JABALI LA KARNE
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 3,093
- 5,850
Kama ni ujanjaujanja thibitisha kibabe uweke heshma
Ushirikina unaujua vizuriiii halafu unajidai kuukataa!? Una lako jambo
Sasa Mwamba, kama hauna tabia ya kufuatilia na kusoma, kama ambavyo waafrika wengi tulivyo, utaendelea kuamini utopolo huo hadi unazeeka. Hata ulaya zamani walikuwa wanaamini uchawi, ila elimu, teknolojia na sayansi zimesaidia kuwapa uhalisia.yawezekana wewe ndo chawi kuu la kufuga misukule ndo maana unakuja na hoja za kupinga ili msikamatwe na tabia zenu chafu za kishetani.
Nakuambia shetani hajawai kumshinda Mungu na haitokaa itokee, wala shetani hawezi kushindana na nguvu za Mungu.
Nakuhakikishia Mungu atawakamata tuu, na ushirikina wenu mtapigwa tuu, na mtakomeshwa hapahapa duniani na bado hukumu ya ahera na ya siku ya mwisho inawangojeni kwa hamu kubwa enyi wachawi wote.
Hata hiyo inayoitwa misukule ni washkaji wamejipaka matope tu na kutembea kama mazombi, wameshachukua hela ya fasta.Hakuna nabii wa kwenye TV aliyewahi kufufua mfu tangu dunia iumbwe.
Wanatoa misukule tu sio wafu.
Hawa wala sadaka hawana uwezo wa kumfufua mtu
Kesi za ushirikina kivipi ?, Tuanze kuwatenga vibibi kizee sababu vina macho mekundu kama zamani ?Nadhani hili jambo serikali imelipa verification Badge,maana mtaani na kila mahali tuna jua uchawi upo,misukule ipo,ushirikina upo lakini ajabu ni kwamba serikali inasema "hamna kesi za ushirikina"
Kiongozi huyo Padre wakati anadai hakuna uchawi alikuwa bado anaamini maandiko yaliyo ndani ya biblia? Maana ndani ya biblia kuna maandiko mengi yanayoonyesha uwepo wa wachawi na uchawi duniani.Duuuh haya, nimetoka kumjibu mama D, uchunguzi wa kina na wa kisayansi ulishafanyikaga mara nyingi, labda nyie mlikuwa bado wadogo.
Mwalimu wangu wa UDSM amepatia PHD yake kupitia utafiti wa mambo kama hayo, aligundua ni upuuzi mtupu, iko hivi, lazima nikiri, kuita ni upuuzi ni kuwa very radical..
Haya mambo yanajumuisha mambo mengi...
Kuna Conspiracy (njama), kuna coincidence(mambo kuangukiana), kuna saikolojia, kuna sayansi, kuna mazingaombwe na mambo mengine mengi yanahusika, kwa amateurs kama nyie(samahani kwa kukuita amateur) ni ngumu sana kuelewa na matokeo yake utaamini uchawi.
Ukiachana na Dr wa UDSM, Padre Yohanes wa shirika la Consolata fathers?, kule Peramiho, alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka ishirini, katika nchi nyingi Afrika kuhusu uchawi, akagundua kwamba haupo, akaandika kitabu kinaitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI BALI SHETANI, kipo kwenye bookshops zote za kanisa katoliki, kakisome upate uelewa kidogo.
Haya maigizo ndiyo anayoamini mleta mada kwamba yanatokea wakati kwa macho na kwa akili ya kawaida ni utapeli mtupu. Na kumtoa huko ni kazi ngumu maana kwa mada yake na mtiririko wa majibu yake kwenye comments za wachangiaji utagundua kwamba hawezi kutoka huko eti hadi afanyiwe tafiti! Pole kwake mleta mada.
I see! Wewe uko makini, umeuliza swali la msingi sana.Kiongozi huyo Padre wakati anadai hakuna uchawi alikuwa bado anaamini maandiko yaliyo ndani ya biblia? Maana ndani ya biblia kuna maandiko mengi yanayoonyesha uwepo wa wachawi na uchawi duniani.
were semarang hivyo badly hujakutana na changamotoHapo kwa Kuhani wala usiangaike na huo ushuhuda unaotolewa maana hakuna kitu hapo. Mjini mipango.
