Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Mkuu tindo akitaka kuhania CDM, asome katiba ya chama asome Sera za chama akubaliane nazo, pia afundishwe itikadi ya chama kwanza alafu ndo akubaliwe kujiunga na chama,

Kuhusu kugombea uongozi wowote, hiyo ni mpaka awe mwanachama kwa miaka 2

Akipewa hayo mashariti akiyakubali apokelewe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu tena mtazamo wa nje, Nyalandu amefanikiwa kukigeuza chama kwa muda mfupi sana. Chadema ya leo sio ile ya kutoa matamko kwa kila jambo. Hata lugha za baadhi viongozi tena wale fire brand zinaanza kubadilika.

Lissu ana mtaji wa maneno na elimu, lakini wafadhili ndio tatizo. Upande mwingine Membe ana uwezo wa kuleta ufadhili na anaweza kwenye uwongozi pia.

Tukija kwa ACT, hicho chama bado kinataka msukumo mkubwa sana mpaka kikubalike zaidi kwa umma wa Tanzania, muda ni mfupi kukipika. Yani inabidi watu wamchukie kweli kweli Magufuli ndio ACT ipate mtaji wa haraka haraka. Hata hivyo, Membe atajipa mtihani mkubwa akisema aende kwa Zitto, bora Zitto apigetope mwenye kidogo kuongeza nguvu ya kukubalika. Membe ana weza kupoteza pesa yake kujenga chama na mwisho wa siku asipate kitu. Japo kuna tetesi Membe ana mtaji ACT (Msinifunge sina uhakika)
 
Acheni kuumiza vichwa kwa Mambo yanayojulikana ambayo hata mtoto wa la nne D anayajua.

"Rais wa JMT baada ya uchaguzi wa oct2020 Ni Dr. John pombe Joseph Magufuli". Hao wote uliowataja ni waamusha mawingu tu.
 
Physical appearance siyo hoja.Kibaki ameapishwa akiwa on wheelchair.
 
Tujipeni moyo tu,uraisi bado upo kwa magufuli hadi 2025.
Wapinzania na team nyingine zijipange na kuwekeza kwa mwaka 2025,kwa sasa washafeli tayari.
 
Yoyote katika hao watatu ndio wananchi watamuunga mkono (Ikiwa Membe, Zitto, Lissu), hata kama upinzani wakimsimamisha "MBUZI" agombee urais tutaenda nae kwakweli. Sio kwa hapa tulipofika kama nchi.
 
mliberali,
Kwa taarifa yako Membe au mwanaccm yoyote hawezi kwenda upinzani kwa ajili ya kuzielewa sera, zaidi ya kusaka madaraka. Hata huko ccm hawako kwa ajili ya ubora wa sera, bali wako kwa ajili ya urahisi wa kupata madaraka.

Enzi za watu kuishi kwa kujali sera ziliishia na kizazi cha kina Nyerere, hawa wote wa sasa ni maslahi Kwanza. Hiyo ya kusema sera ni lugha ya kufurahishia jukwaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…