Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

YESU ni MUNGU

Yohana 5:43
"Mimi nimekuja kwa Jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo."

Waraka wa kwanza wa Yohana 5:7
"Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu: nao hawa watatu ni mmoja."

Yohana 14:8-9
"Filipo akajibu akamwambia, Utuonyeshe Baba, yatutosha.
Yesu akajibu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?"

Yohana 10:30
"Mimi na Baba tu mmoja."


Jina YESU lilishushwa toka mbinguni na malaika
Luka 1:26-31
"Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.
Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu."
Nimefurahi kuona hii 🤝
 
Utatu mtakatifu ni Mungu mmoja katika nafasi zake tatu
1.Baba/Muumba. Huyu ni Mungu katika nafasi yake ya uumbaji
2.Mwana ni Mungu katika nafasi ya ukombozi (Yesu ni jina lake Mungu alilopewa Kristo)
3.Roho mtakatifu ni Mungu ndani yetu. Huulinda mwili, roho na nafsi, huutunza mwili kupitia roho na nafsi kwa hufanya mawasliano na roho hata wakati wa usiku na hata kuushuhudia mwili unapokua umelala
Yesu ni nabii na Yehova ndio mungu.
 
Mtazamo wangu, kwanza kwa Haraka na uhakika vifo vya aina hii vinahusishwa na ushirikina moja kwa moja, nikimaanisha kwa watu hawa wanaoeleza kufa, kuzikwa na hatimaye kufufuka,,,,,tukumbuke uchawi ni dhana inayoishi, hivyo ukifuatilia kwa makini kutoka kwa Huyo mtoto wa geita na mwingine wa Kigoma utaona ni dhahiri shahiri kuwa ushirikina ulihusika kwa Karibu 100%.
Hivyo basi mama D ili serikali kupita WA ifanye kama unavyodai lazima ikubali na kukiri kuwa Ushirikina upo, na unasababisha vifo vya aina hiyo, kisha ije na mbinu mbadala jinsi gani ya kunusuru watu ambao aidha watakufa kwa kudhani ushirikina umehusika, na anayehusishwa na ushirikina huo pia achukuliwe hatua madhubuti kwa mlengo wa sheria za ushirikina ambazo pia zitakuwepo na serikali kupitia WKS itatunga sheria hizo za uchawi na ushirikina kisha ikibidi kuajiri watumishi wenye taaluma hiyo katika ngazi zote.

Kwa kufanya hivyo hoja yako ya kuwabeza wanahabari kuwa hawafuatilii matukio ya aina hiyo ndipo itakuwa na mashiko.

Kwa mfano fikiria, Serikali haitambui uchawi au ushirikina, na hakuna sheria yoyote inayotambua habqri hiyo, halafu Kuna mtu anasimama na kusema yeye alikufa, akazikwa na kisha akafufuka, ambapo kifo chake kilisababishwa na ushirikina huku akionesha ushahidi na vielelzo vyote juu ya tukio hilo na pengine hata muhusika wa tukio Hilo anajulikana, Je nani kwa mlengo wa kisheria(vyombo vya dola) atazungumzia na kuthibitisha taarifa hiyo?

Kwa maana hiyo hiyo nadhani ni busara serikali itambue kuwa uchawi upo, kisha itunge sheria juu ya uchawi, iunde wizara ya kushughulika na uchawi na iajiri watu waliobobea juu ya uchawi na ikibidi iwe na mahakama ya wachawi.

Tofauti na hapo wanahanari tutawalaumu bure kwa wao wanamisingi yao ambayo inawaruhusu kubalance taarifa kwa pande zote!
 
Yesu mtoto wa mariam alikuwa binadamu..hajawahi kuwa Mungu na hakuna sehemu kwenye Biblia pameandikwa Yesu ni Mungu..

Aliyezaliwa katika mwili ni Kristo na huyo ndio mtoto wa Mariam
Mathayo 2: 3-4
"Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, KRISTO azaliwa wapi?


Luka 1:31
"Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU."


YESU NI MUNGU
Yohana 14:8-9
"Filipo akajibu akamwambia, Utuonyeshe Baba, yatutosha.
Yesu akajibu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?"

Yohana 10:30
"Mimi na Baba tu mmoja."


Mungu ni mmoja katika nafasi zake tatu
1.Baba/Muumba. Huyu ni Mungu katika nafasi yake ya uumbaji
2.Mwana ni Mungu katika nafasi ya ukombozi (Yesu ni jina lake Mungu alilopewa Kristo)
3.Roho mtakatifu ni Mungu ndani yetu. Huulinda mwili, roho na nafsi, huutunza mwili kupitia roho na nafsi kwa hufanya mawasliano na roho hata wakati wa usiku na hata kuushuhudia mwili unapokua umelala
 
Ninapaa kwenda kwa baba yangu, nae ni baba yenu, kwa mungu wangu ambae ni mungu wenu Yohana 20:17

mama D Kwetu sisi Mungu ni mmoja tu Wakorintho 8:6.
Hata yesu anasema hapa kwamba Baba ni mkuu kuliko yeye Yohana 14:28.

