Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Nitaanza kuziamini hizi habari nikisikia mtu maarufu, ambaye kila mtu anajua alishafariki amefufuka, kama Nyerere, Sokoine, Kanumba, Magufuli, Ruge, Mkapa etc

Kama anayefanya haya ni Mungu ukumbuke yeye huwa haangalii umaarufu wala hapangiwi, tena hajaribiwi kabisa.

1 Sam 2:8 "Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake."
 
Waganga wa kienyeji kuna dawa wanampa mgonjwa inayoweza ku-‘simulate’ death; then wakati mnaenda kumzika yeye anawahi chap na kumfukua kisha anampa dawa ya kumzindua usingizini na kisha anampa dawa ya kumfanya awe nusu zezeta, baada ya hapo anamkata ulimi ili asije kusema endapo akitoroka, then anaenda kutumikishwa. Huku anawaachia mgomba au ugogo likae.Huu uchunguzi niliuona kwenye national Geographic.
Finally some meaningful explanation!!... Naitaka hiyo documentary

Mwisho wa siku hata wanayoenda kufanya hayana maana...mara kulima!!!

Mzungu anaunda mashine zilime maelf ya hekari, sisi tunahangaika na maiti zitulimie, sasa huo msukule unalima hekari ngapi 😂
 
Wizara ya Afya Tanzania watu wenu mnaothibitishaga wamekufa na jamii ikawazika wanarudi huku wakiwa hai.

Mnaliongeleaje hili? Msije kusema halina ushahidi maana records zao mnazo, wafufuka wapo, wazikaji wapo na makaburi yapo pia.

Tuambieni hili limekaaje?

Mimi naamini kipo cha kufanya kabla ya kufika huko kwa kufa na kufufuka. Kuondoka kwa mtu kwenye familia ni pigo kubwa kijamii hata kiuchumi kwa familia hiyo maana anaweza kufa aliye tegemeo la familia au akafa baada ya kuigharimu sana familia.

Kwa maana nyingine kama kifo ni cha uongo (kiinimacho) basi hata magonjwa au vyanzo vya hivyo vifo ni vya uongo au viini macho

Tukiweza kutegua hili haitakua ahueni kwa familia tuu, hata wizara ya afya itapata ahueni kwa kupunguza budget yake kwenye kudeal na magonjwa na vifo fake
viini macho.. mazingaombwe.
 
Ili huu uwe upuuzi na upuuzwe lazima watokee werevu na kufuatilia kisha waje na proof kwamba huo ni upuuzi
Vinginevyo tukisema ni upuuzi tuu bila kuchukua hatua tunaonekana wapuuzi zaidi ya hao tunaowaita wapuuzi
May be you are not informed, Labda hauna taarifa.

Hivi visa havijaanza leo, vipo tangu zamani, watu walishafuatilia na wengine kufanyia utafiti kwa muda mrefu. Waligundua kuwa ni upuuzi mtupu.
 
Hebu tuletee proof ya ufuatiliaji na data kamili
 
Hii inaonyesha ufupi wa kiwango chenu cha kutumia akili ama ninyi ni wanufaika katika huo mchakato wa kupoteza watu kwa kivuli cha kifo.

Mtu mwenye akili zake, anaona matukio yakiwa dhahiri, mchana kweupe watu wanaonyeshwa walizikwa na baadaye wanatokea wakiwa hai, halafu kijing akijinga tu aseme, 'huu ni ujinga ama upuuzi". Kama mama yako ama ndugu yako angekufa, halafu baadaye umwone akiwa hai katika hali tata ungesema ujinga na upuuzi?

Ninaona pia kukosa elimu kwenu kunachangia uchangiaji wenu wa kijinga. Mtu mwerevu, kabla hajasema haya mliyoyasema, angependekeza uchunguzi wa kina wa kijamii, na kisayansi ufanyike ili kutafuta kilicho nyuma ya pazia la matukio haya badala ya kusema tu "ujinga na upuuzi" huku mambo yakiendelea.

Kama hujui kitu si lazima useme. Ukinyamaza ni hekima zaidi ya huku kuropoka kwenu.
Duuuh haya, nimetoka kumjibu mama D, uchunguzi wa kina na wa kisayansi ulishafanyikaga mara nyingi, labda nyie mlikuwa bado wadogo.

Mwalimu wangu wa UDSM amepatia PHD yake kupitia utafiti wa mambo kama hayo, aligundua ni upuuzi mtupu, iko hivi, lazima nikiri, kuita ni upuuzi ni kuwa very radical..

Haya mambo yanajumuisha mambo mengi...
Kuna Conspiracy (njama), kuna coincidence(mambo kuangukiana), kuna saikolojia, kuna sayansi, kuna mazingaombwe na mambo mengine mengi yanahusika, kwa amateurs kama nyie(samahani kwa kukuita amateur) ni ngumu sana kuelewa na matokeo yake utaamini uchawi.

Ukiachana na Dr wa UDSM, Padre Yohanes wa shirika la Consolata fathers?, kule Peramiho, alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka ishirini, katika nchi nyingi Afrika kuhusu uchawi, akagundua kwamba haupo, akaandika kitabu kinaitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI BALI SHETANI, kipo kwenye bookshops zote za kanisa katoliki, kakisome upate uelewa kidogo.
 
