Kuhani Musa: Aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu

Kuhani Musa: Aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu

Kwanza avue hayo Mavazi ya Mapadri wa kikatoliki

Daudi alipoyavaa hayo mavazi alikua Mkatoliki??

Msituchonganishe wakatoliki, sisi ni kanisa mama wote hao ni uzao wetu
 
Huyu niliona interview yake clouds TV akisema eti alikuwa anafanya kazi Bank huko Arusha wakati aliacha shule std 4
Sawa aliacha std 4 je! uliendelea kumfuatilia kujua historia yake baada ya hpo je km alihamia mkoa mwingne na kuendelea na masomo
 
Huyu niliona interview yake clouds TV akisema eti alikuwa anafanya kazi Bank huko Arusha wakati aliacha shule std 4

Kwa maneno yako haya unaweza kuwa na makaratasi vyeti ya elimu lakini akili huna.

Watu kama wewe ndio mnasabubishaga vyeti na elimu zetu zionekane kama wewe unavyoonekana

Mfyuuuu
 
Kuhani Musa Richard Mwacha anasema aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu aliyemuweka pale, ili atamtereshia maarifa na ufahamu wa kuyafanya mambo mazuri yatakayokufanya ufurahie. Sasa wewe huna maombi.......

Alikuwepo Magufuli pale lakini Mungu alimchukua kama alivyokuwa anasema mwenyewe; akamwacha huyu mama, sasa ulitaka ukae wewe!?

Tujifunze kuwaombea viongozi wetu, tuwasupport! Hakuna mtu anayekusudia kufanya mabaya na hakuna mtu ambaye anataka amalize vibaya aache historia mbaya popote pale

View attachment 2691266

Tumsupport Rais na tumuombee sana
Asante sana mama D kwa uzi huu, wewe ni baraka, Kuhani Musa ni mtumishi wa Mungu wa kweli!. Mimii pia ni mwana Ngomeni!, bila kuhama kwenye dhehebu langu la asili, from time to time huwa najumuika pale Ngome ya Yesu, Kimara Temboni.
P
 
Back
Top Bottom