Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Pamoja na kuwa atakuwa hayuko majukwaani lkn mazingira ya jinsi NEC ilivyomzuia yanatosha kumpigia kampeni, sasa wananchi na jumuia za kimataifa zimejua kweli Tume haiko huru na inapendelea, vyombo vya habari vya ndani na nje vinaripoti habari yake.

Muda huu apumzishe ubongo na akili na mikiki mikiki ya barabarani, afanye tathimini ya kampeni aliyoifanya, muda huu anaweza kuutumia kwa press conferences, kupitia daftari la mpiga kura, kuandaa mawakala, jinsi ya kuzuia wizi, kuandaa polling center, kutafuta pesa za kampeni, kufuatilia rufaa za wagombea, n.k.

Wapinzani walizuiwa kufanya siasa kwa miaka mitano lakini baada ya kuruhusiwa tumeona walivyobadili upepo kwa muda mfupi, nini siku 7. Magufuli amejaza mabango kila kona ya nchi lkn faida yake haina tofauti na yule ambaye hana picha hata moja. Kwa hiyo kama wananchi hawakutaki hata ufanye kampeni peke yako hawatakuchagua.

Lissu afahamu tunatafuta Rais atakaye simamia misingi ya sheria kwa wanaoonewa na wasioonewa, hata kama ameonewa tayari wananchi wameshaona, ajishushe kwa moja ili apate mbili.

Mwisho, Mungu naye ana makusudi yake, hatuwezi kujua ndani ya hizi siku 7 kungetokea nini kibaya walichopanga juu yake.
 
Mitazamo ya wengi Ni kuwa Lissu atavuna Mara 3 zaidi ya kura ambazo angepata. Kuna ukweli huu, Mungu anapotaka kukushusha kwanza anakuondolea maarifa na busara, anakuacha utumie nguvu bila akili.

NEC wanaisaidia sana CHADEMA kupata kura za wale wasio na upande.
Lissu kwa hili la NEC kufumbia yanayoendelea kwa CCM na kuendelea tu kubana upande wa upinzani ni dhahiri sasa Lissu atakuwa mshindi bila kutumia gharama kubwa.

Hii yote kwao ni kuonyesha uoga. Hivi ni kweli hawamsikii na kumuona Magufuli anavyofanya kampeni zake na kuingilia ratiba, kutoa hotuba ya vitisho na kugawa hela huku akionyeshwa live.

Ni uoga gani huo kwa kuvunja kanuni halafu wanakuja nao kusema kuwa wagombea fulani wazungumze sera namna watakavyowaletea watu maji nk.

Je, hawajamsikia JPM akiwatisha watu kuwa hawatapata hayo maendeleo wasipomchagua? Hiyo ni salama kwa umoja wa wananchi watoa Kodi? Uwanyime maji kisa wamemchagua mbunge unayemtaka wewe. Tuseme tu bado nampa Lissu 60% ya ushindi.
 
Mnafunika kombe Lissu apite hahaha yeye kama kweli mwanaume na anajua sheria asimamie maneno yake ya kwamba lazima aendelee na kampeni tuone nani mwamba.

Sio muanzishe uzi za kutaka kuaminisha watu kua Lissu kaamua kuacha kuendelea na kampeni kwa sababu yenu
na ushauri wenu sote tunajua Tundu Lissu amefyata mkia
 
Magufuli alisema yeye ni jiwe hashauriki lakini sikuhizi jiwe anawapigia magoti watu kwanini asiendelee na ujiwe wake?
 
Mnafunika kombe Lissu apite hahaha yeye kama kweli mwanaume na anajua sheria asimamie maneno yake ya kwamba lazima aendelee na kampeni tuone nani mwamba.

Sio muanzishe uzi za kutaka kuaminisha watu kua Lissu kaamua kuacha kuendelea na kampeni kwa sababu yenu
na ushauri wenu sote tunajua Tundu Lissu amefyata mkia
Wewe akili huna, si kwamba umekunywa maji ya bendera ya ccm tu, ia umekula mavi yake. Umerogwa ukarogeka.
IMG-20200906-WA0005.jpeg
 
Back
Top Bottom