Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Wale wenye access na Plus TV, watch now kipindi cha Uso kwa Uso, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman asema uongo wa wazi wa mchana kweupe kuhusu muungano wetu.

Mhe. Masoud anadanganya u kuwa Tanganyika na Zanzibar tulipoungana, ile 1964, ni nchi moja tuu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ndio pekee iliyopoteza sovereignity yake na kuikabidhi kwa Jamhuri ya Tanganyika, lakini Tanganyika haikupoteza sovereignity yake, bali Tanganyika ilibadili tuu jina kutoka Tanganyika kugeuka Tanzania with its sovereignity, kitu ambacho sii kweli!.

Kiukweli kabisa Tanzania bado tunahitaji sana civic éducation kuhusu huu muungano wetu, hata kwa baadhi ya Viongozi wetu, hawaujui vizuri huu muungano wetu hivyo wanapotosha bure watu wao na umma kwa ujumla.

Msingi mkuu wa muungano wetu ni dhima, kuwa sisi Watanzania ni ndugu moja, sisi ni wamoja, hivyo muungano ni kurudisha tuu asili yetu iliyotenganishwa na wakoloni. Dhima hiyo ndio ikatumiwa na Nyerere na Karume kuasisi huu muungano uliopo hadi leo. Hivyo anapoibuka kiongozi yeyote kutaka kuipotosha hii Dhima, Wazalendo tuliopo tunaoujua ukweli huu hatuwezi kunyamaza !.

Ukweli ni kuwa, tulipoungana ile 1964, nchi zote mbili, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, nchi zote mbili zilipoteza sovereignity zake, kwa Zanzibar kupoteza sovereignity yake na kuikabidhi kwa Tanzania, la Tanganyika pia sio tuu ikapoteza sovereignity yake, bali hadi jina lake la Tanganyika na kuikabidhi kwa Tanzania. Tukaunda taifa moja jipya la Tanzania lenye nchi mbili ndani yake na zote hazina sovereignity zake. Nchi iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikawa haipo tena na nchi ya Jamhuri ya Tanganyika pia ikawa haipo, kilichopo ni nchi moja mpya ya JMT, ambayo ina sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Mimi sitatizwi na uongo wowote wa kawaida ambao hauna madhara, lakini uongo mkubwa kama huu, kuhusu muungano wetu adhimu, na kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama hiki, aliyekuwa mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, huu ni uongo wenye madhara makubwa kwa mustakabali mwema wa muungano wetu. Uongo kama huu una kitu kinachoitwa "ill motives" kwenye "the reasons or motivés behind" Jee lengo la uongo huu ni nini?.

Wakati wa Bunge la Katiba, niliwahi kutoa angalizo hili kuhusu mtu huyu
na kweli Dr. Shein alimshughulikia.

Muungano wetu ni muungano wa nchi mbili zenye hadhi sawa sawa, hakuna mkubwa wala mdogo, ndani ya muungano Tanganyika na Zanzibar ziko sawa sawa na zote mbili zilipoteza sovereignity zake na kuikabidhi kwa serikali ya JMT.

Muungano wetu ni aina ya muungano very unique duniani, kimataifa muungano wetu ni union wa nchi mbili zimeungana na kuunda nchi moja ya Tanzania. Hivyo Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, ni taifa moja, ni dola moja yenye rais mmoja, rais wa JMT ambaye ni Samia. Pia tuna Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu. Kimataifa Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa nchi mbili, yaani federation, hivyo ndani ya muungano, Zanzibar ni nchi, yenye rais wake, serikali yake, ina katiba yake, ambayo mabadiliko yaliyofanywa 2010 kuunda SUK, hayatambuliwi na katiba ya JMT. Kwa vile ndani ya muungano Zanzibar ina mamlaka yake huru bila kuingiliwa na serikali ya JMT, la katiba hiyo ni kwa ajili ya mambo yake ya ndani, japo katiba hiyo iko kinyume cha katiba ya JMT, lakini kwa vile ni ya ndani ya Zanzibar,

Kwa upande wa GNU au SUK,
ni serikali ya coalition. Kwenye coalition zote kuna the majority na a minority. A minority ndani ya coalition anatekeleza sera za à majority. Hivyo Viongozi wa ACT ndani ya serikali ya SUK ya Zanzibar, wanatekeza sera CCM.

