Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

Kufunga 'PM' ni dalili ya uchoyo; ni sawa na kupika chakula kizuri na kitamu, na kujifungia ndani na makufuli makubwa, ili mgeni yeyote atakayependa kuja kukutembelea, asiweze kuingia na kula chakula hicho ulichokiandaa; kwa namna nyingine tunasema huo ni uchoyo.

Pia inazuia mgeni kuja kukuletea habari njema; kwa sababu ataishia nje ya mlango, na hatoweza kuja kukuhabarisha habari njema zenye tija.

Ni sawa pia na kujenga nyumba na kuzungushiwa na ukuta mrefu; ili wapitao bara barani wasiweze kuingia ndani; na mara nyingi waliojifungia ndani, wanakuwa hawana furaha mpaka pale watakapo toka nje ya uzio na kujumuika na wapita njia n.k

Kwa ujumla, hiyo ni dalili ya uchoyo; fungueni 'PM'​
Unakuta una bonge la mchakato alafu PM unakuta lock .. ila ndio binadamu walivyo
 
Back
Top Bottom