Kuhama kituo cha kazi kutoka mkoa X kwenda mkoa Y ndani ya taasisi moja

Kuhama kituo cha kazi kutoka mkoa X kwenda mkoa Y ndani ya taasisi moja

Jackline Akyoo

New Member
Joined
Aug 23, 2025
Posts
3
Reaction score
2
Mimi ni mwajiriwa kwenye taasisi X na nimepangwa mkoa ambao mazingira yake sio mazuri kuendana na afya yangu. Nataka niombe kuhama kwenda mkoa Y.

Je, inawezekana ikiwa bado sijathibitishwa kazini? Na nifanye nini ili uhamisho wangu uweze kukubalika?
 
Mimi ni mwajiriwa kwenye taasisi X na nimepangwa mkoa ambao sijaupenda na mazingira yake sio mazuri. Nataka niombe kuhama kwenda mkoa Y, je inawezekana ikiwa bado sijathibitishwa kazini? Na nifanye nini ili uhamisho wangu uweze kukubalika?
Wewe dada kafanye kazi ukifika uko Lima ata mpunga na mtama utatatoboa
 

Kuwa mzalendo dada, Tanganyika ni moja.
 
Nenda kazini kwanza uingie kwenye mfumo kisha uanze kutafuta uhamisho, unatafutaje uhamisho na bado hawakujui.
 
Hakuna kinachoshindika kiongozi.Pesa yako na unamjua nani ndio mkombozi wako.Sema huu mkoa Y ni upi ambao mazingira yamekuchanganya ndugu?(Bariadi unapajua kweli?kama nimeweza kuishi mimi hapa basi na wewe utaweza ,vumilia kidogo badae utazoea)

Usicheze na fursa hiyo,mtaani kuna wenzako ni any job sir,any place.Wanaweza kupita na hiyo fursa
 
Mimi ni mwajiriwa kwenye taasisi X na nimepangwa mkoa ambao sijaupenda na mazingira yake sio mazuri. Nataka niombe kuhama kwenda mkoa Y, je inawezekana ikiwa bado sijathibitishwa kazini? Na nifanye nini ili uhamisho wangu uweze kukubalika?
Utafuta kazi, ukapata kazi, kafanye kazi. Hayo mazingira magumu, walioko huko wamekufa?. Wenzio hata hiyo nafasi hawana, Acha madeko
 
Hayo ni mambo ndani ya Taasisi, pambana na maboss wako
 
Sababu ni afya yangu nd inanifanya nitake kuhama pia nilisharipoti tayari nipo kazini sio kwamba bado sijafika
 
Uhamisho wa ndani huo, Nadhani unaishia kwa Mkurugenzi wako. Omba tu
 
Back
Top Bottom