Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Umejitahidi kutafuta matusi lakini umeshindwa. Ni wachache sana ( kama wapo) wanaotumia hayo maneno.
Nyie mna bunge lenu, jeshi lenu na Rais wenu kwa nini msipeleke hoja katika bunge lenu kudai Muungano uvunjwe? Lakini kama ilivyo siku zote, mnataka mtanganyika awafanyie hii kazi ili baadae mjidai kuwa hamkutaka Muungano uvunjwe.
Watanganyika hawana serikali yao, nyie wenye serikali ndio mnatakiwa kulianzisha. Au mnaogopa kuwa mkifanya hivyo kweli utavunjika? Na mambo ya " changu changu na chako chetu" yatakoma.
Amandla...
Kama unavyoona ni wachache na Mimi naona pia ni wachache.
Umesema wabunge au wawakilishi wapeleke hoja ,
Uchaguzi wote wa Hao wabunge na wawakilishi husimamiwa na wa Tanganyika.
Wewe huwezi ukagombea nafasi yoyote bila idhini ya mkoloni Tanganyika.
Sijawahi kusikia kuna jeshi la Zanzibar. Jeshi ni la Tanganyika
Polisi wanaosimamia ni wa Tanganyika , Usalama ni Tanganyika.
Uchaguzi wa 2015 Baada kuona wabunge na wawakilishi wa upinzani wameshinda , Kikwete akaleta jeshi kwenye ofisi Za Tume ya uchaguzi na akalazimisha kufutwa uchaguzi.
Ondoweni majeshi na mapolisi kutoka kila mtaa ndio utuambie maneno hayo