Majibu yanapatikana kanisani, misikitini na kwa waganga. Nchi hatuwezi tumia nguvu kubwa kuwekeza kwenye tafiti za ujanja janja, mazingaumbwe na ushirikina.
 
Haya mambo kama hujawahi shuhudia unaweza sema pengine ni uongo!
Lakini kuna jamaa hatukujuwa chochote kuhusu alikotokea wala historia yake,lkn tulifahamiana nae kama miaka 3 hivi!
Basi kuna siku wakafika ndugu zake kutoka Lusaka na kuanza kuangua kilio na kisha kumchukua na kuondoka nae kurudi Lusaka!
Kumbe yule jamaa alikuwa amefariki miaka 3 nyuma na ndugu zake walikuwa wanapewa taarifa kwamba ndugu yao japo amekufa lakini yupo huko Nakonde?
 
Muache tu. Akikua ataacha.
 
Huu ni upuuzi mtupu... na ndiyo maana unapuuzwa.
yawezekana wewe ndo chawi kuu la kufuga misukule ndo maana unakuja na hoja za kupinga ili msikamatwe na tabia zenu chafu za kishetani.

Nakuambia shetani hajawai kumshinda Mungu na haitokaa itokee, wala shetani hawezi kushindana na nguvu za Mungu.

Nakuhakikishia Mungu atawakamata tuu, na ushirikina wenu mtapigwa tuu, na mtakomeshwa hapahapa duniani na bado hukumu ya ahera na ya siku ya mwisho inawangojeni kwa hamu kubwa enyi wachawi wote.
 
Duuuh haya, nimetoka kumjibu mama D, uchunguzi wa kina na wa kisayansi ulishafanyikaga mara nyingi, labda nyie mlikuwa bado wadogo.

Mwalimu wangu wa UDSM amepatia PHD yake kupitia utafiti wa mambo kama hayo, aligundua ni upuuzi mtupu, iko hivi, lazima nikiri, kuita ni upuuzi ni kuwa very radical..

Haya mambo yanajumuisha mambo mengi...
Kuna Conspiracy (njama), kuna coincidence(mambo kuangukiana), kuna saikolojia, kuna sayansi, kuna mazingaombwe na mambo mengine mengi yanahusika, kwa amateurs kama nyie(samahani kwa kukuita amateur) ni ngumu sana kuelewa na matokeo yake utaamini uchawi.

Ukiachana na Dr wa UDSM, Padre Yohanes wa shirika la Consolata fathers?, kule Peramiho, alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka ishirini, katika nchi nyingi Afrika kuhusu uchawi, akagundua kwamba haupo, akaandika kitabu kinaitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI BALI SHETANI, kipo kwenye bookshops zote za kanisa katoliki, kakisome upate uelewa kidogo.

Kwanza kabisa naomba tuwekee hapa hilo andiko tuone uchunguzi ulifanyikaje hadi kufikia hapo unapotuelezea. Ukiongea maneno matupu mimi nitakuweka kwenye kundi la 1.Wazushi 2. Tapeli 3. Mmoja wa hao wanafanya mazingaombwe ya kuua watu

Na ukumbuke pia haikatazwi majibu ya uchunguzi kupingwa na uchunguzi mwingine
 
Wewe Unatuletea Clip za Ma actors Wa Hizi 'dini' Zetu...!
Mbona Hawaendi Mochware Kufufua Wafu!!...Wamekazana Majukwaani Kuwarubuni Watu...Next time Usianzishe nyuzi Za Mizaha..!

Kwani hao waliofufuka kuna aliyeenda makaburini kuwafufua!?
Umeona wapi yule police au mchungaji akisema walikusudia kuwafufua hao?

Kuonekana kwa hao watu ni matokeo ya nguvu ipatayo ile nguvu iliyowapoteza, ambapo nguvu hiyo inajengwa na imani na dua za watu bila hata kutarget nini kitokee au nani afufuke. Baada ya ufufuo na nguvu kudhihirika ndio yanatokea mengi zaidi

Tafuta ukweli wa hayo mambo kwa kupita sehemu zinazostahili kabla ya kupinga
 
Haya mambo kama hujawahi shuhudia unaweza sema pengine ni uongo!
Lakini kuna jamaa hatukujuwa chochote kuhusu alikotokea wala historia yake,lkn tulifahamiana nae kama miaka 3 hivi!
Basi kuna siku wakafika ndugu zake kutoka Lusaka na kuanza kuangua kilio na kisha kumchukua na kuondoka nae kurudi Lusaka!
Kumbe yule jamaa alikuwa amefariki miaka 3 nyuma na ndugu zake walikuwa wanapewa taarifa kwamba ndugu yao japo amekufa lakini yupo huko Nakonde?

Kipo cha kujifunza hapa
 
Majibu yanapatikana kanisani, misikitini na kwa waganga. Nchi hatuwezi tumia nguvu kubwa kuwekeza kwenye tafiti za ujanja janja, mazingaumbwe na ushirikina.

Kama ni ujanjaujanja thibitisha kibabe uweke heshma
Ushirikina unaujua vizuriiii halafu unajidai kuukataa!? Una lako jambo
 
Back
Top Bottom