😂😂😂@Wizara ya Afya Tanzania watu wenu mnaothibitishaga wamekufa na jamii ikawazika wanarudi huku wakiwa hai.
Mnaliongeleaje hili? Msije kusema halina ushahidi maana records zao mnazo, wafufuka wapo, wazikaji wapo na makaburi yapo pia.
Una andiko linalosema Mungu mmoja katika nafsi tatu?kuna MUNGU mmoja katika nafsi tatu, unavyosema YESU hilo ni jina la MUNGU kwani wote ni mmoja
mwanadamu amepewa mamlaka hata ya kumuamrisha malaika na chochote kupitia jina YESU KRISTO
Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo. Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina. Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi. Biblia inafundisha kuwa Baba ni Mungu, ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho mtakatifu ni Mungu. Biblia pia inafundisha kuna Mungu mmoja tu. Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu. Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya Biblia.Una andiko linalosema Mungu mmoja katika nafsi tatu?
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Umeandika gazeti refu lakini hakuna linalosema Mungu mmoja katika nafsi tatu.Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo. Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina. Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi. Biblia inafundisha kuwa Baba ni Mungu, ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho mtakatifu ni Mungu. Biblia pia inafundisha kuna Mungu mmoja tu. Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu. Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya Biblia.
Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu. Aya za biblia zifuatazo zitatumika kufafanua neno hili.
1) Kuna Mungu mmoja: kumbukumbu la torati 6:4; wakorintho wa kwanza 8:4; wagalatia 3:20; Timotheo wa kwanza 2:5.
2) utatu una nafsi tatu: mwanzo 1:1; 1:26; 3:22; 11:7 Isaya 6:8; 48:16; 61:1; Mathayo 3:16-17; Mathayo 28:19; wakorintho wa pili 13;14. Katika mwanzo 1:1 neno la wingi “Elohim” linatumika. Katika mwanzo 1:26; 3:22; 11:7 na Isaya 6:8, neno la wingi “sisi” limetumika. Kwa hivyo neno “Elohim’ na “sisi” kumaanisha zaidi ya mmoja halina pingamizi.
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.
3) Nafsi hizi tatu zinatambulika katika maandiko. Katika agano la kale “ BWANA” linatofautishwa na “Bwana” (mwanzo 19:24; Hosea 1:4). “BWANA” ana “Mwana” (zaburi 2:7, 12; Methali 30:2-4). Roho anatofautishwa na “BWANA” (hesabu 27:18) na pia kutoka “Mungu” (zaburi 51:10-12). Mungu mwana atofautishwa na Mungu Baba (zaburi 45:6-7; waebrania1:8-9). Katika agano jipya, Yohana 14:16-17 ndipo Yesu anazungumza na Baba juu ya kuleta Msaidizi, Roho mtakatifu. Hii ina maana ya kuwa Yesu hakujichukulia yeye mwenyewe kuwa Baba wala Roho Mtakatifu. Katika kila mahali ndani ya agano jipya Yesu alipozungumza na Mungu Baba alikuwa akizungumza na nafsi moja wapo ya Utatu – Baba.
4) kila nafsi katika utatu huu ni Mungu: Baba ni Mungu: Yohana 6:27; warumi 1:7; petro wa kwanza 1:2. Mwana ni Mungu: Yohana 1:1, 14; warumi 9:5; wakolosai 2:9; waebrania 1:8; Yohana wa kwanza 5:20. Roho mtakatifu ni Mungu: Matendo ya mitume 5:3-4; wakorintho wa kwanza 3:16 (anayedumu ndani ni Roho mtakatifu –warumi 8:9; Yohana 14:16 –17; Matendo ya mitume 2:1—4).
