Duuuh haya, nimetoka kumjibu
mama D, uchunguzi wa kina na wa kisayansi ulishafanyikaga mara nyingi, labda nyie mlikuwa bado wadogo.
Mwalimu wangu wa UDSM amepatia PHD yake kupitia utafiti wa mambo kama hayo, aligundua ni upuuzi mtupu, iko hivi, lazima nikiri, kuita ni upuuzi ni kuwa very radical..
Haya mambo yanajumuisha mambo mengi...
Kuna Conspiracy (njama), kuna coincidence(mambo kuangukiana), kuna saikolojia, kuna sayansi, kuna mazingaombwe na mambo mengine mengi yanahusika, kwa amateurs kama nyie(samahani kwa kukuita amateur) ni ngumu sana kuelewa na matokeo yake utaamini uchawi.
Ukiachana na Dr wa UDSM, Padre Yohanes wa shirika la Consolata fathers?, kule Peramiho, alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka ishirini, katika nchi nyingi Afrika kuhusu uchawi, akagundua kwamba haupo, akaandika kitabu kinaitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI BALI SHETANI, kipo kwenye bookshops zote za kanisa katoliki, kakisome upate uelewa kidogo.