Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Aliyesema kuwa watapewa mafuta na Oman ni mzanzibari sio mimi. Na ni kitu gani kinachowazuia wa Omani kuwamegea utajiri sasa hivi kama ambavyo wanawamegea waomani wenzao?

Unaposema kuwa Muungano umeshindwa kuwaletea faida Wazanzibari una maana kuwa mlitegemea watanganyika ndio wangewapelekea maendeleo? Shule, hospitali zote ziko chini ya serikali yao, JMT inahusika vipi? Kama wameuchoka kwa sababu walitegemea watanganyika wawabebe basi bora wauvunje watafute mjomba wa kuwabeba. Wazanzibari wanatakiwa wajitathmini wenyewe ili wajue wapi wanakosea.

Waunguja wapime athari za kuwaminya wapemba kwa uchumi wao halafu wajirekebishe. Unadhani wapemba wamewekeza Bara kwa sababu wanawapenda sana machogo? La hasha, walifanya hivyo baada ya kunyimwa fursa na wazanzibari wenzao. Wazanzibari wajitahidi kujenga nchi yao wenyewe kama ambavyo Singapore na Mauritius walivyofanya. Wakiendelea wao na sisi tutaendelea ndio maana hatufurahii umasikini wao.

Amandla...
 
Viongozi aina ya Othman watatuchelewesha sana kufikia Muungano wa kweli na kuondokana na huu Muungano wa magumashi.
 
Nani mnufaika mkuu wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanzania bara ?
 

Oman haina jukumu la kuinua uchumi na kupunguza umasikini wa Zanzibar ambayo sasa hivi ni sehemu ya Tanzania. Hilo ni jukumu la serikali ya JMT ambalo na wewe unakubali limewashinda mpaka sasa hivi. Sasa Wazanzibari lazima wajiulize huu muungano faida yake nini? Unaweza kujibu hilo swali?
 
Hapana. Jukumu la serikali ya JMT sio kupunguza umasikini Zanzibar. Jukumu hilo ni la SMZ. Jukumu la JMT ni kuhakikisha usalama wa nchi ya Tanzania, kuhakikisha hali ya uchumi ( sio biashara) iko vizuri na mahusiano yetu na nchi nyingine uko vizuri. JMT ina jukumu la kupambana na umasikini bara lakini sio Zanzibar. Wakifanya hivyo watakuwa wanaingilia uhuru wao.

Hivi kweli unataka JMT iwajengee shule, iwapangie yatakayofundishwa katika shule hizo, iajiri walimu wa kufundisha katika shule hizo? Unataka JMT iwajengee dispensari, hospitali na iwape dawa na madaktari na manesi wakuwahudumia?

Hauoni hiyo ndio itakuwa kuigeuza Zanzibar kuwa kama Rukwa? Wanatakiwa kusimama wenyewe na kutumia rasilimali zao vizuri ili ziwaletee maendeleo. Hilo ni jukumu la SMZ sio JMT au Oman.

Amandla...
 
Uchumi na umasikini vinaenda pamoja kwa mfano GDP per capita ni moja ya njia ya kujuwa uchumi uko vipi. Huwezi kusema serikali ya JMT inasimamia uchumi lakini haisimamii kupunguza umasikini. Ni vitu haviendani. Sasa leo Tanzania GDP per capita (wastani wa kipato cha mtu kwa mwaka) ni USD 2,000 lakini ya Oman ni USD 30,000. Sasa kwa umasikini wa leo wa Wazanzibari, ni bora wangekuwa raia wa Tanzania au Oman?
 
Unakosea tena. Imethibitishwa kuwa GDP per Capita sio kipimo sahihi cha hali ya wananchi. Marekani ina GDP per Capita kubwa lakini katika indicators za maendeleo kama afya ya wananchi wake iko nyuma ya Cuba. Kwa sababu hiyo hata wangekuwa sehemu ya Oman, hamna uhakika kuwa hali ya wananchi wake ingekuwa bora kuliko sasa.

Aidha, Pemba ambayo ni sehemu ya Zanzibar ni maskini wa kutupwa ingawa wao ndio wanaozalisha karafuu nyingi kuliko Zanzibar. Serikali yao ( iliyokuwa na waunguja wengi) ilifanya juhudi za wazi kuwanyima Pemba maendeleo ya aina yeyote. Waliwanyima nafasi za masomo, uongozi katika serikali na walifikia mahali kumtilia fitna Salim Ahmed Salim kupata nafasi ya kugombea urais wa JMT kwa sababu tu ni mpenda. Yote haya yalifanyika ingawa Mwalimu alimtaka sana awe Rais.

Chimbuko la CUF kuwa na nguvu zaidi Pemba ni dhulma waliyokuwa wanafanyiwa na waunguja na sio dhulma ya machogo. Dhulma na uonevu huu unaendelea mpaka leo. Kwa hali hiyo bado utalaamu serikali ya JMT kwa umaskini wa Pemba?
Zanzibar wameshindwa kuendeleza bandari yao ingawa wana Mamlaka yao wenyewe ya Bandari. Wana shirika la Bima, benki yao n.k. lakini yote wameyadumaza. Walikuwa na viwanda lakini navyo vimekufa.

