Sijakana Makanisa bali nimesema hao wanaofanya huo utapeli hayo siyo Makanisa na hata usajili wao wamesajiliwa kama jumuia za kidini na siyo Kanisa. Hiyo heading ndiyo maana hata mwandishi kaandika kanisa badala ya Kanisa. Hakuna Kanisa linatoa huduma za Kiroho kwa malipo na ndiyo tofauti na hao matapeli. Makanisani hakuna maji, chumvi, keki, asali au vitamba vyaupako,huo ni ushirikina tu hakuna maelezo zaidi ya hayo.Hata kwenye mikusanyiko yao wanaofika ni watu wa dini zote Wakristo, Waislam na hata wa dini za asili , lakini Kanisani wanakwenda Wakristo wa Madhehebu husika na hata ibada zao zina mfumo unaoeleweka yaani Liturgia lakini huko ni makelele tu na kumwagiana maji kisha kuuziana hizo azima zao.