5) Katika mpangilio ndani ya utatu huu: maandiko yanaonyesha kuwa Roho Mtakatifu humtumikia Baba na Mwana na Mwana humtumikia Baba. Huu ni uhusiano wa ushirika wao wala hupunguzi uungu wa nafsi yoyote ile. Kuhusu Mwana tazama: luka 22:42; Yohana 5:36; Yohana 20:21; Yohana wa kwanza 4:14. kuhusu Roho Mtakatifu tazama Yohana 14:16; 14:26; 15:26; 16:7 na hasa Yohana 16:13-14.
6) Majukumu ya kila nafsi katika utatu: Baba ndiye aliyesababisha kuwako kwa 1) ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Ufunuo wa Yohana 4:11), 2) ufunuo wa kimungu (Ufunuo wa Yohana 1:1) 3)wokovu (Yohana 3:16-17); Matendo ya kibinadamu ya Yesu ( Yohana 5:17; 14:10). Baba anaonekana kwanza katika haya yote.
Mwana ni wakala ambaye Baba humtumia kufanyia haya: 1) Kuumba na kustawisha ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Yohana 1:3; wakolosai 1:16-17); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 1:1; Mathayo 11:27; Yohana 16:12-15; Ufunuo wa Yohana 1:1); na 3) wokovu ( wakorintho wa pili 5:19; Mathayo 1:21; Yohana 4:42). Baba alifanya mambo haya yote kupitia Mwana anayetenda kazi kama mwakilishi wake.
Roho Mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kufanya haya: 1) uumbaji na ustawishaji wa ulimwengu (mwanzo 1:2; Ayubu 26:13; zaburi 104: 30); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21); 3) wokovu (Yohana 3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1;2); na 4) matendo ya Yesu ( Isaya 61:1; Matendo ya mitume 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.
Baba, Mwana na Roho si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu. Mungu asiyeonekana na macho hawezi kuelezwa kwa usahihi na mwenye kuona na macho ya kibinadamu akaeleweka. Lakini katika hali zote tazama Mungu kama nafsi tatu zisizogawanyika kuwa Miungu mitatu bali Mungu mmoja tu. “jinsi zilivyo kuu utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana?” 9 warumi 11:33-34)
😂😂😂
Nadhani watu hao ndo waliongelewa kwenye andiko hili:
Isaya 42:22
Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha..
Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo. Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina. Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi. Biblia inafundisha kuwa Baba ni Mungu, ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho mtakatifu ni Mungu. Biblia pia inafundisha kuna Mungu mmoja tu. Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu. Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya Biblia.
Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu.
Roho Mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kufanya haya: 1) uumbaji na ustawishaji wa ulimwengu (mwanzo 1:2; Ayubu 26:13; zaburi 104: 30); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21); 3) wokovu (Yohana 3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1;2); na 4) matendo ya Yesu ( Isaya 61:1; Matendo ya mitume 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.
Baba, Mwana na Roho si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu. Mungu asiyeonekana na macho hawezi kuelezwa kwa usahihi na mwenye kuona na macho ya kibinadamu akaeleweka. Lakini katika hali zote tazama Mungu kama nafsi tatu zisizogawanyika kuwa Miungu mitatu bali Mungu mmoja tu. “jinsi zilivyo kuu utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana?” 9 warumi 11:33-34)
Umeandika gazeti refu lakini hakuna linalosema Mungu mmoja katika nafsi tatu.
Andiko linasema
1wakorintho 8:6
Lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba
Anaapa kwa nafsi yake, haapi kwa nafsi zake.
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Mimi naona wewe umenielewa japo tu uandishi tunatofautiana ya kuwa MUNGU jina lake YesuUtatu mtakatifu ni Mungu mmoja katika nafasi zake tatu
1.Baba/Muumba. Huyu ni Mungu katika nafasi yake ya uumbaji
2.Mwana ni Mungu katika nafasi ya ukombozi (Yesu ni jina lake Mungu alilopewa Kristo)
3.Roho mtakatifu ni Mungu ndani yetu. Huulinda mwili, roho na nafsi, huutunza mwili kupitia roho na nafsi kwa hufanya mawasliano na roho hata wakati wa usiku na hata kuushuhudia mwili unapokua umelala
Mimi naona wewe umenielewa japo tu uandishi tunatofautiana ya kuwa MUNGU jina lake Yesu