Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Ntakuwa Samaki Samaki M city nikiwa sehemu ya kizazi kilichoshuhudia TANZANIA ikiend AFCON kwa mara ya pili!
 
Tuwatakie kila la kheri tu vijana wetu washinde, lakini tusimhusishe Mungu kabisa katika hili. Mungu hawezi kutubariki wakati nchi inavurugwa kwa makusudi. Nchi hii ina maana jamani na sasa kwa utawala huu wa awamu ya tano ndiyo laana inazidi kuimarika. Sisi ni watu wa ku-loose tu mpaka tupate akili.
 
Hili taifa lina upinzan wa kipuuz huenda hakuna dunia nzima.Mtu anakuambia Mungu ibariki Lesotho, sababu za mcng utasikia oooh taifa stars ikishinda jiwe atapata sifa mara CCM watasema ni mafanikio yao.

-tatizo ni akili mkuu,

-akili ndogo ni nyingi sana nchi hii

-tuwasamehe.
 
-ni kweli Mungu hawezi kutusamehe maana sasa hivi tunapinga hadi ushoga, tunamkosea sana huyo mungu wako asee.
 
ukiona unaloose mkuu jua ni wewe na family yako tu mkuu wengine sisi mwendo mdundo aka moto mchibuyu yaana hakuna kuloose wala kufeli, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TAIFA STARS,
 
Wakati JIWE aliishaipiga mkosi! Safari, May bê safari ya sinza Kwa Remy
 
Mkuu hayo leo hayasaidii. Tujifunze kujua tuseme nini wakati gani. Lolote litakalotokea leo huko nje itakuwa ni sura ya Tanzania wala si TFF wala nani. Pamoja na mapungufu yote lakini tukishinda ni ushindi wa Tanzania.
Ukweli hujitenga na uongo. Sitegemei jipya huko Lesotho, walikuja japa TFF wakawapeleka Chamazi tukatoka sare, Leo wako Kwao Maseru unawafungaje? Samatta naye kadi za mano hachezi. Tufungwe tubadirike.
 
Mbona mpaka sasa mshindi anafahamika, ujue unashangaza sana mkuu, mi nakupa ukweli daima,

Najua mtaniita sio mzalendo,
Sisi tut ashiriki hayo mashindano kupitia kwa diamond platnumz.
Naunga mkono hoja yako, ache Madanganyika yajitie mazalendo wakati hao viongozi wenyewe hawako tayari kubadirika.
 
na kwa sababu hii hatuta kuja kuendelea.
 
Tuliposhiriki AFCON ya mwisho mwaka 1980 wengi humu tulikuwa tunachezea maringi na kuendesha matairi kwa miti.

Enzi hizo magazeti yanauzwa pale posta mpya na posta ya zamani. Uhuru, Mzalendo, Daily News na Jumapili Sunday News. Katuni maarufu ni zile chakubanga. Mwandishi maarufu ni James Nhende wa gazeti la mfanyakazi lililokuwa likitoka jumamosi.

Hawa kina Diamond, Wema, Rooney Ronaldo, Chris Brown na Jokate walikuwa bado wanatembea viunoni mwa Baba zao.

Na kwa wale wadogo zao pengine hata wazazi wao walikuwa hawajakonyezana.

Mungu ibariki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania, nchi pekee uliyotujalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…