Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Mna bifu tu na mama yenu mkubwa hivyo mnamtafuta uchawi. Hadi mnaanza kutunga habari za kutokewa na mzee. Mwishowe ni kwenda kumkata mapanga. Achaneni na hizo habari karne hii.
 
Kama wewe unadanganywa na shuhuda pole sana, Hizo shuhuda ni upuuzi mtupu.

Usipokuja na ushahidi wa kwamba huo ni udanganyifu hutakua na tofauti na wale wakuu wa makuhani, na Mafarisayo waliojitahidi kuamuru kaburi lilindwe ili Yesu asifufuke lakini siku ya tatu mwanaume akafufuka kama alivyosema

Mathayo 27: 62-66
Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.

Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.

Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo. Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.
 
Things of the spirit!
Huwezi kuelewa kama unafikiria tu mambo ya mwilini!
Walio na Mungu wa kweli kwa kumaanisha wanaelewa hivi vitu vizuri, hata wale wa upande wa pili wa gizani wanaelewa vzr!
Wasioelewa ni wale ambao Kwa Mungu hawapo,kwanza shetani hawapo!
 
Mna bifu tu na mama yenu mkubwa hivyo mnamtafuta uchawi. Hadi mnaanza kutunga habari za kutokewa na mzee. Mwishowe ni kwenda kumkata mapanga. Achaneni na hizo habari karne hii.

Kama hujavurugwa basi wewe ndio kivuruge mwenyewe 🥁🥁🥁
 
Hili ni dili la waganga na wachungaji kama Gwajima kupiga pesa

Unatumiaga kipimo gani kuwajua wapiga pesa. Kumbuka kila binadamu ana udhaifu haijalishi ameitwa katika wito gani na Mungu, hata Musa kama nabii alikua na udhaifu wake na bado Mungu alikataa wanadamu wasimsemee vibaya ila yeye alideal nae

1 Mambo ya Nyakati 16:22 "Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu."
 

Kabisa Christine1

Mambo ya rohoni yanapingwa na roho. Na roho wa Mungu anafanya kazi kupitia mwanadamu roho zipingazo pia zinafanya kazi kupitia mwanadamu

Sasa hapo ndio utajua nani ni wa nani
 
Mwenye anapinga hizo habari zenye proof bila yeye kuja na proof kwamba ni za uongo kama unavyofanya wewe ndio kichaa zaidi
Hizo habari hazina proof, ndiyo maana wanahabari hawahangaiki nazo. Unaamini Gwajima alifufua mtu? Inasemwa "Dunia imejaa wajinga, mtu akitaka kudanganya hawezi kosa wa kuwadanganya."
 
Kwahio waandishi wawape promo hawa watu ?

Uzuri wa uchunguzi hata wewe unaweza kufanya huenda ukawa wa kwanza kupata hii kitu iloyowasumbua watu toka enzi na enzi (how to defy death)

Huenda wengine wanaona hio ni dead avenue na wanatumia muda wao kwa other concerning matters (kama kweli wamefufuka hao watu basi walikuwa hawajafa)
 
Mna bifu tu na mama yenu mkubwa hivyo mnamtafuta uchawi. Hadi mnaanza kutunga habari za kutokewa na mzee. Mwishowe ni kwenda kumkata mapanga. Achaneni na hizo habari karne hii.



Burudika ulale unono😃😃😃
 
Hizo habari hazina proof, ndiyo maana wanahabari hawahangaiki nazo. Unaamini Gwajima alifufua mtu? Inasemwa "Dunia imejaa wajinga, mtu akitaka kudanganya hawezi kosa wa kuwadanganya."

Rudi kwenye video chache juu fanya utafiti urudi hapa kutuambia ulichokutana nacho.
Wachana na habari za Gwajima sisi hapa tunaongelea wafu kurudi uzimani
 


Kama wewe mwandishi na kwako kufanya uchunguzi wa habari na kurudi na majibu kwa jamii ni kuwapa watu promo bado tuna safari ndefu sana kwenye tasnia
 

Dingi anaonekana mida gan??? ya night au mchana kweupe..tujuze mwamba
 
Poole Sana.
 
Kama wewe mwandishi na kwako kufanya uchunguzi wa habari na kurudi na majibu kwa jamii ni kuwapa watu promo bado tuna safari ndefu sana kwenye tasnia
Uchunguzi wa nini Hearsay ?..., Hio itakuwa ni kufanya reporting na sio kuchunguza.., huenda baada ya initial observation wakaona dalili za uongo / kupotosha (sasa badala ya kurudi na jibu la shutuma wanawaachia wengine kuripoti kilichojiri / kilichohadithiwa) ndio wewe umekiona hata kukileta hapa....

Na hizi story hazijaanza leo (kuanzia story za Gamboshi, Misukule n.k.) kwahio hakuna uhaba wa reporting...

Thus my point is..., hizi habari zinapata derserved attention hakuna haja ya kuzi-excalate zaidi ya hapo; tuwekeze nguvu kwenye uchunguzi wa mafisadi, tabia nchi, na kwanini si tu masikini with all these resources....
 
Nimesema kitabu cha Padre Yohannes kinapatikana kwenye bookshops za kanisa.

Utafiti wa Udsm upo mtandaoni, tafuta Dr. Simeon Mesaki, Thesis (PHD).
 
Nadhani hili jambo serikali imelipa verification Badge,maana mtaani na kila mahali tuna jua uchawi upo,misukule ipo,ushirikina upo lakini ajabu ni kwamba serikali inasema "hamna kesi za ushirikina"

eti madai yao hawa amini "uchawi", nadhani ndio mana hata waandishi wa habari na jamii kwa ujumla inapotezea haya mambo kwasababu hata ukisema ufukue,ufukunyue Serikali haipo upande wako,mwisho utashndwa wewe TU.

Siku ninayoamini ukweli wa hizi mambo utawekwa peupe na adhabu kutolewa kama makosa mengine ya jinai yanavyotolewa adhabu ni pale serikali itapo ruhusu na kukubali kuanza shughulika na kesi zote za kishirikina/kimauza uza/kimazingaombwe/kichawi,nk

siku tu serikali inasema Yeyote mwenye ushahidi wa flani n mchawi anatesa watu anaua watu anachukua watu misukule akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria,nadhani ndio Tutajua ukweli na mbivu na Mbichi za hawa wanaokufa na kufufuka,maana watatajana tu huwa wanafanyaje makosa yao wanafanyaje kazi zao.

Polisi wakikamata jambazi,wakitaka aseme silaha alipoficha wanalipiga wanampa adhabu zote wazijuazo hadi anasema,nadhani na hili la ushrikina serikali iingilie kati kila kitu kitakua kweupeee. Serikali tu iamue.

ila hv hv hili jambo ni gumu,linatisha waandishi wa habari hapa tutawaonea tu bure,hili sio sakata kama la fumanizi ni sakata ambalo ukichunguza kama unakaribia kujua ukweli WANAKUMALIZA na ndio hofu ya wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…