Kuna Mungu mmoja tu ambae ni Yehova.
 
Ninapaa kwenda kwa baba yangu, nae ni baba yenu, kwa mungu wangu ambae ni mungu wenu Yohana 20:17

mama D Kwetu sisi Mungu ni mmoja tu Wakorintho 8:6.
Hata yesu anasema hapa kwamba Baba ni mkuu kuliko yeye Yohana 14:28.

Kuna Mungu mmoja tu ambae ni Yehova.

Mungu ni mmoja kweli kabisa. Naye baada ya kutuumba amendelea kuishi nasi katika roho (roho mtakatifu) na katika mwili (kupitia mwili wa Kristo)
 
Uko sahihi
Uchunguzi wa nini Hearsay ?..., Hio itakuwa ni kufanya reporting na sio kuchunguza.., huenda baada ya initial observation wakaona dalili za uongo / kupotosha (sasa badala ya kurudi na jibu la shutuma wanawaachia wengine kuripoti kilichojiri / kilichohadithiwa) ndio wewe umekiona hata kukileta hapa....

Na hizi story hazijaanza leo (kuanzia story za Gamboshi, Misukule n.k.) kwahio hakuna uhaba wa reporting...

Thus my point is..., hizi habari zinapata derserved attention hakuna haja ya kuzi-excalate zaidi ya hapo; tuwekeze nguvu kwenye uchunguzi wa mafisadi, tabia nchi, na kwanini si tu masikini with all these resources....
 
Mleta mada hayuko sawa upstairs
Haya maigizo ndiyo anayoamini mleta mada kwamba yanatokea wakati kwa macho na kwa akili ya kawaida ni utapeli mtupu. Na kumtoa huko ni kazi ngumu maana kwa mada yake na mtiririko wa majibu yake kwenye comments za wachangiaji utagundua kwamba hawezi kutoka huko eti hadi afanyiwe tafiti! Pole kwake mleta mada.
 
Tatizo Tanzania hatuna waandishi wa habari. Tunawaandishi wa magazeti na wasaka fedha you tube. Taaluma za chini, ubunifu hakuna ni full stereotyped. Siku akija Kikeke, au mwandishi kutoka BBC kuyafuatilia matukio haya, utaona vile watakavyoanza kuyakimbilia kama nyumbu. Inakarahisha.
Shida ni kwamba ukisema upekenyue hizi habari kwa undani malamka zitakuandama kwamba unapromote ulozi..
 
Haya ni mambo ya kiroho. Kuna vifo vya aina mbili cha Matakwa ya Muumba na cha Matakwa ya wachawi. Matakwa ya wachawi ipo namna mtu anarudishwa.
 
Sijafungua hizo links ila nahisi tu ni za nabii uchwara wa pale Kimara ambaye mkewe mama D ni chawa wake, kabla sijaendelea…. hisia zangu ziko sahihi?
 
May be you are not informed, Labda hauna taarifa.

Hivi visa havijaanza leo, vipo tangu zamani, watu walishafuatilia na wengine kufanyia utafiti kwa muda mrefu. Waligundua kuwa ni upuuzi mtupu.
BILA SHAKA WEWE NI MCHAWI.
 
Duuuh haya, nimetoka kumjibu mama D, uchunguzi wa kina na wa kisayansi ulishafanyikaga mara nyingi, labda nyie mlikuwa bado wadogo.

Mwalimu wangu wa UDSM amepatia PHD yake kupitia utafiti wa mambo kama hayo, aligundua ni upuuzi mtupu, iko hivi, lazima nikiri, kuita ni upuuzi ni kuwa very radical..

Haya mambo yanajumuisha mambo mengi...
Kuna Conspiracy (njama), kuna coincidence(mambo kuangukiana), kuna saikolojia, kuna sayansi, kuna mazingaombwe na mambo mengine mengi yanahusika, kwa amateurs kama nyie(samahani kwa kukuita amateur) ni ngumu sana kuelewa na matokeo yake utaamini uchawi.

Ukiachana na Dr wa UDSM, Padre Yohanes wa shirika la Consolata fathers?, kule Peramiho, alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka ishirini, katika nchi nyingi Afrika kuhusu uchawi, akagundua kwamba haupo, akaandika kitabu kinaitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI BALI SHETANI, kipo kwenye bookshops zote za kanisa katoliki, kakisome upate uelewa kidogo.
WEWE NI MCHAWI MBAYA SANA.

KILA MTU AKUEPUKE.
 
Back
Top Bottom