ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Tumeshasimama turudi kwenye misingi yetu.Mngetengwa mgeweza kusimama?Dunia ilkua kwenye mabadiliko!period
Tumeshasimama turudi kwenye misingi yetu.Mngetengwa mgeweza kusimama?Dunia ilkua kwenye mabadiliko!period
Tumeshasimama turudi kwenye misingi yetu.
Mkuu jua kanisa ni kama jumuiya nyingine za kiraia zinazosajiliwa serikalini.... ukizingua msajili analifuta chap. Hata kanisa lako la SDA limesajiliwa. Gwajima kulitumia kanisa lake kufanya siasa ilikuwa sio sahihi. Kacheleweshwa sana.Mambo yanazidi kuchemka!
Huwezi ng'oa meno yote kisa jino Moja linauma.
Huwezi kufunga msikiti kisa sheikhe amefanya uhalifu.
Huwezi kufunga Kanisa kisa mchungaji mmoja amelumbana na serikali.
Kama kweli yatafanyika maamuzi ya kufunga Kanisa la Gwajima, hautakuwa uamuzi wa akili na hiyo sio suluhu kwani itachochea na kubadili uelekeo wa ugomvi.
Kwa sasa makanisa mengine yataangalia hoja za kufungiwa Kanisa la Gwajima zinamashiko au laa.
Kama hazina zitajenga kitu kingine ambacho hakitakuwa kizuri.
Gwajima hoja yake ni kupinga Utekaji na mauaji. Hiya ndio hoja kuu ya Gwajima. Ambapo serikali ilipaswa iwe upande wake. Sasa uje kufungia Kanisa kisa mtu kapinga utekaji na mauaji kwa kweli hiyo italeta shida.
Ni akheri taarifa hiyo ibaki kuwa fake lakini isiwe kweli.
Pili, kufunga Kanisa la Gwajima ni kuwakosesha waumini wanaosali na kuamini katika kanisa Hilo haki ya kuabudu. Ni kutengeneza ugomvi usio na sababu na watu.
Hii pia itatoa taarifa kwa wale waamini wa miungu iwe ni Allah, Yesu, Yehova yakuwa hata wao hawapo salama.
Ugomvi huu unahitaji umakini. Kwa sababu unahusisha imani za watu ambao kimsingi MTU anaweza kuwa tayari kufa kwaajili ya Mungu wake.
Hii kesi ilikuwa imeshaisha, kwani Gwajima yeye alisharusha kete yake kimakusudi ili iliwe. Jambo ambalo serikali ingepuuza kupunguza tension.
Huku Lisu kwa kesi hiyohiyo.
Kule Kitima kapigwa,
Hapa, sheikhe kauawa!
Leo kanisa lafungiwa.
Hata kwa sisi watunzi wa riwaya, na filamu, hatuwezi kutengeneza action movie au action story kwa kiwango hicho.
Ukishatoka kwenye taharuki unaipoza filamu kidogo kupunguza tension.
Lakini bandika bandua sio nzuri kwani huweza kuleta ujasiri wa liwalo na liwe.
Hata Marekani anapodili na adui zake hawezi kuwapiga bandika bandua. Kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuwapa adui zake muunganiko wa haraka, na ujasiri wa liwalo na liwe.
Ni kweli kwa sasa watanzania wengi sasa wanajua watekaji ni kina Nani. Kutokana na mazingira.
Kwa sasa tunajua msimamo wa serikali kuhusu utekaji na Yale yanayoendelea nchini.
Mungu awe sehemu yetu.
Barikiweni
Mkuu jua kanisa ni kama jumuiya nyingine za kiraia zinazosajiliwa serikalini.... ukizingua msajili analifuta chap. Hata kanisa lako la SDA limesajiliwa. Gwajima kulitumia kanisa lake kufanya siasa ilikuwa sio sahihi. Kacheleweshwa sana.
Kwanini wachungaji wako hawatumii muda wa ibada jumamosi kuongelea hayo mambo ya utekaji?Kupinga utekaji na mauaji ni kufanya siasa?
Utekaji na mauaji si uhalifu ambao hata serikalo inaupinga?
Kwanini wachungaji wako hawatumii muda wa ibada jumamosi kuongelea hayo mambo ya utekaji?
Na Tanzania ikiwemo,tukikomesha vibaraka wa Mabeberu kwisha habari Yao.Kwa vichwa vipi?
Taiga lenye uwezo wa kusimamia misingi yake na kukabiliana na ubeberu ni Uchina na urusi
Kasajili kanisa uendeleze alipoishia Gwajima..Ni sehemu ya Watekaji. Au wanapenda utekaji!
Au wanaunga Mkono utekaji.
Hilo ndio jibu
Kasajili kanisa uendeleze alipoishia Gwajima..
Na Tanzania ikiwemo,tukikomesha vibaraka wa Mabeberu kwisha habari Yao.
Eti roporopo kama Gwajiboy anajikuta biiiingwa 😂😂
Ndugu zako wewe wasio na maadili Wana faida gani?Kwa hiyo watekaji ndio KAZI yenu hiyo kukomesha ndugu zenu kwa kisingizio cha vibaraka wa mabeberu?
Ndugu zako wewe wasio na maadili Wana faida gani?
Waingize tuu king wenzio wasiokujua
Ndio mamlaka inatekeleza wajibu wake hivyo Sasa wa kisheria.Mtu asipokuwa na maadili Sheria za nchi zinasema atekwe na kuuawa?
Wewe keyboard warrior kaandamane kumtetea Gwajima.Mtu asipokuwa na maadili Sheria za nchi zinasema atekwe na kuuawa?
Hawezi anataka kuingiza wenzie King 😂😂Wewe keyboard warrior kaandamane kumtetea Gwajima.
Wewe keyboard warrior kaandamane kumtetea Gwajima.
Taharuki kwamba alichokiongea hakipo?Sio mtu mmja Bali ni Kiongozi wa hilo mnaloliita kanisa.
Mhuni mmja anatumia hiyo platform kuleta taharuki Nchini.
Rwanda Huwa hawacheki na Hawa wapuuzi na vijikanisa vyao vya kuibia pesa wajinga.
Kipo wapi? Kama kipo wewe ungepata nafasi s kuchati?Taharuki kwamba alichokiongea hakipo?