Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali

Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali

Kwa maana hio malipo yale pia Wizara ya Mambo ya Ndani unapokea mgao?
Wanalipia usajili tu, baada ya hapo hela yote ni yao.Huyu Hassan Wamba aka Kiboko ya wachawi alikuja hapa miaka michache tu iliyopita akiwa hohe hahe leo hii ni multi billionaire akiwa jumba kubwa la kifahari na fleet ya magari ya kikubwa.
 
Kwa hio unakubariana na MIMI kwamba Serikali ndio inayowapa airtime na go ahead, Jamaa sio kwamba kafungiwa sababu ya nini na nini sababu hajailipa Serikali

Hapo unaposema ....baada ya hapo Hela yote ni yao..... sikubariani na Wewe hata robo Serikali hauwezi ukaiacha mikono mitupu wakati Wewe imekupa kibari cha kuingiziwa mabillion ya shillings hakuna HIO Serikali
 
View attachment 3053355

Serikali kweli IPO kazini Kwa kuchukua hatua ya haraka pale inapobainika mahali watu wanaenda isivyo. Kiboko ya wachawi amekuwa akimfanyia kazi ya Mungu kama kufanya uganga na ushirikina ufanyikavyo.

Pia soma: DOKEZO - Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Ukristo umekuwa ukidharirishwa sana na watu wanaojiita watumishi wa Mungu lakini wakifanya mambo ya ajabu.

Tumeeona athari za imani potofu pale watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha. Nampongeza sana rafiki yangu na aliyekuwa CR wangu pale chuoni Mr. Emmanuel Robert, msajili wa jumuiya za kijamii Kwa kazi nzuri inayoendelea kufanya. Unamuwakilisha vema Dr. Samia
Balua=barua
Shughuri= shughuli
Kabra=kabla
Talehe=tarehe
Ishilini=ishirini
Mahubili=mahubiri
Ushilikina=ushirikina
Kilaia=kiraia
Kimeamliwa=kimeamriwa
 
Qur'an haina ujinga huo, aliyekwambia anatumia Qur'an kufanya "uganga wa kienyeji" kakutapeli huyo.

Isome Qur'an kijana, usidanganywe kijinga.
Kwenye korani ndimo kuna habari za majini na mapepo na yanaabudiwa na waislamu. Uliona wapi biblia inayasifia majini na mapepo?
 
Leo unayakana makanisa? Kwani hii mada umeisoma kichwa cha habari?
Sijakana Makanisa bali nimesema hao wanaofanya huo utapeli hayo siyo Makanisa na hata usajili wao wamesajiliwa kama jumuia za kidini na siyo Kanisa. Hiyo heading ndiyo maana hata mwandishi kaandika kanisa badala ya Kanisa. Hakuna Kanisa linatoa huduma za Kiroho kwa malipo na ndiyo tofauti na hao matapeli. Makanisani hakuna maji, chumvi, keki, asali au vitamba vyaupako,huo ni ushirikina tu hakuna maelezo zaidi ya hayo.Hata kwenye mikusanyiko yao wanaofika ni watu wa dini zote Wakristo, Waislam na hata wa dini za asili , lakini Kanisani wanakwenda Wakristo wa Madhehebu husika na hata ibada zao zina mfumo unaoeleweka yaani Liturgia lakini huko ni makelele tu na kumwagiana maji kisha kuuziana hizo azima zao.
 
Vipi lile ambalo padri ameshikwa kwa kuua albino?
 
View attachment 3053355

Serikali kweli IPO kazini Kwa kuchukua hatua ya haraka pale inapobainika mahali watu wanaenda isivyo. Kiboko ya wachawi amekuwa akimfanyia kazi ya Mungu kama kufanya uganga na ushirikina ufanyikavyo.

Pia soma: DOKEZO - Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Ukristo umekuwa ukidharirishwa sana na watu wanaojiita watumishi wa Mungu lakini wakifanya mambo ya ajabu.