Hivyo Viongozi wote wa ACT Wazalendo waliomo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar wanapaswa kuhubiri na kutekeleza sera za CCM, hivyo hata wanapoalikwa popote kwenye public, watatanguliza maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa sera za chama tawala.

Sasa mtu huyu ndio yuko ndani ya nyumba, yuko jikoni kabisa, asipothibitiwa, amini usiamini, amini nawaambieni akija tokea kufika kule juu kileleni, very soon, tutagawana fito!.

Paskali
 
Sasa mtu huyu ndio yuko ndani ya nyumba, yuko jikoni kabisa, asipothibitiwa, amini usiamini, very soon, tutagawana fito!.
Paskali weka sawa hapa;

Sina access na hiyo tv but makamu wa pili wa rais Mh. Hemed Suleiman ni mwanaCCM na makamu wa kwanza wa rais Mh. Othman Masoud ni ACT ambaye ndiye alikuwa mwanasheria Mkuu wa serikali kipindi hicho.
 
Kwanza rekebisha. Jee in makamo was kwanza au wa Pili. Kwenye mada.
Mtoa mada wewe ni mkereketwa ulie na chuki zilizojificha dhidi ya Zanzibar.

Kujificha nyuma ya kiini macho cha Tanzania wakati unajua fika by practice na reality kilichoondoka ni neno Tanganyika tu.

Hakuna Muungano huu. Wizara za Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika zinaitwa za Tanzania.

Kibaya zaidi kumezaliwa matatizo kibao ya Muungano Leo zinaitwa kero. Lkna shida ni mfumo na muundo. Linapokuja suala LA haki za Zanzibar, wasomi wote wa Bara na wachambuzi wanakuwa wanafiki.

Nini kimejificha nyuma ya chuki hii?
 
MPE walau heshima take ya Umakamu was Rais.

Ficha chuki zako binafsi. Hebu pitia tena hayo maandishi yako, yahakiki vizuri wewe in mwandishi Mkongwe uone ulivyotumia maneno ya kubeza.

Nadhani umenielewa
 
Kwanza rekebisha. Jee in makamo was kwanza au wa Pili.
Kwenye mada.
Mtoa mada wewe ni mkereketwa ulie na chuki zilizojificha dhidi ya Zanzibar...
Eti mkuu, hivi ugumu wa kujitenga na kullirudisha Taifa lenu lililomezwa na Tanganyika, uko wapi?

Imagine Rais wa Tanganyika kwa sasa ni Mzanzibari mwenzenu! Kwa nini msimshawishi auvunje huu Muungano ili Visiwa vyenu vigeuke na kuwa Dubai ya Afrika?
 
Maelezo mengi sijaona ukiifafanua Zanzibar inatambulikaje?

Ni nchi ama mkoa ama yenyewe ni sehemu tu ya Tanzania?

Tuna waziri mkuu ambaye miaka humuoni hata Zanzibar..naye tunasema ni waziri wa JMT.

Tuna bunge la JMT ambao mawaziri wake wanawajibika TZ tu..spika na naibu wake nao ni wa hapa hapa.

Inapokuja masuala mengine ya Zanzibar kuamua kama nchi, tunawaambia hapana.
 
Paskali weka sawa hapa;

Sina access na hiyo tv but makamu wa pili wa rais Mh. Hemed Suleiman ni mwanaCCM na makamu wa kwanza wa rais Mh. Othman Masoud ni ACT ambaye ndiye alikuwa mwanasheria Mkuu wa serikali kipindi hicho.
Asante sana, anayezungumza ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe
Othman Masoud Othman Sharrif sio Makamo wa Pili.

