Mkuu mimi mseminary nimekuwa kwenye misingi hiyo ....hakuna maombi bora kama kujisafisha mwenyewe na kuomba kwa Baba wa Mbinguni ........Imani thabiti ipo ndani yako wewe mwenyewe hawa sijui nabii mara mtume au mara kuhani ......tunapoenda hatujui maana unaweza kusema huyu mlevi ameingia vipi halafu kuhani na nabii au mtume feki tunaonja joto la jiwe.....basi mitume na manabii wote enzi za agano la kale mpaka jipya wangekufa wakiwa matajiri
Unajua maana ya neno Kuhani? Kule seminary ulifundishwa tofauti gani kati ya mitume, manabii; wainjilisti, wachungaji na waalimu? Unajua Kuhani ni nani na padre ni nani?
Mungu wetu hana mipaka. Yeye ndio huchagua nani amtume, amtunze lini na amtume wapi?
Hata Yesu alipingwa na wakuu wa dini tena makuhani wakuu. Jitafute kwenye maelekezo ya Mungu, usikariri ndugu
WAEFESO 4:11-13
"Naye alitoa wengine kuwa 1 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo"
1 WAKORINTO 3: 3:12
"kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?
Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri."
MHUBIRI 9:11
"Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba
si wenye mbio washindao katika michezo,
wala si walio hodari washindao vitani,
wala si wenye hekima wapatao chakula,
wala si watu wa ufahamu wapatao mali,
wala wenye ustadi wapatao upendeleo;
lakini wakati na bahati huwapata wote."