Tumeeona athari za imani potofu pale watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha. Nampongeza sana rafiki yangu na aliyekuwa CR wangu pale chuoni Mr. Emmanuel Robert, msajili wa jumuiya za kijamii Kwa kazi nzuri inayoendelea kufanya. Unamuwakilisha vema Dr. Samia
Wamechelewa sana na sijui Serikali itawasaidia vipi wale Watu ambao si tu Wametapeliwa bali Wameumizwa na huyu Tapeli.
 
Mfalme Zamaradi yupoo?

Tukisema wajinga ndiyo waliwao mnapinga.

Njooni katika Uislam kama kweli mnaimani na Mwenyezi Mungu.
 
Sababu walizozitaja mpaka kumfungia ni dhaifu.
Eti kiwango kikubwa cha kumuona , wao kama wasajili wanataka kiwango gani?
Kila nabii na watumishi wengine maarufu hapa Bongo wana kiingilio cha kuwaona sema inakuwa siri . Kiboko ya wachawi tatizo aliweka wazi tofauti na hao wengine.
Nchi hii drama nyingi akienda kuomba msamaha na kukubali kuunga mkono CCM na kumnadi Samia atafunguliwa soon
Wewe ni kiazi pale kuna watu wanalia kama watoto sio kumuona tu baada ya kumuona unaambiwa pesa ya kukumbea sio chini ya milioni watu wanatoa hadi milion 20 na hawapati matokea maana pale ni utapeli tu hakuna lolote

USSR
 
Wanalipia usajili tu, baada ya hapo hela yote ni yao.Huyu Hassan Wamba aka Kiboko ya wachawi alikuja hapa miaka michache tu iliyopita akiwa hohe hahe leo hii ni multi billionaire akiwa jumba kubwa la kifahari na fleet ya magari ya kikubwa.
Alikuwa muuza kuku Buza ,anasema alinunua nguvu ya wachawi milioni 7

USSR
 
Shalom!

Serikali inayojali raia wake na mali zao ni ile inayochukua hatua za haraka sana pale jambo tatizi linapotokea kwa raia wake.

Ni hapa hapa Jamii Forum nimeandika na kurudia kwamba huyu Raia wa DRC anatumia imani ya Watanzania kutapeli na kujipatia fedha nyingi mno kinyume na taratibu za kiimani.

Hata kama nchi yetu haina dini lakini watu wake wana dini na imani zao, ni sharti Serikali inayojali watu wake kuangalia kama imani hizo zinaistawisha jamii au kuangamiza?

Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi ameteua "engo" ya kuwapiga Watanzania masikini bila huruma akitumia staili ya ramli chonganishi. Kuna vifo vimetokea na vinaendelea kutokea kutokana na mahubiri ya Dominic anayevaa "gloves" nyeusi saa zote za ibada yake pamoja wasaidizi wake ambao wote ni wakongo.

Shuhuda za waliopoteza fedha kwa Dominic ni nyingi mno. Wengi wameuza mali zao kusaka maisha bora kwa Mzee wa Buza kwa Lulenge bila mafanikio. Baadhi ya kina mama wamefilisika kwa Dominic maana kukutana name ni Sh 500,000. Kukutana na wasaidizi wake (wakongo) ni kuanzia 100 000 hadi 300,000.

Wengine wameuza samani za ndani, nyumba, mifugo, nakadhalika kuponyeshwa magonjwa ya wazi kama Ukimwi. Presha, Saratani, Minyoo na kaswende. Wizard ya Afya iko wapi ku-clearify mambo haya ya kisayansi?

Kwa nini asiyafanye haya nchini Kongo? Kwamba mahaba yake ni kwa Watanzania pekee? Wajinga waliwao. Rwanda wameweza kudhibiti upumbavu huu. Kenya wamefuata na Burundi nao wameweza. Na sisi tuweze. Huyu tapeli apewe saa 24 kuondoka nchini na mali zake zitaifishwe ili iwe fundisho. Lakini na sisi umma tujiepeshe na hizi ramli chonganishi kupitia madhabahu ya kiimani. Hongera Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
#KaziIendelee!
 
Back
Top Bottom