Naombeni sana mnisamehe kuwachanganya hawa Makamo wawili, hivyo vyeo vya Zanzibar ambayo havitambuliki ndani ya katiba ya JMT, vinatuchanganya sana sisi waumini wa supremacy ya Katiba. Kama katiba yetu ya JMT haiwatambui Makamo hawa, who M I nisiwachanganye ?

Mixing is highly regreted. Mode please do the needful.
P
 
Wanabodi
Wale wenye access na Plus TV, watch now kipindi cha Uso kwa Uso, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman asema uongo wa wazi wa mchana kweupe kuhusu muungano wetu.

Masoud Masoud anadanganya uongo kuwa eti tulipoungana, ile 1964, ni nchi moja tuu ya Zanzibar, ndio pekee iliyopoteza sovereignity yake na kuikabidhi kwa serikali ya Tanganyika, lakini Tanganyika haikupoteza sovereignity yake, kitu ambacho sii kweli.

Ukweli ni kuwa, tulipoungana nchi zote mbili, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, nchi zote mbili zilipoteza sovereignity zake, kwa Zanzibar kupoteza sovereignity yake na Tanganyika pia ikapoteza sovereignity yake, tukaunda nchi moja mpya ya Tanzania. Nchi ya Zanzibar haipo na nchi ya Tanganyika pia haipo, kilichopo ni nchi moja mpya ya JMT, ambayo ina sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Mimi sitatizwi na uongo wowote wa kawaida ambao hauna madhara, lakini uongo mkubwa kama huu, kuhusu muungano wetu adhimu, la kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama hiki, ni uongo wenye madhara makubwa sana kwa mustakabali mwema wa muungano wetu ambao una ill motives behind. Jee lengo la uongo huu ni nini?.

Wakati wa Bunge la Katiba, niliwahi kutoa angalizo hili kuhusu mtu huyu
na kweli Dr. Shein alimshughulikia.

Muungano wetu ni muungano wa nchi mbili zenye hadhi sawa sawa, hakuna mkubwa wala mdogo, ndani ya muungano Tanganyika na Zanzibar ziko sawa sawa na zote mbili zilipoteza sovereignity zake na kuikabidhi kwa serikali ya JMT.

Muungano wetu ni aina ya muungano very unique duniani, kimataifa muungano wetu ni union wa nchi mbili zimeungana na kuunda nchi moja ya Tanzania. Hivyo Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, ni taifa moja, ni dola moja yenye rais mmoja, rais wa JMT ambaye ni Samia. Pia tuna Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu. Kimataifa Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa nchi mbili, yaani federation, hivyo ndani ya muungano, Zanzibar ni nchi, yenye rais wake, serikali yake, ina katiba yake, ambayo mabadiliko yaliyofanywa 2010 kuunda SUK, hayatambuliwi na katiba ya JMT. Kwa vile ndani ya muungano Zanzibar ina mamlaka yake huru bila kuingiliwa na serikali ya JMT, la katiba hiyo ni kwa ajili ya mambo yake ya ndani, japo katiba hiyo iko kinyume cha katiba ya JMT, lakini kwa vile ni ya ndani ya Zanzibar,

Sasa mtu huyu ndio yuko ndani ya nyumba, yuko jikoni kabisa, asipothibitiwa, amini usiamini, amini nawaambieni akija tokea kufika kule juu kileleni, very soon, tutagawana fito!.

Paskali
Samahani ni makamu wa Kwanza au wa pili?

Maana ulisema wa Kwanza ndio Yule aliyetokea ACT na ndio alikuwa mwanasheria wa Dr shein wa pili ni huyo wa CCM jina silikumbuki vzr hebu tusaidie

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom