Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

NI wapumbavu pekee wanaamini kwamba Mungu huenda hakuwa sahihi aliposema kufa NI UHAKIKA.....hamnaga hizo ndugu zangu mwili ukifa unakufa labda roho ndo inaweza kuhuishwa.

Ovaaaa

Kufa ni uhakika na ni amri ya Mungu na kufufuka kupo kwa waaminio, hata lazaro alifufuka. Swala linakuja kwenye proof ya ufufuko
 
Habari za watu kufa na kuzikwa na baadae kupatikana wakiwa hai ni za kushangaza mnooo.

Yaani mtu amekufa kwa kuugua au ajali au ghafla tuu, hospitalini wanahakikisha amekufa na wanatoa cheti cha kifo na mwili mnakadhiwa, mnaenda kuzika na viongozi wa serikali za mtaa, viongozi wa dini na familia wanashiriki na kusema Mungu amempenda zaidi.

Imagine wafiwa wanaomboleza na kusahau kisha baada ya muda marehemu anapatikana yupo hai katika hali tata. Hili jambo ni la kutisha na kushangaza sana na ni jambo linalodhihirisha uwepo watu wengi wanaodhaniwa wamekufa lakini inawezekana kabisa wapo kama walivyopatikana hawa.

Waandishi wa habari nadhani huu ni muda muafaka wa kulifanyia hili jambo habari za uchunguzi wa kina. Uchunguzi ambao utasaidia kujua haswa ni nini kinatokea hadi binadamu anaonekana amekufa, tena kitabibu kabisa mahospitalini, anazikwa na kisha anapatika akiwa hai.

Hizi habari zinagusa uhai wa mwanadamu lakini bahati mbaya hazipewi airtime kivileee na medias rasmi wala zile za udaku wala hazifanyiwi uchunguzi utakaoisaidia jamii mbeleni. Badala yake habari Zinazokik ni zile za Connections (ngono) na hapa ndio utagundua nguvu gani imeshikilia mitandao ya kijamii

Mungu atusaidie kumtafuta yeye na nguvu zake

Waandishi wa Habari hawazi kufanya uchunguzi kwa Matapeli wa dini,
Ulishawahi kusikia wapi waisilamu wamefufua wafu ?
 
Huu ni upuuzi mtupu... na ndiyo maana unapuuzwa.
Kama ni upuuzi mtupu Hawa waliorudi kutoa hizi shuhuda na wenyewe ni wapuuzi? Ufike wakati watu wakubali kuwa haya mambo yapo yafanyiwe uchunguzi unaostahili na hatua zinazofaa zichukuliwe kusema ni rahisi kabla hayajakukuta.
 
Tatizo Tanzania hatuna waandishi wa habari. Tunawaandishi wa magazeti na wasaka fedha you tube. Taaluma za chini, ubunifu hakuna ni full stereotyped. Siku akija Kikeke, au mwandishi kutoka BBC kuyafuatilia matukio haya, utaona vile watakavyoanza kuyakimbilia kama nyumbu. Inakarahisha.

Surely. Yaani wandishi wetu wamepoteza weledi wala hawabadiliki kama nyakati zinavyobadilika.
Vile sasahivi kila mtu ana kismartphone ana uwezo wa kushare taarifa, waandishi wa habari walipaswa wao wajikite kwenye uchunguzi wa kina waongeze thamani kwenye habari zao ili waendelee kuwa na thamani kwenye tasnia yao. Lakini sasa dah
 
Ujinga hautakaa uishe Africa
Huu ni upuuzi mtupu... na ndiyo maana unapuuzwa.
Hii inaonyesha ufupi wa kiwango chenu cha kutumia akili ama ninyi ni wanufaika katika huo mchakato wa kupoteza watu kwa kivuli cha kifo.

Mtu mwenye akili zake, anaona matukio yakiwa dhahiri, mchana kweupe watu wanaonyeshwa walizikwa na baadaye wanatokea wakiwa hai, halafu kijing akijinga tu aseme, 'huu ni ujinga ama upuuzi". Kama mama yako ama ndugu yako angekufa, halafu baadaye umwone akiwa hai katika hali tata ungesema ujinga na upuuzi?

Ninaona pia kukosa elimu kwenu kunachangia uchangiaji wenu wa kijinga. Mtu mwerevu, kabla hajasema haya mliyoyasema, angependekeza uchunguzi wa kina wa kijamii, na kisayansi ufanyike ili kutafuta kilicho nyuma ya pazia la matukio haya badala ya kusema tu "ujinga na upuuzi" huku mambo yakiendelea.

Kama hujui kitu si lazima useme. Ukinyamaza ni hekima zaidi ya huku kuropoka kwenu.
 
Waganga wa kienyeji kuna dawa wanampa mgonjwa inayoweza ku-‘simulate’ death; then wakati mnaenda kumzika yeye anawahi chap na kumfukua kisha anampa dawa ya kumzindua usingizini na kisha anampa dawa ya kumfanya awe nusu zezeta, baada ya hapo anamkata ulimi ili asije kusema endapo akitoroka, then anaenda kutumikishwa. Huku anawaachia mgomba au ugogo likae.Huu uchunguzi niliuona kwenye national Geographic.
 
haya mambo yapo chamsingi ni kulishika jina takatifu la mungu na kutenda mema AMIN
Hivi unamjua Mungu Baba wa Bwana Yesu Kristo na Uweza wake?
Jina takatifu ni lipi na unalishikaje? Matendo mema ni yapi? Kuacha wachawi watamalaki kupoteza watu na wewe kukaa kimya wakati Bwana amekupa Mamlaka ya kuwatikita? Please fafanua.
 