Matatizo na umasikini wao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubadhirifu, ufisadi na uzembe wa baadhi ya watu waliowaamini. Chuki dhidi ya wapemba nayo imechangia maana bila shaka utajiri mkubwa waliokuwa nao Tanganyika wangewekaza kwao kama sio hizo chuki.

Amandla....
 

Oman ni nchi masikini? Raia wa Oman na raia wa Tanzania wa Zanzibar ni yupi amezidi umasikini? Wazanzibari wangejiunga kabisa na Oman wakapewa na uraia leo wangekuwa na umasikini walionao? Ndiyo maana mwanzo nilisema wengi waliyajutia mapinduzi na baadaye walijuta na Muungano.
 
Nisome vizuri. Sijasema Oman ni nchi maskini. Nimesema nchi kuwa na GDP per Capita kubwa haina maana wananchi wake wote wana maisha bora.
Kwa mantik yako, watanganyika wengi wanajuta kupata uhuru maana wangekuwa bado sehemu ya empire ya Uingereza maisha yao yangekuwa bora kwa sababu Uingereza ni nchi tajiri.

Mapinduzi yalifanyika kwa sababu ya dhulma ambayo baadhi ya wazanzibari ( pamoja na waarabu wa Umma) waliona watawala wao wenye damu ya kiomani walikuwa wanawatendea. Wanaosema kuwa maisha yalikuwa bora chini ya usultani ni wale tu waliofaidika nao na sio wale waliokuwa wanahesabiwa kama watwana.

Amandla...
 
Sovereignty inajengwa pamoja na vitu vingine na:
1. Rais
2. Katiba
3. Wimbo wa taifa
4. Bendera ya taifa
5. Mipaka ya nchi
6. Bunge (kwa Znz Baraza la Wawakilishi na Baraza la Mapinduzi)
7. Vikosi (kwa Znz KMKM na Valantia)
8. Uanachama wa FIFA (sijui)
9. Uanachama ktk jumuiya za kimataifa (OIC inahusika pia)
10. Serikali (governance)

Tanganyika ina vitu vingapi katika hivyo hapo juu? SMZ ina vitu vingapi katika hivyo hapo juu?

Tupate uelewa mwingine toka kwa mwingine, tuko tayari kujifunza.
 
 
Zanzibar inabidi wajifunze kutoka kwa Quebec Canada. Quebec ilikuwa kila siku inalalamika kuonewa kwa sababu wao lugha yao ni kifaransa wakati Rest of Canada (ROC) wanatumia kiingereza. Pamoja na kupewa upendeleo mkubwa, wanasiasa wao (wakiongozwa na Parti Quebecois)walidaii kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi wakiwa nje ya Canada. Mwaka 1980 ikaitwa referendum na waliotaka kujitoa wakashindwa vibaya.

Ikaitwa nyingine 1995, lakini bado wakashindwa. Mwaka 1995 hawakushindwa vibaya kama mwaka 1980, baada ya kusema kujitenga kokote ni lazima uwe pamoja na makubaliano ya uhusiano maalum na wa upendeleo kati yao na ROC maana walijua talaka tatu ingewasababishia matatizo makubwa ya kiuchumi. Hivi hivi kwa Zanzibar. Inabidi waangalie kwa macho makavu faida na hasara watakayoipata Zanzibar ikiwa kama Kenya katika mahusiano na Tanzania. Upuuzi wa kuwa wa Oman na waarabu wengine watawamwagia mapesa kibao waachane nao.

Muigereza alipodai Brexit aliamini nchi Marekani itawakumbatia kwa kuingia nao mikataba maalum ya kibiashara. matokeo ni Wamarekani wamewaambia kuwa wao kipaumbele ni ushirikiano na E.U kibiashara na sio Uingereza ambao uchumi wake ni kiduchu ukilinganisha na wa E.U. Leo Uingereza wana shida ya mafuta na kuna uwezekano mkubwa kuwa hali ya chakula itakuwa mbaya itakapofika mwisho wa mwaka kwa sababu tu hawana madereva wa kutosha wa kusafirisha mafuta na bidhaa zao.

Wachina wana usemi, " uwe mwangalifu sana unachomuomba Mungu kwa sababu anaweza kukupa unachokiomba".

Amandla...
 


Kwani huo ni Muungano au Uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar ???
 

Kuna Mquebec aliwahi kuuwawa , kunajisiwa kuchukuliwa mali yake , kujeruhiwa kwa risasi na Mcanada yeyote ??

Nadhani nyinyi watanganyika mjifunze kuwa huu si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar.
 
Nyerere ndio chanzo cha Matatizo yote haya,sijui alikuwa na lengo gani kuweka Muungano wa kidwanzi hivi.


Nyerere alishapinduliwa na wanajeshi , ni Waingereza ndio walimweka madarakani na mzungu hawezi kukuweka bure madarakani isipokuwa ana masharti yake na malengo yake
 


Nchi haijengwi kwa kuweka makambi ya majeshi kila mtaa , vituo vya polisi na usalama wa taifa kila unapotembea . Haya majeshi ya Tanganyika ya kazi gani ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…