Watoto wanne(4) wa familia moja waliokufa mwaka jana kwa miezi tofautitofauti kuanzia mwezi September hadi December wafufuka.
Habari ya YUSUFU IBRAHIM MUSA kwa ufupi
Bwana YUSUFU IBRAHIM MUSA ambae ni mwenyeji wa Kigoma anaeleza kwamba miaka mitatu iliyopita alikua mzima wa afya yeye, mke wake na watoto wake wote wa4.
Lakini kipindi hichohicho mke wake alifariki ghafla, na alikua na rafiki yake aliyetoka musoma na mkewe kwenda kigoma kumzika mke wa YUSUFU IBRAHIM MUSA. Wakiwa bado pale msibani, mke wa huyo rafiki yake alikufa palepale kwa ghafla. Ndipo YUSUFU akatakiwa kusafirisha msiba hadi musoma na kuzika. Baada ya mazishi wakiwa kwenye gari binafsi kurudi kigoma ndipo alipata ajali na kulazwa Bugando hospitali kwa miezi 20.
Anasema baada ya miezi 20 kuwa hospitali alipata nafuu sehemu zingine lakini mguu uliendelea kumpa shida na madaktari wakamshauri waukate maana hapakua na uwezekano wa kutibika. Akiwa anasubiri tarehe ya kukatwa mguu alipita mtu alimuuliza kama anaamini kwenye matumizi ya vifaa vitakatifu(maji na mafuta). YUSUFU alikubali na alipotumia tuu mguu ulipona na akaruhusiwa kutoka hospitali.
Baada ya kupona bwana YUSUFU IBRAHIM MUSA anasema alitoka hospitali akaenda nyumbani kigoma kisha akaanza safari ya kwenda Dar es salaam ili afike kwenye kanisa lililompatia uponyaji.
Lakini bahati mbaya alipofika Dar es salaam tuu kabla ya kufika kanisani mwezi wa tisa 2021, mtoto wake wa kwanza alifariki kwa kuvamiwa na wezi na kuchomwa visu. Alienda kuzika na baadae watotonwake wengine wa3 walikufa kati ya mwezi october hadi december na wote vifo vyao vikihusisha ajali kitu kilichomfanya yeye ashindwe kufika kanisani kama alivyodhamiria.
Bwana YUSUFU IBRAHIM MUSA anasema alifanikiwa kufika ibadani kwa Kuhani Musa January 2022 baada ya kuwazika watoto wake wanne. Wiki chache baada ya kufika kanisani alipata faraja na tumaini jipya la kuishi kwa jinsi Mungu alivyokua akimuonyesha ukuu wake haswa kwa kumuonyesha wale waliokua wabaya kwake waziwazi. Na kubwa zaidi alipigiwa simu toka kigoma kuwa yule mtoto wake aliyefariki mwishoni, tarehe26 December 2021 ameonekana huko kigoma. Mtoto huyu alipata ajali akiwa kigoma akaumia vibaya kichwani, wakampa rufaa ya kwenda muhimbili hospital Dar es salaam (MOI) alifika akiwa na hali mbaya lakini baada ya siku 2 akafariki wakasafirisha mwili na kwenda kuzika Kigoma.
Hadi naandika hapa watoto wote wa4 wa YUSUFU IBRAHIM MUSA waliofariki na wakazikwa wamepatikana (katika maeneo tofautitofauti wakiwa hai, mmoja akipatikana kigoma na watatu wakipatikana kwenye visiwa tofautitofauti vya ziwa Victoria wawili wakiwa upande wa Tanzania na mmoja Uganda) na wote ameshawafuata na kuwafikisha kanisani kwa Kuhani Musa.
Habari mpya toka kwa YUSUFU ni kwamba amepigiwa simu kuwa mke wake nae amepatikana upande wa ziwa karibu na Zambia
Bwana YUSUFU anasema imekua rahisi kuwa anapokea taarifa hizi sababu amezaliwa kwenye familia ya wavuvi babu yake Mzee MUSA akiwa mvuvi mkubwa na maarufu na hawa watoto wote walitambulika baada ya watu kuwakuta kwenye mazingira tata na wavuvi waliokua ziwani wakiwa wanawashangaa waliweza kuwatambua
Bila kusahau babu wa YUSUFU mzee MUSA alifariki ghafla mara tuu YUSUFU alipofika kwa kuhani MUSA na ndipo watoto hawa wakaanza kuonekana. Babu huyu hakufariki peke yake, alifariki yeye na watu wengine 17 wanaodhaniwa kushirikiana nae kuwapoteza watoto hawa
KUHANI MUSA RICHARD MWACHA NI NANI??