Waandishi wa Habari hawazi kufanya uchunguzi kwa Matapeli wa dini,
Ulishawahi kusikia wapi waisilamu wamefufua wafu ?

Kwani Misingi ya uislam ikoje kwenye hilo?

Misingi ya ukristo inasema yapo maandiko kama hili la kitabu cha mathayo

Mathayo 10:8 "Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure."
 
Kama ni upuuzi mtupu Hawa waliorudi kutoa hizi shuhuda na wenyewe ni wapuuzi? Ufike wakati watu wakubali kuwa haya mambo yapo yafanyiwe uchunguzi unaostahili na hatua zinazofaa zichukuliwe kusema ni rahisi kabla hayajakukuta.

Ni kweli Mama Pasco
Kuuita huu upuuzi bila kuja na proof kwamba ni upuuzi, nao ni upuuzi mwingine tena mkubwa zaidi
Na sijui kwanini watu wanashindwa kulifanyia kazi wakati hao wafu wapo kati yetu kwenye jamii zetu
Au Wanataka hadi wazungu waje kufuatilia ndio waamke
 
Waganga wa kienyeji kuna dawa wanampa mgonjwa inayoweza ku-‘simulate’ death; then wakati mnaenda kumzika yeye anawahi chap na kumfukua kisha anampa dawa ya kumzindua usingizini na kisha anampa dawa ya kumfanya awe nusu zezeta, baada ya hapo anamkata ulimi ili asije kusema endapo akitoroka, then anaenda kutumikishwa. Huku anawaachia mgomba au ugogo likae.Huu uchunguzi niliuona kwenye national Geographic.

Na wanaopinga bila proof wanaweza kuhusika na hao wanafanya wengine wazike mgomba au wakawa ma agents wao kwa kujijua au bila bila hata kujijua

Ni bora Waje na proof tuujue ukweli waouamini wao tupone
 
Hivi unamjua Mungu Baba wa Bwana Yesu Kristo na Uweza wake?
Jina takatifu ni lipi na unalishikaje? Matendo mema ni yapi? Kuacha wachawi watamalaki kupoteza watu na wewe kukaa kimya wakati Bwana amekupa Mamlaka ya kuwatikita? Please fafanua.
kuna MUNGU mmoja katika nafsi tatu, unavyosema YESU hilo ni jina la MUNGU kwani wote ni mmoja
mwanadamu amepewa mamlaka hata ya kumuamrisha malaika na chochote kupitia jina YESU KRISTO
 
Hawa watu mimi binafsi nachoka naudhika nasumbuka natingwa kwa utapeli huu
Mbona huwa ni watu wa maisha duni tu kwani wenye pesa hawafi?
Mochwari zhospitali zipo mbona hawaendi huko kuponya watu
Hi kuwafungulia mashtaka iwe fundisho kwa wengine

Umefuatilia nini kilitokea hadi hao wafu wakafufuka Pakawa?
Mimi kabla ya kuandika hapa nimefuatilia, sijaona popote ambapo walipangiwa kufufuka ila nilichoona ni imani ya kuomwomba Mungu aliyetenda maajabu atendende tena.

Tulifuatilie hili sababu liko ndani ya jamii yetu na linakua kwa kasi ili tuweze kulisema kwa usahihi zaidi na kwa manufaa
 
Uzi fikirishi sana huu

Ngoja tufuatilie zaidi. Mimi nitafanya hivyo pia tujue ilianzaje hadi kufa na ufufuko
Kwa wale tunaotaka kuujua ukweli tutaupata tuu maana wafu ni watanzania
 
Inawezekana akili zetu zilishageuzwa au kutekwa, na hao wanaofanya hayo mambo ili tusipate muda wa kujadili maovu yao. Ndio maana wengi tunapuuzia
 
Habari za watu kufa na kuzikwa na baadae kupatikana wakiwa hai ni za kushangaza mnooo.

Yaani mtu amekufa kwa kuugua au ajali au ghafla tuu, hospitalini wanahakikisha amekufa na wanatoa cheti cha kifo na mwili mnakadhiwa, mnaenda kuzika na viongozi wa serikali za mtaa, viongozi wa dini na familia wanashiriki na kusema Mungu amempenda zaidi.

Imagine wafiwa wanaomboleza na kusahau kisha baada ya muda marehemu anapatikana yupo hai katika hali tata. Hili jambo ni la kutisha na kushangaza sana na ni jambo linalodhihirisha uwepo watu wengi wanaodhaniwa wamekufa lakini inawezekana kabisa wapo kama walivyopatikana hawa.

Waandishi wa habari nadhani huu ni muda muafaka wa kulifanyia hili jambo habari za uchunguzi wa kina. Uchunguzi ambao utasaidia kujua haswa ni nini kinatokea hadi binadamu anaonekana amekufa, tena kitabibu kabisa mahospitalini, anazikwa na kisha anapatika akiwa hai.

Hizi habari zinagusa uhai wa mwanadamu lakini bahati mbaya hazipewi airtime kivileee na medias rasmi wala zile za udaku wala hazifanyiwi uchunguzi utakaoisaidia jamii mbeleni. Badala yake habari Zinazokik ni zile za Connections (ngono) na hapa ndio utagundua nguvu gani imeshikilia mitandao ya kijamii

Mungu atusaidie kumtafuta yeye na nguvu zake

Mungu atunusuru
 
Back
Top Bottom