au kuchora au kwa njia yoyote.


Huyu dc, rso, dso, rpc kamanda wa ffu na ocd wanapaswa muda huu wawe wanatoka kunywa uji butimba, keko na segerda.
 

Wale ni Waigizaji, Wao kama Fanani uhusika wao ni kwenye filamu, hadhira yao haipo kwenye filamu, Ipo kwenye Ulimwengu Halisi ambao ni Sisi.

Je Kwa upande wa DC Fanani uhusika wao umefanyika kwenye Filamu au mazingira halisi? Je hadhira Ipo kwenye filamu au Ipo kwenye mazingira halisi?

Je dhamira juu ya igizo hilo ni ipi?
Ujumbe wake ni upi?
Fanani ambaye yupo kwenye mazingira halisi alitaka hadhira yake ipate ujumbe gani?

Vipi Fanani ni nani na majukumu yake ni yapi katika mazingira halisi?
 
Mkuu, kuna mambo mengi DC anatakiwa kufanya ikiwemo kutatua kero lukuki za wananchi, kuwa na mipango endelevu kama ujenzi wa shule, zahanati, maji nk, sio kuigiza vitu visivyokuwa na tija. Nadhani DC hakuwa sahihi hata kidogo. Rais anapokuteua kwa ngazi yoyote, amekuamini, kwahiyo unavaa urais nafasi ya Urais kwa sehemu husika. Sasa kama Dr. Samia naye angekuwa anaigiza igiza, sisi wananchi tengemwelewaje?? Watanzania tuwe serious kidogo.
 
Ukiacha kuwa wao ni watumishi wa umma kujikita katika maigizo ya protocal za kiusalama kitu ambacho si sahihi lakini ile display ya risasi za moto mbele ya raia DAMN!!!! ni kitu cha ajabu sana kwa nchi zetu,
Niliwahi kudokezwa kuwa hata maonesho ya sherehe za uhuru na nyinginezo huwa yana vibali maalum,
Lengo lake lilikua ni zuri lakini hapana acha aende tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Nilichogundua nchi masikini hazijiamini kwa lolote[emoji3][emoji3]

Marekani wanaigiza siri nzito za serikali tena ambazo zinaionesha marekani ikifadhili ugaidi au ikipanga shambulio ona series kama Condor,odyses,deep state

Kifupi nchi masikini zinawasiwasi! katika kuigiza wenzetu ndio wanaongeza kufikiri kuboresha, na kuangalia mianya ambayo wao hawakuiona

Mfano mwingine :
budget ya ulinzi
vifaa vya kijeshi nk huwezi pata tz lakini mabeberu wanazo na wanatengeneza video za firepower index.Lakin huku izi taarifa zinAfichwa balaa sasa najiuliza zinafichwa kwa kumlenga nani??
Nchi za nje wanajua hata vya siri? maadui wanazo sisi tunamficha layman au wananchi wasio na hata impact
 
Kuna haja ya kuwapima hawa watu "afya ya akili" kabla ya teuzi kwani ile haikuwa kawaida!
hata vaa yake kuna kitu hakiko sawa kwa yule Binti, I'm so sorry
 
'Umenipa madaraka ya kuleevya....' Ilisikika sauti ya mlevi hiviii.
 
Kama umeshindwa kung’amua hili basi ungekuwa mwanasiasa mbaya kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…