Ni swali Zuri.
Moses phili si MCHEZAJI mzuri kihivyo mnavyo fikilia.
Nitaweka hoja chache useze kunielewa Moses Phili.,
1. Kwanza kabisa haendani na Falsafa ya Robertinho, kimo,kutokukaba, KUPOTEZA MIPIRA.
2. Moses phili ni mchezaji anayependa kucheza No 10.
Namba kumi Simba Kuna Chama, Saido na sasa ongezeko la Ngoma ambaye AMECHEZA kwenye no 10 kwa Muda mrefu, vita, raja.
3. Moses phili Hana uwezo wa kukabia juu, anapoteza sana MIPIRA, featness level yake IPO CHINI ukilinganisha na Onana, KIBU na Baleke
Hili haliitaji hata kulielez.
Uwezo wa phili kukaa na mpira ni mdogo sana.
4. Hana madhara Nje ya 18.
Ni kama Kagere anafunga ndani ya 18 ni potcher mzuri mno
5. Si MCHEZAJI WA Michezo mikubwa.
JARIBU kufuatilia mchezo WA Simba na yanga ulioisha kwa goli 1-1 Azizi ki na Okra. Moses alipoteana kabisa uwanjani alicheza Dakika 80 hakupiga shuti hata Moja muda worte aliocheza
6. MAKOCHA wawili WA Simba kutomuelewa.
Zoran mark na Robertinho wote hawana Imani na phili, Zoran maki ALIWAHI kumtumia kyombo kwenye Mechi ya Simba na yanga Ngao ya Jamii dk 80 na KUMUACHA BENCHI PHILI.
Magoli ya Sakho na Mayele 2-1
BINAFSI NIMESIKITIKA SANA KUONA SIMBA INA MAWINGA 10
NIMESHANGAZWA SANA KUMUONA BANDA.
Yanga 1-1 Simba
Mechi ya Yanga na Simba ilisababishwa na uchoyo wa Okrah na hilo wote tunalitambua.
Phiri ndio mchezaji ambaye hajaonesha ubinafsi anapokuwa na mpira mguuni.
Ile mechi Phiri ndio alikuwa mchezaji wakuchungwa sana kwasababu alikuwa yupo katika peak ya juu karibia kila mechi zilizopita alizocheza alikuwa anafunga.
So Yanga waliwekeza nguvu kubwa mno kumdhibiti asiweze kufanya madhara na ndio hapo ambapo Okrah akapata mwanya wa kung'aa kwasababu hakuna mtu alitegemea kuona Okrah anaweza kuwa tushio kiasi awekwe kwenye uangalizi.
Lakini pia sio kweli kuwa Phiri hakupiga shuti hata moja golini kwenye mechi hiyo.
Hana uwezo wa kukabia juu
Kwanza kabla hajasema hawezi kukabia juu angalia na role yake anayocheza, kisha angalia majukumu ya hiyo nafasi utaona kama swala la kukaba ni swala la kumpa mtu lawama.
Haendani na falsafa ya Robetinho
Ndio kile kile tulichokisema alipomtoa Chama kwa hoja hiyo hiyo kuwa haendani na mfumo wa kocha. Lakini saizi hakuna mtu mwenye swali kwanini Chama haendani na mfumo wa kocha.
Je ni kocha kaweza kum train Chama aendane na mfumo? Why asifanye hivyo kwa Phiri pia?
Hana madhara nje ya 18
Hapa ungeweka ufafanuzi wa aina ya madhara unayokusudia.
Ni kwamba akiwa na mpira katikati ya uwanja ulitegemea kuona madhara gani kwa eneo hilo?
Ukisema nje ya 18 hana madhara wakati tumemuona mara nyingi anatokea huko akiwa amekusanya kijiji hadi kwenye 18 na kufunga goli unakuwa unatuchanganya.
Makocha wawili kutomuelewa
Hapa na mimi nikuulize swali
Kwani wewe uliwahi kumuelewa Zoran?
Zoran wachezaji aliokuwa anawaelewa karibia wote tumewatimua, so bado unataka tuendelee kuamini mawazo yake?
Zoran pia hakuwahi kumuelewa Chama, vipi na wewe humuelewi Chama kwasababu Zoran hakumuelewa?
***********
Hayo madhaifu uliyoyaelezea ingekuwa hayapo kwa wachezaji ambao Robertinho anawapanga basi tusingeruhusu goli hata 1 achilia mbali kupoteza mechi.
Lakini preference ya kocha kwa Kibu mwenye kiwango cha mashaka ambacho hakina consistency ndio tunapoamua kupaza sauti zetu.
Hatulaumu mchezaji kukaa benchi, tunalaumu mchezaji bora kukaa benchi huku wapo waliopewa nafasi na hawaoneshi kiwango bora na Kocha hafanyi mabadiliko.