VP mambo ya kiroho kama vile uçhawi, ushirikina , mapepo , mashetani , miujiza je unayaamini ? Na kama huyaamini kwànn yanazunguzwa maeneo mengi, tunasikia visa kama vile mtu karogwa flani ni mchawi na visa vingi vya kichawi Kwa njia ya Mikasa na stori za mtaani je hvyo vyote unaviamini au ushawah kuvishuhudia ? Naomba SoMo apo mkuu. Mana japo sijawah kushuhudia vtu km hvyo vya kichawi lakn stori zote hzo nazozisikia kuhusu uchawi ziwe za uwongo🤔 VP mtu kaenda Kwa mganga na hawajuan na mganga afu mganga anamfunulia vtu vya huyo mtu kana kwamba wanafahamiana . Pia kwñy upande wa Mali za Giza zinazohusisha utoaji kafara wa damu , misukule stori za chama Cha kishetani , utajiri wa nyoka nk je mkuu vitu vyote hv viwe ni vya kufikirika kwel🤔 mana vitu hvi vyote vinahusiana na uwepo wa MUNGU. Pia uko marekani Kuna watu wanamtukana na kumfanyia dhihaka MUNGU na yesu kristo je kwann wanatumia nguvu nyngi kutukana vitu ambavo havipo ni vya kufikirika🤔
Mambo ya imani za uchawi, ushirikina, mapepo, mashetani, miujiza ni derivatives za maongezi ya Mungu tu. Ukimuondoa Mungu na kwenda kwa ulimwengu wa kisayansi unaona hizo habari zote ni ujinga tu.
Jamii ambayo hata haijaelewa changamoto za afya ya akili mtu akiwa na matatizo yoyote jibu rahisi ni "karogwa" tu.
Hao waganga wanatumia saikolojia ndogo tu kumjua mtu na mara nyingi hata story wanaipata kw amtu mwenyewe na kuirudia tu.
Ukiwa hujiamini, ukaenda kwa mganga, mganga akakufanyia uchawi w akafara mkatoa tambiko, na lile tambiko likakupa confidence ya kisaikolojia kupigana mpaka ufanikiwe, ukifanikiwa utajuaje umefanikiwa kwa sababu uchawi umefanya kazi kichawi na si kwa sababu umepata psychological boost kujiamini na kufanya kazi zaidi tu?
Kuhusu kutukana Mungu ambaye hayupo, mimi sitaongelea kutukana, nitaongelea mfano wa mtu anayetumia muda mwingi kuelimisha jamii kwamba Mungu hayupo, kwa nini atumie muda mwingi kuelimisha jamii kuhusu Mungu ambaye hayupo? Kama hayupo si hayupo tu?
Kuna tatizo gani kuamini Mungu ambaye hayupo?
Kuna tatizo kubwa. Fikiria daktari anayeishi na jamii ya watu wajinga yenye ugonjwa ambao hauna tiba wala chanjo. Watu wale hawajali maambukizi ya ugonjw ahuu, kwa sababu wameaminishwa kuna dawa ya ugonjw ahuu. Lakini dawa ile si ya kweli, ni ya uongo.
Huyu daktari hana wajibu wa kuwaelimisha wale watu kwamba hiyo dawa wanayoitegemea si ya kweli? Ana wajibu. Uongo unaathiri, unaua. Ukiamini dawa ya uongo unaweza kufa.